Nimemkataa baba mzazi, na sitaki kupima DNA

Nimemkataa baba mzazi, na sitaki kupima DNA

kwakweli umekosea sn kukataa kupima DNA. Pia ujue ukweli coz hii haitaathiri respect ambayo unampa huyo baba aliekulea. Pia inabidi uwajue pia shangazi zako, babazako wadogo na hata ndugu zako wengine kutoka upande wa biological father. Ukweli haukimbiwi ndugu yangu bali unatafutwa. Nafkri mama mzazi inabidi akutake maana amekukosea kama ni ukweli.
 
Nimekusoma kwa makini na nimeamini kweli wewe ni msomi na unajua namna ya kupambanua mambo.Maamuzi uliyoyatoa ni sawa na Mwenyezi Mungu akujalie hekima katika maisha yako nijuavyo mama kwa hasira alikuwa anamkomoa yule mumewe kwa hasira alizokuwa nazo
Ila nakubaliana kabisa kwamba inawezekana asiwe biological father ila kuwa au kutokuwa sio jambo la msingi kikubwa ni upendo na kujali ndio kipimo cha baba mwema
 
Umefanya vzr ssna., na hiyo baba aliekulea zidisha upendo na kumthamin na kua karibu nae zaidi kwa sababu hapo alipo ana uchungu wa kuambiwa maneno mabovu na huyo mama nahis ameumia kweli juu ya hiyo taarifa kua si mtoto wake. Mpende baba mlezi, mthamini, mjali na kila utakapomtazama endelea kuona kuwa huyu ndio baba mzazi.
 
Sijui niseme au ninyamaze kusema ngoja nitafute la kusemea hapa

ila mkuuu pole sana kwa hayo yaliyokukumba ni makubwa sana
 
yan ni sawa kabisa. na hakuna cha laana wala tambiko. huyo jamaa alitia mbegu tuu akasepa zake. ni kama mwanamke. akizaa tuu alafu amtupe mtoto angali kichanga kisha mwanamke mwingine amuokote amnyonyeshe na kumkuza laana itakayo kubalika hapo ni ya huyo alomnyonyesha na si ya huyo alozaa.

Sperm donor
 
Je waungwana nilichofanya ni makosa?

Wala, tukumbuke, baba hasa ni yule aliyemtunza mtoto, kumfundisha, kumlea, mpaka ukawa mtu mzima namna huyo, sasa tukisema umkane huyu aliyekutunza wengine tunaona sio haki, ila huyo wanamsema kuwa ndio baba yako sio mbaya pia kumjuwa kama ni kweli, uamuzi juu yako, lakini sidhani kama atabadilisha mawazo yako ya jinsi unavyowathamini wote, kwani ukipata kuwa na wazee wawili wa kiume wenye busara zao ambao wote ni baba zako kuna ubaya gani?
Ila kama ulivyodai hapo juu, ugomvi wa wazee sio wako, ila kama kuna ukweli basi uujuwe..
 
Mimi nina miaka 38 sasa, msomi wa elimu ya juu na nina kazi nzuri pia, nilikuwa naishi vizuri na wazazi wangu wawili I mean baba na mama, sasa hapa juzi baada ya ugomvi, mama ameondoka nyumbani na kuniambia eti baba nilienae sio baba yangu biological na baada ya kikao kirefu nimeonyeshwa baba mwingine wanaomsema ndio baba biological ila mbele ya watu wote nilimkana na kumwambia asinijue kabisa na wala sitaki kuharibiwa maisha yangu.

Mimi nina baba yangu ambae amenilea na ndio naamini ni baba halisi kwangu, sasa wanakazania DNA mimi nikasema sitaki chochote na nisiingizwe kwenye ugomvi wa wazazi wangu na ninampenda sana baba yangu alienilea kwasababu amenisomesha shule za gharama na amenitembeza duniani na kunipa kila nilichotaka mpaka hapa nilipo namwona kama mtu namba moja muhimu kwangu hapa duniani.

Je waungwana nilichofanya ni makosa?

Majibu uliyompa mama yako ni murua kabisa, unajua kwa nini, mama yako alivyo mwagwa akaona naye amwage mboga. Nataka ujue kwamba ungekuwa ni tahira tahira siku anamwagwa angeondoka huku akimwambia baba yako "naondoka wewe kaa na toto lako hilo taahira" wala hungemjua biological father, achana na mama yako songa mbele na "dereva" aliyekufikisha hapo.
 
Kijana Baba yako mwenyewe unamjua! Maana kwa maelezo yako inaonekana kabla ya ugomvi hukuwahi ambiwa hayo! Nakushauri mpende na kumheshimu baba yako wa kwanza (aliye kulea, kusomesha n.k) huyo mwingine (wa pili nasema wapili kwa kuwa umemfahamu ukubwani) mchukulie kama jirani (mzee jirani yenu) au huwa huheshimu wa wazee majirani zenu? Basi kama unawaheshimu wazee majirani zako hivyo hata huyo unaambia ndo baba yako wa kibaiolojia mheshimu pia kwani mara nyingi kwa waliojaliwa wenye busara ikibidi huwasaidia wazee wanapohitaji msaada na siyo tu mpaka awe baba yako. Na USIKUBALI KUPIMWA DNA maana wewe huna shida ya baba. Kama wao wangekuhitaji wangelishughulikia mapema.

KWANI HUMU HAMMO AMBAO MNAZAA NJE? FUNDISHO. JIFUNZENI
 
Nini maana ya baba by the way?? Huyo baba ulipaswa kumkata makofi *****. Wewe usome,uishi miaka yote yeye yupo tuu na tezi zake!! Dah mie ningemkata makofi.
 
Aisee huyo mama yako anastahili adhabu, yaani anaongeza makosa juu ya makosa, kwanza alichepuka kwenye ndoa, pili kambambikizia mtoto mumewe, tatu kalikoroga tena baada ya kukosana. Uamuzi ulioufanya ni wa busara sana ila dhambi hii bila huyo mama yako kuiweka sawa itamtafuna mpaka anaingia kaburini!
 
Nini maana ya baba by the way?? Huyo baba ulipaswa kumkata makofi *****. Wewe usome,uishi miaka yote yeye yupo tuu na tezi zake!! Dah mie ningemkata makofi.

Hahahaha...kaja na tezi zake kimbele front...tehetehe..

Yaani hilo baba jinga kweli, mwenzie kalea mpaka mtoto kawa mkubwa ndo linaibuka kaa kambalee...
 
Ulichoamua ni kizuri lakini nina ushauri kidogo juu ya hilo suala, Wanawake wamekuwa wakipoteza asili ya vijana wengi sana kwa kuingiza chuki na ugomvi binafsi na wazazi wenzao na kuupandikiza kwa watoto, Umeshakuwa mtu mzima sasa na wewe pia huenda una watoto wako, sasa kama baba mwenye busara tafuta uhalisia wa asili yako, tambua baba yako mzazi na ndugu zake wengine kwani kule ndio kwenu kabisa na usimkate baba mzazi kwa kuwa tuu amechoka kimaisha tofauti na huyo aliekulea.

Usiruhusu ugomvi wa wazazi ukakuteka ila tumia hiyo nafasi kujitambua zaidi maana uzembe wako katika hilo utaathiri na watoto wako na vizazi vitakavyofuatia. Wote ni wazazi wako brother huyo wa kukuzaa na huyo wa kukulea, wapokee ishi nao kwa upendo, wasaidie na kamwe usimtupe aliekulea maana nae ana mengi amefanya na kuvumilia juu yako pia mama yako nae usimtupe, ndio maana Mungu kakuumba mwanaume ili utumie busara na hekima kutatua huo mgogoro na changamoto. Mimi nakupongeza kwa kufanikiwa kuujua ukweli ukiwa hai na hasa ukiwa na nafasi ya kurekebisha kizazi chako.

Mimi nina miaka 38 sasa, msomi wa elimu ya juu na nina kazi nzuri pia, nilikuwa naishi vizuri na wazazi wangu wawili I mean baba na mama, sasa hapa juzi baada ya ugomvi, mama ameondoka nyumbani na kuniambia eti baba nilienae sio baba yangu biological na baada ya kikao kirefu nimeonyeshwa baba mwingine wanaomsema ndio baba biological ila mbele ya watu wote nilimkana na kumwambia asinijue kabisa na wala sitaki kuharibiwa maisha yangu.

Mimi nina baba yangu ambae amenilea na ndio naamini ni baba halisi kwangu, sasa wanakazania DNA mimi nikasema sitaki chochote na nisiingizwe kwenye ugomvi wa wazazi wangu na ninampenda sana baba yangu alienilea kwasababu amenisomesha shule za gharama na amenitembeza duniani na kunipa kila nilichotaka mpaka hapa nilipo namwona kama mtu namba moja muhimu kwangu hapa duniani.

Je waungwana nilichofanya ni makosa?
 
Uhalisia huwa haupingwi hata siku moja...

Watu wanakwepa kumwambia ukweli...

Baba yako ni baba yako tu hata kama alikuacha wapi, haijalishi ulilelewa na mfalme ama rais bado asili yako ni kwa yule baba yako na huyu mwingine atabaki kuwa baba "mlezi" (wengine wanasema wa kufikia)
 
Kula tano. Huyo jamaa wanayedai ni biological father ni "sperm donor" tu na watu kama hao wapo wengi tu duniani. Baadhi ya hospitali Ulaya wana utaratibu wa kununua "sperm" toka kwa wachangiaji mbalimbali na kuziuza kwa akina mama wenye kuhitaji watoto kwa masharti kuwa mtoaji hatakiwi kujulikana ni nani.

Baba wa kweli ni huyo aliyekufahamu toka utotoni, kukutunza, kukupenda na kukulea.
Huyo playboy ni kama walivyosema wengi humu, ni sperm donor na hana uchungu wala upendo kwako. Inasikitisha mno kwamba mama yako amekuwa mkatili kiasi hicho
yaani kiasi cha kuwaumiza wewe na baba yako. Mkatae huyo wa kubumbwa kwa nguvu zote na huna haja ya eti kupika DNA! Sasa ndiyo wakati wa kuwa na mshikamano mkubwa zaidi na baba yako uliyemjua kuliko wakati wowote.
 
Kula tano. Huyo jamaa wanayedai ni biological father ni "sperm donor" tu na watu kama hao wapo wengi tu duniani. Baadhi ya hospitali Ulaya wana utaratibu wa kununua "sperm" toka kwa wachangiaji mbalimbali na kuziuza kwa akina mama wenye kuhitaji watoto kwa masharti kuwa mtoaji hatakiwi kujulikana ni nani.
Kwa hiyo mkuu kama ni kweli unadhani inabadilisha ukweli kuwa huyo ndiye "biological father". Angalia hata lugha uliyotumia "biological", hilo neno lina maana kubwa sana vinginevyo kwanini hakuandika father peke yake?? kwani haitoshi. Ila kwa mimi ningekaa kimya tu.
 
Mimi nina miaka 38 sasa, msomi wa elimu ya juu na nina kazi nzuri pia, nilikuwa naishi vizuri na wazazi wangu wawili I mean baba na mama, sasa hapa juzi baada ya ugomvi, mama ameondoka nyumbani na kuniambia eti baba nilienae sio baba yangu biological na baada ya kikao kirefu nimeonyeshwa baba mwingine wanaomsema ndio baba biological ila mbele ya watu wote nilimkana na kumwambia asinijue kabisa na wala sitaki kuharibiwa maisha yangu.

Mimi nina baba yangu ambae amenilea na ndio naamini ni baba halisi kwangu, sasa wanakazania DNA mimi nikasema sitaki chochote na nisiingizwe kwenye ugomvi wa wazazi wangu na ninampenda sana baba yangu alienilea kwasababu amenisomesha shule za gharama na amenitembeza duniani na kunipa kila nilichotaka mpaka hapa nilipo namwona kama mtu namba moja muhimu kwangu hapa duniani.

Je waungwana nilichofanya ni makosa?

Hujafanya makosa kaka, upo sahihi kabisa. "Fatherhood does not determined by DNA. It is determined by RESPONSIBILITIES!!!! Remember " ANY FOOL WITH A D.ICK CAN MAKE A BABY, BUT ITS ONLY A REAL MAN WHO WILL TAKE CARE OF HIS FAMILY ". Kuwa na uvimbe mrefu katikati ya miguu hakumfanyi mtu kuwa mwanaume.
 
Back
Top Bottom