Nimemkataa baba mzazi, na sitaki kupima DNA

Nimemkataa baba mzazi, na sitaki kupima DNA

Congratulations! You made the right decision Madame.
 
Uhalisia huwa haupingwi hata siku moja...
Uhalisia ni kuwa huyu jamaa amelelewa na kukuzwa na BABA yake mzazi ambaye kwa miaka yake yote amekuwa akimjua. Huyu mwingine ambaye amesubiri mpaka kutokee ugomvi baina ya wazazi wa huyu jamaa ni mharibifu endelevu tu. Kwanza amempa mimba mke wa mtu kinyume na taratibu (Uharibifu wa kwanza), na sasa anataka kuharibu uhusiano uliopo kati ya mama, mtoto aliyemleta duniani kinyume na taratibu na BABA ya mtoto ambaye alimlea, kumtunza na kumsomesha mtoto mpaka alipofikia. Kwa hiyo kuihalisia huyu baba fake angeendelea tu kuwa underground kwani ndipo kunapomstahili
 
sabudi

What else do you think you should do? Hayo mengine ni mambo ya Ngoswe...ya ngoswe muachie ngoswe mwenyewe
 
Mama kakuficha miaka yote hiyo?
Kweli dunia haiishi maovu....i woudn't forgive my mother for that..
Hata hivyo, baba mlezi ndiye baba yako..huyo mwingine ni donor tu.

Mkuu unashangaa miaka mingi' ila kwa huku mitaani tunawajua wa mama dizain hiyo wengi sana.
 
Sawa kabisa, your biological father is irrelevant. Alikuwa sperm donnor maybe, kwanini asikulee, kwanini aibuke sasa, kwanini alisepa. kwako wewe baba halisi ni huyo unaemjua toka miaka kadhaa iliopita. DNA haisadii chochote kwasasa kitu cha muhimu ni uhusiano wako na mzee unaemjua wewe, zaidi ni kukutia stress za bure.
 
Huyo mamako naye ana roho ngumu kuzaa nje na kumdaganya mwenzie miaka yote mwanaume analea kumbe wa mwanaume mwenzake cha msingi waheshimu wote hata huyo really father alikua wapi
 
Bigupaliekulea ndiye baba kuzaa hata mbwa anazaa . Aliyekulea ndiye alikufanya wewe uwe mtu leo. Ndiye baba wa kweli ungekufa angesema hili ni kaburi la mwanangu?asikuzoooe
 
Mimi nina miaka 38
sasa, msomi wa elimu ya juu na nina kazi nzuri pia, nilikuwa naishi
vizuri na wazazi wangu wawili I mean baba na mama, sasa hapa juzi baada
ya ugomvi, mama ameondoka nyumbani na kuniambia eti baba nilienae sio
baba yangu biological na baada ya kikao kirefu nimeonyeshwa baba
mwingine wanaomsema ndio baba biological ila mbele ya watu wote
nilimkana na kumwambia asinijue kabisa na wala sitaki kuharibiwa maisha
yangu.

Mimi nina baba yangu ambae amenilea na ndio naamini ni baba halisi
kwangu, sasa wanakazania DNA mimi nikasema sitaki chochote na
nisiingizwe kwenye ugomvi wa wazazi wangu na ninampenda sana baba yangu
alienilea kwasababu amenisomesha shule za gharama na amenitembeza
duniani na kunipa kila nilichotaka mpaka hapa nilipo namwona kama mtu
namba moja muhimu kwangu hapa duniani.

Je waungwana nilichofanya ni makosa?

da mama wengine majanga ivi mtu kakulea miaka iyoo yote leo eti analetwa mjinga mwingine? imeniuma
 
sabudi.

Baba ama 'ubaba' unatokana na kutimiza majukumu ya kuwa mlezi wa kiroho na kimwili. Kuzaa kibaolojia hata wanyama huzaa na wasiwe na habari na watoto wao.

Ingawa kuna mambo yananipa shaka juu ya uamuzi wako, huyo mzazi wako 'mpya' ulipata muda wa kumsikiliza au walau kumhoji kwanini hakujitokeza siku zote... Labda ana sababu za msingi ima aliepuka kuharibu ndoa ya mamayo kipenzi.

Kwanini msisitizo umeuweka kwenye ubora wa baba wako wa siku zote kwa vigezo vya kusomeshwa shule za gharama na kutembezwa mahala tofauti duniani? Unanipa imani kuwa kinachoendelea hapo ni falsafa ya 'mtu-kitu', yaani ubora wa mtu kupimwa kwa aliyotekeleza kutokana na uwezo wake kifedha.

Vipi kama angekuwa amekusomesha shule za kawaida na sehemu pekee aliyokutembeza kuwa kijijini kwenu, bado ungekuwa na ujasiri wa kufungamana nae na kumkana waziwazi huyo mshua mpya?
 
Last edited by a moderator:
Hakuna sababu ya kuharibu mahusiano yaliyodumu kati yake na babaye wa kufikia....

Pamoja na kufanya hivyo bado haiondoi uhalisia kuwa damu yake ni sehemu ya huyo mzee mwingine...

Waungwana huwa wanasema mwana hawezi mkana mzazi maana ni laana hiyo...

Hata hivyo hapa hatujaelezwa sababu ya kutoishi na babaye mzazi ni ipi?

Wewe ndugu yangu mbona unamambo ya ajabu ajabu sana. Alikuwa wapi all that time 38years, aje leo na suruali yake kwenye maisha ya grown up human being.

Hiyo misemo misemo ni wazee wa zamani na si ya waungwana, uungwana uko wapi hapo 38years then unakuja kusema wewe mtoto wangu huo ni ujinga kabisa.

Kuwa baba au mzazi si kuweka mbegu tu lazima ujue what it take to be a father. Fungua macho na uchangie kwa kufikiri.

Mwisho haina sababu ya kueleza sababu kwanini hakuishi na baba sababu hilo lilikuwa jukumu la huyo mweka mbegu na si la mtoto. Kwa kifupi alisepa majukumu hivyo hastahili hata kuthubutu kuja kusema mimi ni baba yako mtoa mbegu.
 
We ndo kidume kweli kweli. Huyo mama kama kakosana na babako aliyekulea toka kliniki mpaka kote aliko kupeleka, kakapa na jina, ukoo, family tree. Leo mama (shamba) tuu, tena wamama wengine mnisamehe kwa neno hilo. Aje akuambie twende kwa babako. Yupi?? Hana haya kabisa, kwanza anajigamba kuwa yeye ni kicheche?? Jamani, dunia limekwisha nalo lime malizwa na wakaaji wake.
Huyo mamangu angeanzaje?? Babako ni huyo aliyekulea akakusomesha akakujali kwenye shida zoote. Mbegu ni nini?? Mwambie aksante sana kwa mbegu yako ilodondoka njiani tu. Kama anaujua ubaba alitakiwa aulize kliniki sio nyumbani kwa mtu.
Huyo mama anisamehe tu, kama ni DNA akaitoe yeye si weye. Kaa na huyo baba mlezi tena mwambie yeye sio baba mlezi bali babako wengine wakaokote watoto kulee msimbazi mtoni.
 
songa mbele huyo mama mambo yake asiyalete kwako yeye aende kwa huyo mwanaume anayemtaka.
 
Pongezi nyingi mkuu!
Hakuna haja ya kupima DNA, nakushauri ongeza mapenzi na ukaribu kwa uliye muita baba tangu ulipojua kuongea, atakuwa kwenye wakati mgumu sana! Huyo aliye kulea ndio baba yako! Huyo mwingine hastahiri hata nafasi ya kusikilizwa!
 
Back
Top Bottom