Nimemkataa baba mzazi, na sitaki kupima DNA

Nimemkataa baba mzazi, na sitaki kupima DNA

Huyu mama na alaaniwe kabisa. Kesho akigombona na huyo mpya utapata baba mwingine. Akili mu kichwa.
 
"Ni rahisi kuwa baba lkn ngumu kuwa mzazi" nadhani ni fid q!
 
Hongera kwa uamuzi mzuri! Nakushauri baada ya mama kutulia muulize what happened mpaka ikawa hivyo? Yaani ilikuwaje ulelewe na baba mwingine? Utakuta mama ndo alimdhulumu baba yako mzazi haki ya kuwa na wewe na kumpa huyo baba mlezi jukumu la kukulea.

Baba mlezi alikuwa anajuwa kuwa wewe si mwanaye?
 
Mimi nina miaka 38 sasa, msomi wa elimu ya juu na nina kazi nzuri pia, nilikuwa naishi vizuri na wazazi wangu wawili I mean baba na mama, sasa hapa juzi baada ya ugomvi, mama ameondoka nyumbani na kuniambia eti baba nilienae sio baba yangu biological na baada ya kikao kirefu nimeonyeshwa baba mwingine wanaomsema ndio baba biological ila mbele ya watu wote nilimkana na kumwambia asinijue kabisa na wala sitaki kuharibiwa maisha yangu.

Mimi nina baba yangu ambae amenilea na ndio naamini ni baba halisi kwangu, sasa wanakazania DNA mimi nikasema sitaki chochote na nisiingizwe kwenye ugomvi wa wazazi wangu na ninampenda sana baba yangu alienilea kwasababu amenisomesha shule za gharama na amenitembeza duniani na kunipa kila nilichotaka mpaka hapa nilipo namwona kama mtu namba moja muhimu kwangu hapa duniani.

Je waungwana nilichofanya ni makosa?
wewe ni mtu mzima, nitakushauri kama mtu mzima. hautakiwi kumkana baba yako wa damu, huyo ni baba yako. ulichotakiwa kufanya, ni kuwa na moyo mgumu, ungewakubalia kuwa nashukuru nimemfahamu baba yangu wa damu, na niko tayari kupima DNA ili nijue vizazi vyangu yaani watoto wangu wasijeingiliana baadaye na familia ya huyu baba mpya. lakini ungewaambia kuwa, huyo baba wa damu nitamwita baba tu kama kawaida lakini baba ambaye sitamsahau ni huyu aliyenilea na pengine alijua kuwa wewe si mwanae tangu ulipozaliwa lakini alinyamaza.

wazazi wako ndio wanajua kwanini ilitokea hivyo, na waache wazazi wako wenyewe walilijua hilo na ni leo tu wameamua kulianika. ukiona hadi ukoo umeweka kikao ujue watu wazime wameona ni muhimu wewe kumjua baba wa damu ili ukoo wako unyooke usije tembea na dada zako au wajomba zako wa damu. na pengine ulishalala na ndugu zako kwa huyo baba mpya bila kujua, iyo kujua tu ni bahati, shukuru. hiyo ni muhimu kwako kwasababu kufanya mapenzi na dada yako wa damu hata kama haujui ni laana na inaenda hadi vizazi. hivyo wewe kama umekataa, upande wa huyo baba mpya kuna vijana watazaa watoto ambao usipokuwa makini watafanya mapenzi na watoto wako na mtaingiza laana.

ninamfahamu jamaa alikuja kujijua yeye si wa ukoo husika baada ya kuzaa watoto sita. hata watoto walikuwa wanaitwa kwa ukoo wa mtu mwingine wakati wa kubadilisha ilibidi baba na watoto wabadilishe jina la ukoo. inauma lakini ni utoto kujifanya unampenda sana uyo baba aliye kulea ati kwasababu alikulea na kukutembeza nchi kadhaa. unatakiwa kuchukulia mambo kikawaida sio kama mtoto mdogo kiasi icho, au ndio ninyi watoto wa masaki kujifanya ulayaulaya? achana na mbwebwe.

uamuzi ni wako, ukitaka ukoo wako ujulikane na unyooke mkubali baba yako na umheshimu kwasababu usipofanya hivyo laana iko juu yako. vilevile usimsahau huyo aliyekulea endelea kumwita baba na kumthamini kama kawaida. na inawezekana huyo mpya akawa ni baba jina tu lakini ukawa upande zaidi wa huyo wa zamani. mama yako ndio unatakiwa kumlaumu kwanini hakukuambia ulipokuwa mdogo anakuja kusema leo, that means mama yako alikuwa hajatulia, malaya na alitoka nje ya ndoa au alichepuka ukapatikana na ili kulinda ndoa ya huyo aliyekulea alificha. pengine asingeficha hata iyo opportunity ya kutembezwa nchi kadhaa na baba wa zamani usingeipata na pengine baba wazamani angeshamuua mamako, unategema reaction gani baba wa zamani angeichukua mamako angemwambia wewe si mtoto wake? ujue mama alikuwa ameficha na umefika wakati mwafaka kuweka wazi na unatakiwa kulipokea kama lilivyo wewe kama mtu mzima. acha utoto.

kwani huyo baba wa zamani amekuambia nini baada ya hapo?
 
acheni kumpoteza jamaa yenu. anatakiwa kumkubali huyo baba mpya, na apokee jina la ukoo ili atambulike na watoto wake watambulike na kizazi chake kitambulike. asipofanya hivyo kuna hatari watoto wake wakaja kuoleana na watoto wa baba wa damu n.k vilevile, hautakiwi kumlaumu baba aliyefichwa, pengine alikuwa hata hajui, anayetakiwa kulaumiwa ni mama yako ambaye alijua tangu uko mbimba lakini akaficha. hata hivyo, be careful reaction utakayochukua dhidi ya mama yako kwasababu huyo ni mama yako hata kiwa na makosa unatakiwa kuwa na adabu. "waheshimu baba yako na mama yako siku zako zipate kuwa nyingi katika nchi uliyopewa na Bwana Mungu wako", kati ya laana nyingi watu wanapata ni kutoishi vizuri na baba na mama. hivyo mama hata kama ana makosa, don't react as if wewe ni under 18. nakuona una miaka 38 naamini hata akili itakuwa na umri huo. mamako ameishi na jambo hilo gumu moyoni, limemuumiza hadi amelitapika, shukuru kwa hilo. babako mpya amejulikana shukuru ili ujuue ukoo wako na ndugu zako. huyo aliyekulea endelea kuishi naye kama baba mzazi lakini kama adopted tu na umheshimu kwa heshima zote na usimtupe. usimkatae huyo mpya pengine kwasababu unaona masikini labda mamako alimtosa ukiwa mimba kwasababu jamaa alikuwa hana hela sasa huyo aliyekulea alikuwa nazo ndio maana amekupeleka nchi kadhaaa...hahaha, usifanye hivyo. baba ni baba. kuna watu wanatumia hela nyingi sana kumtafuta baba wamjue hata kwa sura lakini wanashindwa. shukuru Mungu umempata babako.
 
Tatizo hapo ni mama ako,hao wazee wawili hawana matatizo...ni vyema ukakaa kimya kuliko kukubali kupandikizwa mbegu za chuki kwa mzee mmoja wapo kwa sababu hawana matatizo,kwa ulivyoeleza tu inaonyesha tena kwa hakika mama ako ni tatizo.
 
Kudos.. you did right pal! Huyo wa DNA mwambie akae na DNA zake. Mambo ya DNA ni non sense, Ukishajua DNA then what?
 
kitanda akizai haramu , kwanza shukuru mungu kwa kuweza kuelewa asili yako au baba halisi,
ni watoto wangapi amabao wameweza kupelekwa kusiko na asili yao ?? ni wangapi wamebambikiwa koo zisizo kuwa zao?? wangapi ambao hadi sasa hawajitambui na huko walikopelekwa hawatambuliki na wananyanyasika???

sidhani kama kuna sababu ya kusimama katika kati ya ugomvi wa wazazi wako maana huwezi kujua nini kilitokea hadi kufikia mama yako kukaa na hiyo siri miaka yote ... na siku zote hasira hasara na vita vya panzi neema kwa kunguru ... hasira za mama yako zimesaidia wewe kuelewa asili yako (baba yako halisi) hilo ni la kushukuru . naamini we ni mtu mzima na wapaswa utumie sana busara katika maamuzi yasije kuathiri familia yako baadae ikajikuta inanyanyasika au kutengwa , elewa huko kwa baba mlezi wameelewa ukweli je mapokeo yao yatakuwaje baad YA MIAKA 5??

cha msingi ukweli umeujua mhesimu baba mzazi na mlezi kila mmoja ana nafasi yake na hata mama yako mpe heshima yake japo kitendo cha kukuficha miaka yote ni kizuri
 
mkuu pole sana,, uko sahihi.... but kwanini mama yako alikuficha mda wote huo!!! je wasingegombana ungejuaje?? Hapo shetani anaaibishwa......... i hate ur mom.......Kaa na baba yako, huyo alikulea, wewe ni mtu mzima sasa, talk to him, yeye aliyajua haya yote kabla au nae yuko gizani.....ila elewa alikulea ndio baba yako haswa mheshimu na mthamini kama ilivyokuwa, huyo mtoa mbegu mchukulie poa tu....akae mbali na wewe. Mama yako msamehe....endelea na maisha.....
 
Nachukia mambo ya kuambiwa nenda kapima dna sijui nini mara nini
 
Nina swali la msingi saaana na ukijibu hili au hao wazazi wakijibu hili basi...

Ugomvi ni wa wazazi hata kama baba yako sio huyo aliyekulea wanataka ukapime ili iweje?? Huyo biological father akulee au???

Mie nadhani huyo mama anataka kumuumiza huyo aliyekulea miaka yoote. Ushauri wangu kwako:

1. usipime kwasababu kama ni kweli huyo aliyekulea sio biological father then ataumia sana for the rest of his life na atajuta kukusomesha na mengine mengi aliyofanya juu yako na hiyo indirectly ni laana flani. So kufanya hivyo utaepusha mengi na ugomvi wao uendelee kwao.

2. Usipime kwasababu unatumika kama chambo katika ugomvi wao huyo aliye kulea aumizwe moyo.. endelea na maisha like it has never happen.
 
Mwenye kosa ni mama...hata hivyo kwa kuwa kila kitu kiko wazi sasa......hakuna namna zaidi ya kuukubali ukweli....Kwa sababu huenda hata huyo baba mlezi ameshajua kuwa wewe si mwanae.....kwa hio hutakiwi ku react as if huyo baba mlezi hajui chochote......On the other side....huku mtaani wanaume tunalea watoto wa wenzetu sana ...more than 50%
 
  • Thanks
Reactions: BPM
umefanya jambo la busara sana..
ila usimchukie mama na wala usidharau mtoa mbegu ila heshima na salute kwake aliyekulea..
 
Umefanya vyema vema mkuu ila usimkatae kuwa na baba wawili sio vibaya msikikilize anasema nini find a place in your heart to forgive him leave your peaceful life ya nini usononeke moyo na grudges ambazo hukuzitafuta wewe.
 
Mimi nina miaka 38 sasa, msomi wa elimu ya juu na nina kazi nzuri pia, nilikuwa naishi vizuri na wazazi wangu wawili I mean baba na mama, sasa hapa juzi baada ya ugomvi, mama ameondoka nyumbani na kuniambia eti baba nilienae sio baba yangu biological na baada ya kikao kirefu nimeonyeshwa baba mwingine wanaomsema ndio baba biological ila mbele ya watu wote nilimkana na kumwambia asinijue kabisa na wala sitaki kuharibiwa maisha yangu.

Mimi nina baba yangu ambae amenilea na ndio naamini ni baba halisi kwangu, sasa wanakazania DNA mimi nikasema sitaki chochote na nisiingizwe kwenye ugomvi wa wazazi wangu na ninampenda sana baba yangu alienilea kwasababu amenisomesha shule za gharama na amenitembeza duniani na kunipa kila nilichotaka mpaka hapa nilipo namwona kama mtu namba moja muhimu kwangu hapa duniani.

Je waungwana nilichofanya ni makosa?

uamuzi sahihi kabisa
 
Uamuzi uliochukua ni sahihi kabisa nami niko kama wewe alie nilea ndiye mzazi halisi hata kama ni mlezi namdhamini zaidi ya Mzazi,,,!!!
 
Back
Top Bottom