NANDERA
JF-Expert Member
- Mar 18, 2014
- 2,023
- 2,492
Je waungwana nilichofanya ni makosa?
inawezekana umefanya makosa maana hatujui kisa wala mkasa. maelezo yako hayanipi premises za kutosha zilizokufanya ufikie uamuzi wako zaidi ya kuwa baba yako amekulea vizuri kwa kukupeleka shule za gharama za nje ya nchi na kwamba unampenda. Imekuwaje mpaka mkafika hapo mlipofika? Ni kwamba mamako alichepuka akakupata huko halafu sasa hivi ndo baba mlezi kajua mpaka wakaachana? au baba alimuoa mama akiwa tayari ashakuzaa wakakubaliana kuficha siri ila kutokana na ugomvi mmoja wao akaamua kumwaga mboga? Au mama alichepuka halafu hakujua mimba ni ya nani kati ya hao mababa wawili ndo maana wanataka DNA ifanyike? Je, huyo baba uliyeletewa sahivi alikuwa na taarifa kuhusu uwepo wako? Pia umesema baada ya vikao kadhaa wameamua ukapime DNA, je kupima huko ni kwa ajili yako au ni sehemu ya usuluhishi wa ugomvi baina ya wazazi wako? sidhani kama kujua umebeba nasaba za nani kati yao kutaondoa heshima na upendo ulio nao kwa baba yako. ni kweli maisha yako yatabadilika kwa namna unavyojitazama lakini si big deal kiasi hicho, itakuwa kwa muda tu. Hakuna binadamu anayekaribisha mabadiliko kirahisi. Halafu kwani wamekwambia umkane baba aliyekulea? unakimbia kivuli chako tu maana hapo ulipo hata kama unajikaza vipi kuna ukweli unaozunguka kichwani kwako juu ya probability ya kuwa mtoto wa flani au flani. Kama umeamua kutopima ili kumkomoa huyo baba mwingine utakuwa unajitesa bure, wala hastahili kukalia moyo wako kwa mfumo wa hasira na kinyongo na chuki. Face reality. Pima tu ujue, ukishajua utapata hisia nzito za kusalitiwa na mamako au na babako mzazi au mlezi kulingana na walivyoshiriki kwenye sakata maana hujatuambia, kisha utalia, utanyamaza na baadae kuamua rationally.