Nimemkataa baba mzazi, na sitaki kupima DNA

Nimemkataa baba mzazi, na sitaki kupima DNA

sabudi

Member
Joined
Aug 22, 2014
Posts
66
Reaction score
92
Mimi nina miaka 38 sasa, msomi wa elimu ya juu na nina kazi nzuri pia, nilikuwa naishi vizuri na wazazi wangu wawili I mean baba na mama, sasa hapa juzi baada ya ugomvi, mama ameondoka nyumbani na kuniambia eti baba nilienae sio baba yangu biological na baada ya kikao kirefu nimeonyeshwa baba mwingine wanaomsema ndio baba biological ila mbele ya watu wote nilimkana na kumwambia asinijue kabisa na wala sitaki kuharibiwa maisha yangu.

Mimi nina baba yangu ambae amenilea na ndio naamini ni baba halisi kwangu, sasa wanakazania DNA mimi nikasema sitaki chochote na nisiingizwe kwenye ugomvi wa wazazi wangu na ninampenda sana baba yangu alienilea kwasababu amenisomesha shule za gharama na amenitembeza duniani na kunipa kila nilichotaka mpaka hapa nilipo namwona kama mtu namba moja muhimu kwangu hapa duniani.

Je waungwana nilichofanya ni makosa?
 
Well kuna vitu umezaliwa umevikuta duniani. Huna nguvu ya kuvibadilisha. Kama ni baba na alikuzaa basi ni baba yako huyo, haijalishi kama alikukimbia.

ILa huyo aliyekulea Heshima yake isibadilike kamwe...Maana kwa tafsiri halisi ya ubaba, huyo ndiye baba yako.

We mkubali tu huyo mwingine lakini isibadilishe mtizamo wako kuhusu huyo aliyekulea. Pia achana na ugomvi wa wazazi mara nyingi ni kuvuna laana tu!
 
Hakuna sababu ya kuharibu mahusiano yaliyodumu kati yake na babaye wa kufikia....

Pamoja na kufanya hivyo bado haiondoi uhalisia kuwa damu yake ni sehemu ya huyo mzee mwingine...

Waungwana huwa wanasema mwana hawezi mkana mzazi maana ni laana hiyo...

Hata hivyo hapa hatujaelezwa sababu ya kutoishi na babaye mzazi ni ipi?

uhalisia usingeonyeshwa kama kusingekuwa na ugomvi.... kama alikuwa anaona umuhimu wa kumweleza baba yake ni yupi angemwelkeza kwa utaratibu mzuri... lakini tofauti zao zisipelekee kuharibu mazuri ya huyo mlezi hapana
 
Mkuu hili suala lililokukuta ni zito lakini limetokea nje ya uwezo wako.. Nadhani kama ni kweli huyo ulieambiwa ni baba yako mzazi nae ni victim tu katika sakata hili lote.. Labda unisaidie kunijibu hili.. Huyo ambae umeelezwa ndo baba yako mzazi ndo ambae anashinikiza wewe ukafanyiwe vipimo vya DNA..? Na jeee huyo baba mlezi alikuwa anajua toka zamani kama wewe sio mtoto wake..?
 
Umetumia busara sana. Kuwa baba sio sawa na kuwa sperm donor. Huyo sperm donor aendelee na maisha yake huko huko. Na usimhukumu mama kwa sababu yaliyotokea kati yao huyajui na hayakuhusu.

Focus kwenye wema wa baba yako, aliekutunza na kukulinda toka mtoto. Pole na confusion hii lakini katu usikubali kufanya dna
 
Mama kakuficha miaka yote hiyo?
Kweli dunia haiishi maovu....i woudn't forgive my mother for that..
Hata hivyo, baba mlezi ndiye baba yako..huyo mwingine ni donor tu.
 
Hakuna sababu ya kuharibu mahusiano yaliyodumu kati yake na babaye wa kufikia....

Pamoja na kufanya hivyo bado haiondoi uhalisia kuwa damu yake ni sehemu ya huyo mzee mwingine...

Waungwana huwa wanasema mwana hawezi mkana mzazi maana ni laana hiyo...

Hata hivyo hapa hatujaelezwa sababu ya kutoishi na babaye mzazi ni ipi?

sawa mkuu
 
Kula tano. Huyo jamaa wanayedai ni biological father ni "sperm donor" tu na watu kama hao wapo wengi tu duniani. Baadhi ya hospitali Ulaya wana utaratibu wa kununua "sperm" toka kwa wachangiaji mbalimbali na kuziuza kwa akina mama wenye kuhitaji watoto kwa masharti kuwa mtoaji hatakiwi kujulikana ni nani.
 
Back
Top Bottom