mkuu usijifanye kama upo smart sana,haya yamenikuta ila na wewe siku yako inakuja hasa kama una aamini ukiwa kwenye ndoa ndio utakuwa salama,nimekiri makosa yangu,lkn pia kuishi nae miaka 3 nilimaanisha kuwa nae kwenye mahusiano,sikuwa sawa kipindi naandika,nilipanga kuanza kuishi nae baada ya ndoa,naomba usinihukumu hasa kama bado upo hai,lolote nawe laweza kukutokea,tena huwenda likawa baya zaidi ya hili la kwangu,kinachonipa moyo ni kwamba wiki tatu zimepita kuna mdogo wa rafiki yangu nilimtolea damu,na nahisi hadi wakaniruhusu nitoe inamaanisha ilikuwa salama,kesho ndio siku ambayo tajua mbivu na mbichi,nahisi kwa sasa nahitaji faraja zaidi na si kejeri,hii ishu haina mwenyewe,tuombe uzima kesho nitarejesha nitakachotoka nacho maabara...all in all nimefarijika sana kwa wana JF wengi kwa kuwa watu dynamic,mnajua jambo la utani na jambo ambalo ni serious,imenipa moyo sana na narudia kushukuru kwa wote mliooonyeshwa kuguswa na tatizo langu,ki`zaidi mlionifuata PM na kunipa msaada wa mawazo na kila kitu...