Mwigulu na Mwalimu wake wa Shule ya Msingi

Chawa wa lumumbashi

JF-Expert Member
Nov 19, 2022
793
1,749
Hili la Mwigulu na Mwalimu wake wa Shule ya Msingi (RIP Maria Mkumbo) ni Darasa la kuigwa.

Nchemba.jpg

Mwigulu Nchemba akiwa na Mwalimu wake wa shule ya msingi​

Nimeshuhudia Mazishi ya Mwl Maria Mkumbo (RIP) ambaye ndiye alikuwa mwalimu wa Darasa la kwanza wa Dr Mwigulu Nchemba (WF). Haya nimeyajua ilipokuwa inasomwa historia ya Marehemu, nilishangazwa na kiwango cha utu alichofanya Dkt Mwigulu Nchemba kwa mwalimu wake huyo.

1) Alipougua kwa mara ya kwanza mwl Mkumbo na akagundulika kuwa na saratani alipokuwa anatibiwa KCMC, akiwa amekata tamaa, mwaka 2014, Mwigulu aliposikia akamtafutia Passport ya kusafiria Mwalimu na mtu wa kumsindikiza akampeleka Mwl wake India kwa check up na matitababu. Mwalimu alikaa miezi saba India kwa gharama za Mwigulu Nchemba kama vile ni mama yake Mzazi.

2) Mwaka 2015 Mwigulu Nchemba akampeleka tena Check UP India alipokaa takribani mwezi na mtu aliyemsindikiza kama vile ni mama yake mzazi.

3) Tangu augue 2014 Mwl Mkumbo kwa kuwa alikuwa anahudhuria clinic Ocean Road, Mwigulu aliamu kumhamishia nyumbani kwake mwalimu wake wa Shule ya Msingi tangu mwaka 2014 hadi sasa umauti ulipomkuta.

4) Yaani watoto wawili wa mwisho wa Mwigulu wamezaliwa wakamkuta Mwl wa Baba yao anaishi hapo wao walidhan tu ni bibi yao.

5) Kubwa zaidi alipougua sasa mwaka 2023 na kugundulika anatakiwa kuongezewa Damu Mwigulu akaenda na rafiki zake kumwongezea damu Mwalimu wake wa darasa la kwanza, Huu ni upendo ambao sijawahi kuuona.

6) Mwigulu aliwachukua na wajukuu waliokuwa wakiishi na Bibi yao ambaye ni mwalimu wake na kuamua kuwasomesha na kuishi nao.

7) Imenifanya nipeleleze zaidi maisha ya kiongozi huyu, nikagundua Amewachukua watoto yatima ambao wazazi wao walisoma shule moja na Mwigulu nakuwaambia kuwa yeye ni mzazi aliyebaki hivyo wasitoe chozi tena, akitolea mfano wa Meles Zenawi na rafiki zake waliopoteza maisha msituni.

8) Najua pia Kiongozi huyu ana mabweni ya watoto wenye uhitaji mbalimbali na yeye ndio amekuwa baba yao akiwepo mtoto aliyemchukua chini ya mti pale Ocean Road kwa tunaokumbuka, amemsomesha na sasa yuko kidato cha tano.

9) Nikajulishwa kiongozi huyu pamoja na majukumu ya nchi huenda mwenyewe mnadani kuwanunulia mahitaji watoto hawa na madukani kama mzazi anavyopaswa kufanya kwa watoto wake.

10) Kiongozi huyu anawatoto wengi amewasomesha na kuwalea achilia wa shule za msingi,sekondari na vyuo, wengine wako masters, Wengine PhD wengine kazini, wengine wabunge.

IMENIPA SURA NYINGINE YA MWIGULU NCHEMBA
 
Huyu ndiye rais ajaye wa nchi hii kupitia chama cha mapinduzi. Kule chadema yupo tundu lissu, hawa wakiingia kwenye mtanange wa kuutaka urais patakuwa patamu sana
 
Nafikiri kutangaza fadhila mtu alizowafanyia masikini hasa kwa kuwataja kwa majina sio jambo jema. Nivizuri tuchape kazi, mambo mazuri mtu anayofanya yataonekana tu.....

Unaweza kutoa laki moja kwenye milioni mia moja unazomiliki ukafikiri unatoa hela nyingi kumbe kuna wengine wanatoa Elf kumi kwenye laki moja wanayomiliki. Utoaji haupimwi kwa kiasi, bali kwa nini ulicho nacho; anayejua hiyo siri ni Mungu pekee.....
 
Naona imeanza kampeni.

Mwambieni tunachohitaji cha muhimu ni mfumo bora wa Afrya na matatibu bora yatakayopatikana hapa hapa Tanzania na sio India ili wengi ambao sio walimu wake wapate hiyo huduma.
Mwambieni tunahitaji mfumo imara wa kuhudumia watu wasiojiweza ili waweze kuishi kama wengine.
 
Mwigulu hata jimboni kwake anapendwa hatari nilishangaa sana huyo jamaa hakuna mtu wa kumung'oa hapo jimboni.
Ona hii takataka, vita ya ushoga ni ngumu sana, tuanze kupiga vita machawa na umaskini ushoga utapunguwa wenyewe.

Imagine kwa mwanasiasa basha si atakuwa anatembea na KY Jerry tu kwenye V8?
 
Pamoja na hayo hatutaki maswala ya kuchafua miamba milimani na madaraja huo wakati ukifika maana nitawashangaa sana NEMC.
 
Yaani Historia ya Marehemu Mwalimu ndiyo imeeleza misaada yote aliyofanyiwa na Mwigulu hatua kwa hatua?
 
Hili la Mwigulu na Mwalimu wake wa Shule ya Msingi (RIP Maria Mkumbo) ni Darasa la kuigwa.

View attachment 2693131
Mwigulu Nchemba akiwa na Mwalimu wake wa shule ya msingi​

Nimeshuhudia Mazishi ya Mwl Maria Mkumbo (RIP) ambaye ndiye alikuwa mwalimu wa Darasa la kwanza wa Dr Mwigulu Nchemba (WF). Haya nimeyajua ilipokuwa inasomwa historia ya Marehemu, nilishangazwa na kiwango cha utu alichofanya Dkt Mwigulu Nchemba kwa mwalimu wake huyo.

1) Alipougua kwa mara ya kwanza mwl Mkumbo na akagundulika kuwa na saratani alipokuwa anatibiwa KCMC, akiwa amekata tamaa, mwaka 2014, Mwigulu aliposikia akamtafutia Passport ya kusafiria Mwalimu na mtu wa kumsindikiza akampeleka Mwl wake India kwa check up na matitababu. Mwalimu alikaa miezi saba India kwa gharama za Mwigulu Nchemba kama vile ni mama yake Mzazi.

2) Mwaka 2015 Mwigulu Nchemba akampeleka tena Check UP India alipokaa takribani mwezi na mtu aliyemsindikiza kama vile ni mama yake mzazi.

3) Tangu augue 2014 Mwl Mkumbo kwa kuwa alikuwa anahudhuria clinic Ocean Road, Mwigulu aliamu kumhamishia nyumbani kwake mwalimu wake wa Shule ya Msingi tangu mwaka 2014 hadi sasa umauti ulipomkuta.

4) Yaani watoto wawili wa mwisho wa Mwigulu wamezaliwa wakamkuta Mwl wa Baba yao anaishi hapo wao walidhan tu ni bibi yao.

5) Kubwa zaidi alipougua sasa mwaka 2023 na kugundulika anatakiwa kuongezewa Damu Mwigulu akaenda na rafiki zake kumwongezea damu Mwalimu wake wa darasa la kwanza, Huu ni upendo ambao sijawahi kuuona.

6) Mwigulu aliwachukua na wajukuu waliokuwa wakiishi na Bibi yao ambaye ni mwalimu wake na kuamua kuwasomesha na kuishi nao.

7) Imenifanya nipeleleze zaidi maisha ya kiongozi huyu, nikagundua Amewachukua watoto yatima ambao wazazi wao walisoma shule moja na Mwigulu nakuwaambia kuwa yeye ni mzazi aliyebaki hivyo wasitoe chozi tena, akitolea mfano wa Meles Zenawi na rafiki zake waliopoteza maisha msituni.

8) Najua pia Kiongozi huyu ana mabweni ya watoto wenye uhitaji mbalimbali na yeye ndio amekuwa baba yao akiwepo mtoto aliyemchukua chini ya mti pale Ocean Road kwa tunaokumbuka, amemsomesha na sasa yuko kidato cha tano.

9) Nikajulishwa kiongozi huyu pamoja na majukumu ya nchi huenda mwenyewe mnadani kuwanunulia mahitaji watoto hawa na madukani kama mzazi anavyopaswa kufanya kwa watoto wake.

10) Kiongozi huyu anawatoto wengi amewasomesha na kuwalea achilia wa shule za msingi,sekondari na vyuo, wengine wako masters, Wengine PhD wengine kazini, wengine wabunge.

IMENIPA SURA NYINGINE YA MWIGULU NCHEMBA
Watu wanatakatisha pesa
 
Back
Top Bottom