Nimekuta mke wangu ana mimba ya mwingine

Nimekuta mke wangu ana mimba ya mwingine

Mhhh! Haupo maskani yako kwa miezi sita unarudi unamkuta mkeo ana mimba ya miezi mitatu hutii neno eti unataka kuona sinema mpaka mwisho!!! Ukistaajabu ya Mussa!!!....Mkuu isije kuwa sinema ni wewe wenzio wanakuchora tu mtaani.

siogopi kitu, nataka nione snema hadi mwisho
 
piga chini hiyo kitu tafta nyingine ugegede sahau ndoa. mkuu
 
Usijeshangaa katika hiyo ndoa mume ndio alikuwa anapangiwa muda wa kupewa na kunyimwa. SWALI LANGU KWAKO umejuaje mimba ina miezi mitatu? au mkuu umetunywesha togwa
 
Pole sana mkuu ila maamuzi ya mwisho unayo wewe
Naomba kufahamu yafuatayo
Wakati we haupo matumizi ya mke na familia kwa ujumla alkuwa unayatoa ipasavyo??
Je kwa kipindi hicho mkeo ulimuwekea mazingira gani ya kukidhi haja zake za ndoa???
Nawe ulikuwa unakidhi vipi haja zako za mwili kwa mda huo??
Kabla ya ndoa mkeo alikuwa muaminifu walau kidogo tu?

??



Ushauri wangu kwako
mchukue mkeo nenda naye hospitalini mkapime?ukishakuwa na majibu mkononi (hakikisha hayaoni majibu) usiku wakati wakulala mwambie kesho asubuhi mnaenda kuwa tembelea wazazi wake ,,,,,baada ya kufika uko kwa wazazi waambie ukweli wote then umeamua kumuacha hapo kwao mpaka ajifungue mtoto na amlee akiwa hapohapo mpaka afikishie miaka saba (7) amkabidhi mwenye mtoto ndo utakuja kumchukua apo apo kwa wazazi wake...
Baada ya hapo mkuu we ondoka wala usitake maongezi mengine ondoka speeeeeeeeeeeed sana usiangalie nyuma
 
Sikuwepo mkoani kwa miezi kadhaa, nimerudi Jana usiku nimekuta mke wangu ana mimba ya kama miezi mitatu, kumbuka sijakuwepo for more than six month.
Sitaki kumuuliza lolote kwa sasa
Yako hiyo, labda uliituma kwa whatsapp. Siku hizi kwa teknolojia kila kitu kinawezekana.
 
Pole sana. Hiyo ni ngumu kumesa. Kila la kheri.

Lakini unaposema humuulizi chochote kwasasa mimi kwakweli nimeshindwa kabisa kukuelewa. Utamuangalia kwa muda gani huku ukitarajia atasema kitu? Na je katika kipindi hicho mtakuwa mnaendelea kubadilishana vikojoleo? Kama jibu ni ndio, je mmepima VVU? Na kama mtakuwa hamgegedani utampa sababu gani za kutokupeana haki ya ndoa hasa ukizingatia kuwa ulikuwa safarini kwa muda??
 
Back
Top Bottom