Nimekula pilau kwa rafiki zangu wakristo

fimboyaukwaju

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2020
Posts
6,699
Reaction score
9,323
Ndio, nimealikwa kwa rafiki zangu wakristo, nami ni mwislamu.

Pilau nimekula, nyama za kuchoma, pilipili, kachumbari, samaki, juisi na pombe juu nimekunywa

Tunafurahi na hata uzi huu nauandika nipo hapa kwa wakristo ndugu zangu.

Siwezi kuacha, eti kwa kuwa kuna shehe karopoka eti tusile

Shubamiti. .
 
FB_IMG_1766661235837.jpg
 
Kama Muislamu basi wewe ndio Muislamu mzigo katika huu Umma.

Unaanzaje kufurahia sherehe za ibada za dini nyingine na kushiriki ?

Sherehe za kuadhimisha kuzaliwa kwa Mungu ambapo kutokana na Imani yetu ya Kiislamu Yesu sio Mungu na Mungu hana Mwana ?

Yaani unakataa kuwa Yesu sio Mungu huku unafurahia sherehe yake utakuwa sawa kweli ?
 
Hayo ya Mungu au sio Mungu hayanihusu,mradi mie wali nimekula sikwenda kwao kuabudu nimeenda kula
 
Screenshot_20250401-171833~2.jpg
 
Hayo ya Mungu au sio Mungu hayanihusu,mradi mie wali nimekula sikwenda kwao kuabudu nimeenda kula
Ingekuwa mtu amemua Mama yako mzazi na kumtukana Kisha kufanya Sherehe kwa ajili ya tukio hilo utampongeza na utapiga msosi kisa tu wewe haujashiriki mauaji ?

Kama Muislamu kweli nakusihi tubia na usishiriki tena katika ibada za dini nyingine sikuuu nzima ni ibada kushiriki katika kitendo chochote ni sawa na kushirikina katika jambo hilo na kulipa nguvu . Mimi mwanzo nilikuwa na mtizamo kama wako niliona hakuna shida yeyote maadamu siendi kanisani na siamini kuhusu Yesu kama wanavyoamini wao ila baada ya kusoma na kufikiria kwa umakini nikafahanu nilikuwa katika mtizamo wa makosa.

Sawa Leo hii usaidie bati Ujenzi wa kanisa na mbao uone sawa kisa haujajenga kanisa lote .
 
Kama Muislamu basi wewe ndio Muislamu mzigo katika huu Umma.

Unaanzaje kufurahia sherehe za ibada za dini nyingine na kushiriki ?

Sherehe za kuadhimisha kuzaliwa kwa Mungu ambapo kutokana na Imani yetu ya Kiislamu Yesu sio Mungu na Mungu hana Mwana ?

Yaani unakataa kuwa Yesu sio Mungu huku unafurahia sherehe yake utakuwa sawa kweli ?
Sehemu gani kwenye Quran inakataza waislamu kusherehekea Christmas?
 
Ingekuwa mtu amemua Mama yako mzazi na kumtukana Kisha kufanya Sherehe kwa ajili ya tukio hilo utampongeza na utapiga msosi kisa tu wewe haujashiriki mauaji ?
Familia ya Khashoggi ilifanya hivyo baada ya MBS wa Saudi Arabia kumkatakata baba yao kama nyama ya mishikaki na kumyeyusha kwenye acid huko Uturuki
 
Hayo ya Mungu au sio Mungu hayanihusu,mradi mie wali nimekula sikwenda kwao kuabudu nimeenda kula
Sheikh Marry Christmas

Ww umenda kula na Halal kabisa

Quran 5 :5
" Leo mmehalalishiwa kila vilivyo vizuri. Na chakula cha walio pewa Kitabu ni halali kwenu, na chakula chenu ni halali kwao"
 
Familia ya Khashoggi ilifanya hivyo baada ya MBS wa Saudi Arabia kumkatakata baba yao kama nyama ya mishikaki na kumyeyusha kwenye acid huko Uturuki
Scenario ya 2018
r.i.p Jamal khashog
 
Safi sana sheh
ukipata kitimoto rosti si unapiga?

Kwa dharula haina shida sheikh.

Quran 2 : 173
"Yeye amekuharimishieni mzoga tu na damu na nyama ya nguruwe na kilicho tajiwa, katika kuchinjwa kwake, jina la asiye kuwa Mwenyezi Mungu. Lakini aliye fikiwa na dharura bila ya kutamani wala kupita kiasi, yeye hana dhambi. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu."
 
Back
Top Bottom