kidunula1
JF-Expert Member
- Apr 2, 2016
- 6,299
- 6,321
Kwanza nawasalimu wajumbe humu!
Mimi bado sijaoa ila muda c mrefu nitaoa. Ingawa bado ila nimeshuhudia watu wawili ktk hatua za awali walipoenda kujitambulisha ukweni.
Mfano, rafiki yangu alitoa machozi kwa sababu ya hili jambo. Jamaa alipokwenda kujitambulisha alikutana na vitimbi balaa toka kwa mashangazi na mashemeji aisee!
Kwanza wakwe wakamuuliza sijui dini yake, kabila, wazazi wake kama wapo na km wapo wanafanya kazi gani. Balaa likaja alipoulizwa yeye anafanya kazi gani? Jamaa alipotaja kazi yake tu kumbe akawa kinyume na matarajio yao. Jamaa kazi yake si mbaya kihivyo kwa sababu ni ya kipato cha kati tu yani hizi hizi laki 5,6.
Baada ya jibu lile madada wengine wa bnt wakanynyuka na kujifanya wanaendelea na mambo mengine, mashangazi ndo kubinua na midomo kidogo. Mbaya zaidi kuna kauli aliitoa dada wa binti kwamba kama kiutani utani hivi, akasema "tulijua shem kweli shem! Shem litaingia hapa na miguu minne, Eeee flani(akitaja jina la mdogo wake) kweli safari hii umetuletea shemeji!" Alisema hivyo huku akijinyanyulisha na kujifanya kuna kitu anakiangalia angalia.
Kilichotokea pale binti akaanza dondosha chozi palepale. Wazazi walikuwa kimya kidogo. Baadae wakamwambia jamaa aende watamjulisha kinachoendelea. Jamaa akaondoka zake na watu wake akaenda kulilia kwake huku akisema "kama ndo hivyo bora flani mi niachane nae tu". Ila cha kushukuru jamaa yangu wakwe walimkubalia na ashamaliza kila kitu hadi harusi, japo ni kitu huwa anakikumbuka sana.
Nilicheka ila nilijifunza kitu kikubwa kwa sababu kwa tukio lile nilifumbuka sn macho, na kama ikija nitokea na mimi sitakuwa mgeni na hvyo vioja.
Nashauri wale wenzangu tuliokaribia kufika ukweni kwa mara ya kwanza tujiandae kisaikolojia. Na wale makaka zetu waliopita huko watufumbue macho zaidi, japo naamini si wote walopitia njiia hii ya udhalilishwaji kidogo!