Niko ukweni kwa mapumziko ya Xmas, ninachokishuhudia hakielezeki

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,894
155,913
Wasalaam waungwana. Amani ipitayo akili na fahamu za binadamu iwe pamoja nami.

Tangu nioe nina mwaka wa kumi sasa ndoani. Wakwe zangu ni wakarimu sana na wacheshi mno. Ni marafiki na washauri wazuri sana kiasi kwamba unaweza kutamani kuwasimulia jinsi mchepuko wako ulivyo pasta kichwa.

Kwa kipindi chote cha ndoa yangu nilikuwa sijawahi kuujua upande wa pili a.k.a kisogo cha wakwe zangu. Nilikuwa nawajua sura tu... yaani upande wao wa mazuri tu.

Mwezi wa kumi na moja ndipo nilikuwa natimiza miaka kumi ya ndoa, anniversary ya kibabe sana nikafanya. Wake ndani ya nyumba.

Basi katika sherehe nikawa na mengi sana ya kuongea na wake zangu. Wakaninisistiza sana hii December nisikose.

Basi tarehe nane nikaliamsha dude kuelekea ukweni. Sina paparazzi wala haraka barabarani, mdogomdogo hadi nikafika upcountry ukweni.

Wakwe wakanipokea vizuri sana. Nikawa na mazungumzo na Baba mkwe wangu.

Tuliongea mengi lakini kila mara alikuwa ananisisitiza ni lazima niingie kwenye ukoo wao.

Kichwani nilikuwa nawaza sana naingiaje kwenye ukoo mara ya pili? Maana kama watoto nimeshazaa na binti yao, kitu ambacho ni kiunganishi haswa cha koo mbili.

Basi usiku ukaingia, akanifuata chumbani kisha akaniita nitoke nje. Nilipotoka akaniambia kibabe huku akipigapiga kifua changu kwa ngumi zisizoumiza "Kesho tunaenda kutafuta malighafi jiandae kiume".

Saa kumi na nusu alfajiri akaniamsha kwamba tuanze safari. Hiyo haina kuoga wala kupiga mswaki. Tukaingia kwenye Toyota Hilux 12R na safari ikaanza.
1639981486804.png


Basi tuliingia majoring kwa saa moja na nusu nzima tukipita kwenye misitu na mapori. Hatimaye tukatokea kwenye kijiji chenye nyumba chache sana.

1639981447188.png


Akaegesha gari kwenye moja ya nyumba ya nyasi kisha akaniashiria nimfuate.

Nikamfuata na tukaufikia mlango. Kabla hata hajaugusa nilistaajabu kuona mlango ukijifungua wenyewe bila ya kuguswa na mtu. Na hata tulipokwisha India ndani, mlango ukajifunga wenyewe.

Hapa kwenye kijisebule palikuwa na vigoda vinne na kiti cha mpando kimoja.
Tulikaa kimya na hamna aliyemuongelesha mwenzake.

Baada ya dakika kama tatu hivi chungu kidogo kama vile wanavyotumia wanawake kujifukiza kikaanguka na kuvunjika. Nikabaki najiuliza chungu hiki kimetokea wapi? Maana hamna sehemu ambayo kingeweza kujishikia au kuwekwa.

Mara akatokea babu kizee aliyekuwa kajitanda shuka huku kifuani kaning'iniza ngozi ya chatu.

Hakusalimia akaanza kuongea peke yake kwa kilugha. Aliongea kwa dakikanne mfululizo kisha akasema nendeni.

Nje tukakuta dume la ng'ombe kubwa lakini fupi kimo kama cha mbuzi.
download.jpeg

Tukampakia kwenye gari. Baba mkwe akaniambia niingie ndani kuna furushi kubwa natakiwa kulibeba pia.

Nikaliingiza ndani ya gari. Baba mkwe alileta mikuki ya aina na saizi mbalimbali kama nane na upinde na mishale yake. Akaweka kwenye gari. Akasema kuna kitu kimoja kmuhimu sana tumekisahau. India ndani kalete ngao.

Basi nikaingia ndani nikakuta ngao ndogo sana kama saizi ya kiganja cha mkono. Nikaichukua na kuingiza garini.

Baada ya hapo tukaanza upya safari yetu kimyakimya. Tukaenda kwa kama dakika 45 tukakutanana Uwanda mpana sana wa majani mafupi na mazuri sana yaani eneo hilo lipo kama uwanja wa golf ila mkubwa sana.

Baba mkwe akasimamisha gari kisha akasema tushuke. Nikashuka , nikamwacha yeye garini nashangaa mwenzangu kaanza kuvua nguo.

Akavua zote akasema na mimi nivue kwani huko hatutakiwi kuwa na mavazi.

Nikaanza kuvua, mara nikaona wanakuja jamaa wanne warefu sana nao wako uchi wa mnyama.

Kadiri muda unavyoenda ndivyo watu walio uchi waavyozidi kuongezeka.

Nilichokigundua ni kwamba hawa watu walikuwa wanatuweka mtu kati. Yaani wanatuzingira huku wakicheza aina fulani ya ngoma ambayo ala zake walizitengeneza kwa kupigapiga mapaja yao makofi na kwa mdomo.

Baba mkwe akaniambia usiogope. Nimekuleta kwenye nchi ya wafu. Hawa wote walikufa siku nyingi.

Basi wale wafu wakaendelea kutuzingira huku wakiongezeka.

Baba mkwe akaniambia kuwa kwao kila mwezi wa kumi na mbili lazima wafanye kafara la kulisha wafu wao damu

Hivyo kuanzia wakati huo mimi nimeshaingizwa rasmi kwenye ukoo wao na ndiye nitakuwa mlishaji wa damu kwa wafu hao.

Akaletwa yule ng'ombe mfupi, ndani ya muda mfupi akawa amevamiwa na wale wafu.

Walimla hawakubakiza hata mifupa. Na ghafla wafu wale wakaanza kuyetuka kisha wakapotea kabisa.

Tukabaki wawili tu mimi na Baba mkwe tukiwa uchi wa mnyama.

Tukavaa nguo zetu na kuanza safari ya kurudi.

Mzee kaniambia baada ya hapo nitaona mabadiliko yangu makubwa sana kwenye uchumi, umiliki na utawala.

Baba mkwe kasema hilo lilikuwa ni tambiko dogo tu la kuni introduce kwa wafu wao na wamenipenda sana.

Kasema mwisho wa mwaka mpya tutafanya tambiko lingine kubwa sana.
Stay tuned
 
Wasalaam waungwana. Amani ipitayo akili na fahamu za binadamu iwe pamoja nami.

Tangu nioe nina mwaka wa kumi sasa ndoani. Wake zangu ni wakarimu sana na wacheshi mno. Ni marafiki na washauri wazuri sana kiasi kwamba unaweza kutamani kuwasimulia jinsi mchepuko wako ulivyo pasta kichwa.

Kwa kipindi chote cha ndoa yangu nilikuwa sijawahi kuujua upande wa pili a.k.a kisogo cha wakwe zangu. Nilikuwa nawajua sura tu... yaani upande wao wa mazuri tu.
Bila shaka ni mapori ya umalila
 
Back
Top Bottom