Almanusura brother kunyimwa mke ukweni

Rabonn

JF-Expert Member
Nov 7, 2018
5,733
10,928
Habari zenu wadau, mambo vipi?
Moja kwa moja kwenye mada.

Juzi kati nikiwa katika harakati zangu za kuzunguka sana mikoani kuuza maneno (marketing) kulingana na nature ya kazi nayofanya ili mradi tu nipate wateja (sales) wa kunipatia mkate wa kila siku nikajikuta niko Iringa mjini.

Hapa mimi ni nyumbani japo kiasili kwetu ni Mbeya Rungwe lakini wazee walijikuta iringa miaka mingi sana hivyo nimezaliwa hapa na elimu yangu yoote nimeipata hapa mpaka kuhitim kidato cha 6.

Kwahiyo kwakifupi nikawa nimerudi Iringa lakini kikazi zaidi na nilikua na plan ya kuwpo kwa siku 6 then ya 7 nigeukie upande mwingine.

Sasa basi, hapa home (nilifikia kwa wazee) nikakuta kuna ratiba ya kwenda maeneo fulani panaitwa KIWELE ambako huko brother alikua amechumbia na anataka kuoa huko.Hii kiwele ni Njia ya kwenda PAWAGA (haya ni maeneo ndani ya Wilaya ya Iringa vijijini chini uwakilishi wa Mh.LUKUVI 😂😂 watu wanaogopa hata kum challenge aondoke).

Basi nikaulizwa kama nitakua na nafasi (ilikua ni siku kama ya 3 mbele toka nifike) ili nijumuike kwenye msafara.
Nikawaambie haina shida , by the way huyu ni brother kukataa kumpa company ni utovu wa nidham wa nje nje.Nikaweka ratiba sawa za nisikosekane.

Siku ya siku ikafika tukaelekea ukweni.Mimi, brother, madogo kadhaa, ma sister, ma aunt na baba na mama.

Baada ya kufika taratibu zote zikaendelea palee ikiwemo suala la kutoa na kupokea mahali (taratib ni ndefu ila kwa kifupi zilifuatwa na kama mjuavyo ni baadhi tu ya watu hujumuika kwenye ile session na sio wote kwa pande zote).

Kama mnavyojua sie wengine tusio na mambo mengine (YASIO NA MSINGI) kama ambavyo imezoeleka siku hizi, tuli plan siku hiyo ya kutoa mahali ndio pia Shemeji atavikwa PETE tufanye mambo simple tu isiwe sherehe separate kama wengi wafanyavyo.

Basi baada ya mahali NDIO KIMBEMBE KILIPOTAKA KUJITOKEZA.

Brother akatakiwa kwenda kuwasalimia mashangazi wa mkewe ambao wao walikua wamekaa location separate kabisa pale nyumbani (ilikua ni shughuli iliyohudhuriwa na ndugu wengi kidogo) na umbali walipokua wamekaa hawa watu ni kama mita 15 toka sitting room ambako mahali ilikua inakabidhiwa na distance hiyo ni mchanga tuuu na vumbi hadi kuwafikia mashangaji waliokua wame relax kwenye viti chini ya ka TENT flani hiv.

Sasa brother akaanza kupiga hatua kuelekea huko akiongozana na wazee na mshenga ndipo na huko ndiko shemeji alikokua na zoez zima la ENGAGENENT (kumvisha pete shemeji) lilitakiwa kufanyika.

akaambiwa sasa bwana huku unakokwenda UNAPASWA KUTEMBEA KWA MAGOTI MPAKA KUWAFIKIA MASHANGAZI NA KUPITA UWASABAHI UKIWA UMEPIGA MAGOTI...

Aaahhhh hapo sijui ilikuaje ila braza akagoma katakataaaaa..Yan ile strongly amamwambia mshenga wake (huku wazee baba na mama) wakisikia bayana kwamba "MIMI SIWEZI TEMBEA KWA MAGOTI KUMFUATA MKE WANGU NA NDUGU ZAKE ILI KUMVISHA PETE "

Akakataa katakata.Mshenga akamsisitiza sana ile kichini chini kwamba tutaaibika maana hiz ndio mila zao hawa na si unaona wanatungoja sisi kule tufike(maana sisi kiumeni tulikua huku na wao kikeni pamoja na wazaz wao walikua kule af hapa kat hizo mita 15 zimetu set apart ambapo braza anatakiwa kutangulia akitembea kwa miguu sis tukimfuata nyuma).

Braza akagomaa katakataaaa.."SIWEZIIIIII.KWANI MIMI NDIO NAMUOA YEYE AU YEYE NDIO ANANIOA MIMI?".

Baada ya zoez kuonekana gumu na hakuna dalili za braza kukubali ikabidi mzee/ baba yaan aingilie kati maana hata yeye hicho kitu kwa mbali niliona kama hajakielewa hiv ila akawa katulia tuuu shughul ana deal nayo mshenga.

Na ikumbukwe hapo wakwe zetu wakawa kama wameduwaa giv wanajiuliza nini kinaendelea kule mbona kama wana jadiliana badala ya kuja tumalize kazi? Ilichukua kama dakika 7 hiv katika hii sintofahamu.

Ikabidi mzee asogee mbele kidogo kuwaelekea wakwe zetu kwa unyenyekevu akasema Jaman kama mnavyojua VIJANA WA SIKU HIZI WAJUAJI hawapendi kufuata mila zetu.Sasa basi naomba kwakwel mumruhusu aje akiwa anatembea kawaida tu kama itawezekana..Basi upande wa pili nao wakajadili kama dakika 3 hiv kisha wakasema SAWA ..

Hapo sasa ndio tukabjongea kuelekea kunako mahala wakwe walipo ili kumaliza zoezi la Kutoa salamu na kumvisha pete mke wetu ila kwakua shemeji ALIJIPANGA KUPIGIWA GOTI KUVIKWA PETE akajikuta ameshindwa kuiga GOTI yeye pia hivyo wakavishana pete wima wima.

Ma aunt wakagewa Hi ki sela huku wamenunaaa 😂😂

Dah nikastaajab sana haya mambo ya mila yalivyo magumu.
Tukamaliza tukala tukanywa tukaondoka kurud iringa mjini.

Nikiwa njiana nikamuuliza brother kama angekaza mpaka mwisho hata kama ingem gharim kukosa mke ??mana alivunja taratibu za watu!!! AKASEMA KATU ASINGEWEZA KUMPIGIA MAGOTI MKEWE MBELE ZA WATU WALA HAWEZ PIGIA GOTI NDUGU YEYOTE WA MKE WAKAT YEYE NDIO ANAKABIDHIWA MTOTO WAO AKAMTUNZE.
"CHUMBANI PEKE YETU NAWEZA PIGIA MKE WANGU GOTI KAMA NIMEMKOSEA KOSA KUBWA SANA LA KUHATARISHA NDOA YETU ILA SIO HAYA MAMBO YA KIPUUZI YA KUCHORESHANA NISIJE NIKAJIKUTA NIMEKABIDHI NAFASI YANGU KAMA KICHWA KWA MKE WANGU KISHA AANZE KUNISUMBUA KUMBE YOTE NIMESABABISHA MWENYEWE.

Nikamkubali sana brother.

Uzi tayari
 
Leo kuna clip inatembea mitandaoni inamuonyesha mama mtu mzima akiwakanya vijana wa kiume wanaotarajiwa kuoa kamwe wasikubali kumpigia goti mwanamke wakati wa kumvisha Pete kwani itapelekea yule mwanamke ajione yeye ni ndie mwenye mamlaka kwako. Amesema kisaikolojia athari zake ni mbaya sana.
 
Hiyo cha mtoto,juzi kati mdogo wangu wa kike,mchumba wake alikuwa anajitambulisha nyumbani kwetu,huyo shemeji yangu ni masai,chakula kilipikwa mapema sana toka saa 7 mchana tayari,kimbembe kilikuja pale tunawasubiri upande wa kiume waje kujitambulisha,tulisubiri wapi hawaji wala nini,nikimuuliza mdogo wangu mbona hao watu hawaji anasema wanakuja subirini,wajomba waliokuwa wametoka moshi wakaona bora waandoke,mama akawaita ndani wajomba wakapewa chakula ndio wakaondoka wakiwa wamechukia sana.

Tuliwasubiri wakaja mda wa saa 10 jioni,na Kigari Chao cha ist,wakiwa wamebeba ndizi mikungu 3,viazi gunia?mafuta dumu kubwa,sukari mfuko mmoja,mchele kilo 50,unga wa ngano kilo 25,kwenye hilo gari kulikuwa hakuna hata mwanaume mmoja,wote walikuwa wanawake.

Kumbembe kilikuja pale waliponiita,nikabebe ile mizigo,niligoma katu katu,yani mimi nikabebe mizigo iliyoletwa na wanawake,tena wamechelewa ,chakula kipo tu kinawasubiri mda wote hakuna aliyekula wanawasubiri mda wote,niliyona yale ni madharau niligoma katu katu mpaka wakatafuta watu wakusomba ile mizigo..
 
Safi sana its very wrong. Mwanaume abaki mwanaume na mwanamke abaki mwanamke. Huyo mwanaume ana msimamo mzuri na hakuna alichokosea. Kwanza mashangaz wengne nuksi tu hawana jipya..wakwende uko.
 
Hiyo cha mtoto,juzi kati mdogo wangu wa kike,mchumba wake alikuwa anajitambulisha nyumbani kwetu,huyo shemeji yangu ni masai,chakula kilipikwa mapema sana toka saa 7 mchana tayari,kimbembe kilikuja pale tunawasubiri upande wa kiume
Hicho kigari ki IST chao kina nguvu sana kinabeba mizigo mingi hivyo plus watu. Kuna watu watasema umewapa chai.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom