Nimejiandaa kisaikolojia nitakapokwenda kujitambulisha ukweni

kidunula1

JF-Expert Member
Apr 2, 2016
6,299
6,321
Kwanza nawasalimu wajumbe humu!

Mimi bado sijaoa ila muda c mrefu nitaoa. Ingawa bado ila nimeshuhudia watu wawili ktk hatua za awali walipoenda kujitambulisha ukweni.

Mfano, rafiki yangu alitoa machozi kwa sababu ya hili jambo. Jamaa alipokwenda kujitambulisha alikutana na vitimbi balaa toka kwa mashangazi na mashemeji aisee!

Kwanza wakwe wakamuuliza sijui dini yake, kabila, wazazi wake kama wapo na km wapo wanafanya kazi gani. Balaa likaja alipoulizwa yeye anafanya kazi gani? Jamaa alipotaja kazi yake tu kumbe akawa kinyume na matarajio yao. Jamaa kazi yake si mbaya kihivyo kwa sababu ni ya kipato cha kati tu yani hizi hizi laki 5,6.

Baada ya jibu lile madada wengine wa bnt wakanynyuka na kujifanya wanaendelea na mambo mengine, mashangazi ndo kubinua na midomo kidogo. Mbaya zaidi kuna kauli aliitoa dada wa binti kwamba kama kiutani utani hivi, akasema "tulijua shem kweli shem! Shem litaingia hapa na miguu minne, Eeee flani(akitaja jina la mdogo wake) kweli safari hii umetuletea shemeji!" Alisema hivyo huku akijinyanyulisha na kujifanya kuna kitu anakiangalia angalia.

Kilichotokea pale binti akaanza dondosha chozi palepale. Wazazi walikuwa kimya kidogo. Baadae wakamwambia jamaa aende watamjulisha kinachoendelea. Jamaa akaondoka zake na watu wake akaenda kulilia kwake huku akisema "kama ndo hivyo bora flani mi niachane nae tu". Ila cha kushukuru jamaa yangu wakwe walimkubalia na ashamaliza kila kitu hadi harusi, japo ni kitu huwa anakikumbuka sana.

Nilicheka ila nilijifunza kitu kikubwa kwa sababu kwa tukio lile nilifumbuka sn macho, na kama ikija nitokea na mimi sitakuwa mgeni na hvyo vioja.

Nashauri wale wenzangu tuliokaribia kufika ukweni kwa mara ya kwanza tujiandae kisaikolojia. Na wale makaka zetu waliopita huko watufumbue macho zaidi, japo naamini si wote walopitia njiia hii ya udhalilishwaji kidogo!
 
Ndio shida ya uchumba wa mijini huu, hii habari yako ina mushkeli mkubwa kwakuwa kwa sehemu kubwa mshenga ndio humaliza kila kitu
Na hata kama ni kujitambulisha binafsi unatakiwa uwe umeshafanya ushushushu wa familia husika na jinsi ya kudeal nayo
 
Nakubaliana Nawe
Pia Watu Wote Hatuwezi Kulingana Uwezo Na Ushushu Hukufanya Kujua Ikiwa Family Ile Mnaendana
Kuna Jamaa Alinunua Gari Japan Kwa Mkopo Kisa
Mkewe Kwao Wanauwezo Mkubwa.
 
Nakubaliana Nawe
Pia Watu Wote Hatuwezi Kulingana Uwezo Na Ushushu Hukufanya Kujua Ikiwa Family Ile Mnaendana
Kuna Jamaa Alinunua Gari Japan Kwa Mkopo Kisa
Mkewe Kwao Wanauwezo Mkubwa.
Hii ni mbaya sana ni lazima uwe halisi tangu mwanzo ili wachague kusuka au kunyoa
 
Mmh kuna familia unaweza jikuta tu umeghairi kuoa/kuolewa huko. Ndo maana tunasemaga chunguza na familia/ukoo wa mwenzi wako kabla hamjaamua kuoana.
Hivi tuseme hawakumuuliza binti chochote kabisa kuhusu mtarajiwa wake hadi mtu afike kujitambulisha ndo muanze kujidhalilisha "eti nilijua shem, shem kweli" mweee. Disgusting! !!

Of course maswali mtamuuliza but inakuwa tu kama kupiga story ili mfahamiane zaidi coz details zake za muhimu lazima binti awe ashawapa mapema ndo mfikie kusema "mlete au usimlete". Me rafiki angu tu akiniambia ana new baby lazima atanipa A, B, C zake. Hivi mtu atasema tu nimepata mchumba afu msiulize chochote mmwambie tu "mlete" mmh?

Fine, mchumba hajameet expectations zao, wameshindwa kujikaza hadi mtu aondoke ndo walete mashauzi yao? They didn't have to stoop so low. Sipati picha binti ndo akipelekwa kwenye hiyo familia, atakavyochambuliwa
 
Hii ni mbaya sana ni lazima uwe halisi tangu mwanzo ili wachague kusuka au kunyoa
Unakumbuka kisa wimbo wa pendo?
Pendo mimi mumeo kazi yangu ni kibarua
Cha kuponda kokoto hapa mjini pend eee
Ulipokuja kwetu kunioa ukisema we we ni muhasibu na una magari mifugo na mashamba vp leo uniambie wewe ni mponda kokoto?
Ila bint alimwambia jamaa asinge mdanganya na ajibidiishe Penye elimu kwani haina mwisho.
So haya mambo yanatokea sana ila ukweli utakuweka huru sio ujitutumue nawe kudanganya.
 
Unakumbuka kisa wimbo wa pendo?
Pendo mimi mume kazi yangu ni kibaaya
Cha kuponda kokoto hapa mjini pend eee
Ulipokuja kwetu kunioa ukisema we we ni muhasibu na una magari mifugo na mashambq vp leo uniambie wewe ni mponda kokoto?
Ila bint alimwambia jamaa asinge mdanganya na ajibidiishe Penywaun elimu kwani haina mwisho.
So haya mambo yanatokea sana ila ukweli utakuweka huru sio ujitutumue nawe kudanganya.
Duu siku hizi huwezi kuzipata tungo kama hizi
 
Mmh kuna familia unaweza jikuta tu umeghairi kuoa/kuolewa huko. Ndo maana tunasemaga chunguza na familia/ukoo wa mwenzi wako kabla hamjaamua kuoana.
Hivi tuseme hawakumuuliza binti chochote kabisa kuhusu mtarajiwa wake hadi mtu afike kujitambulisha ndo muanze kujidhalilisha "eti nilijua shem, shem kweli" mweee. Disgusting! !!

Of course maswali mtamuuliza but inakuwa tu kama kupiga story ili mfahamiane zaidi coz details zake za muhimu lazima binti awe ashawapa mapema ndo mfikie kusema "mlete au usimlete". Me rafiki angu tu akiniambia ana new baby lazima atanipa A, B, C zake. Hivi mtu atasema tu nimepata mchumba afu msiulize chochote mmwambie tu "mlete" mmh?

Fine, mchumba hajameet expectations zao, wameshindwa kujikaza hadi mtu aondoke ndo walete mashauzi yao? They didn't have to stoop so low. Sipati picha binti ndo akipelekwa kwenye hiyo familia, atakavyochambuliwa

Yeahh yaan kwenda ukweni kichwa kichwa ni upuuzi kwa nini mtu asifanye ujanja uwajue vizuri wengi wao hata kama sio wote kabla ya kwenda..

Mbona simple sana kama una mpango naye zile out out haina shida leo kaja na mdogo wake kesho na binamu zake unawapigisha misosi kama wanalewa poa na transport uhakika mpaka kwao kaka zake kama sio wakuda sana unawalinda linda kihivyo

Siku official ukienda kwao mbona wanatamani umchukue siku hiyo hiyo kila mmoja anajidai anakujua wanaleta story nyingi wewe unacheki mission na vission yako hapo hahah
 
aisee niwe mkwel ingekua imetokea kwanguserius after ndoa wale waliosema tulijua shem kumbe shemejiii ningeanza na kwa maana shida hazina odi wala adabu....
 
Mmh kuna familia unaweza jikuta tu umeghairi kuoa/kuolewa huko. Ndo maana tunasemaga chunguza na familia/ukoo wa mwenzi wako kabla hamjaamua kuoana.
Hivi tuseme hawakumuuliza binti chochote kabisa kuhusu mtarajiwa wake hadi mtu afike kujitambulisha ndo muanze kujidhalilisha "eti nilijua shem, shem kweli" mweee. Disgusting! !!

Of course maswali mtamuuliza but inakuwa tu kama kupiga story ili mfahamiane zaidi coz details zake za muhimu lazima binti awe ashawapa mapema ndo mfikie kusema "mlete au usimlete". Me rafiki angu tu akiniambia ana new baby lazima atanipa A, B, C zake. Hivi mtu atasema tu nimepata mchumba afu msiulize chochote mmwambie tu "mlete" mmh?

Fine, mchumba hajameet expectations zao, wameshindwa kujikaza hadi mtu aondoke ndo walete mashauzi yao? They didn't have to stoop so low. Sipati picha binti ndo akipelekwa kwenye hiyo familia, atakavyochambuliwa
kuna familia zina mambo ya ajabu sanaaaa af wanawake ndo huwa tuna matatizo wanaume hawana shida eti, ndo mana tunaambiwa tuchunguze na familia za wenza wetu ili kuepuka udhalilishaji kama huo. Sipati picha naenda ukweni navoanza kunyambuliwa sasa weeeee
 
Aisee! mkuu ushaanza kunitisha,hivi karibuni nategemea kupeleka posa. Na kwa details nilizopata ni kwamba baba mkwe ni mkorofi balaa...na huwa hana soni kwa mtu yeyote hata kama ndo anakuona kwa mara ya kwanza.
Sasa nikiunganisha dots hapo juu ndo tumbo linazidi kuniuma yani. Sijui nitatoka salama siku hiyo!? nawaza tu mwenyewe.
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom