Nimejenga ujenzi rahisi kwa Milioni 7 tu

Nimejenga ujenzi rahisi kwa Milioni 7 tu

Hii hapa ina
1.master bedroom
2.jiko
3.sitting room
4.mfumo kamili wa maji
5.mfumo wa umeme
6.plaster nje na ndani
7.gypsum
8.rough floor ya zege

ImeCost 7.5M

NB:.tiles na rangi vyote vimenunuliwa na fedha hyohyo, najikongoja nimlipe fundi afanye finishing. View attachment 1427385View attachment 1427386View attachment 1427387View attachment 1427388

Supu ya mawe
Dah hii ni 100 times better kuliko kumpelekea mtu 150,000 kila mwezi. Tokea hapo unaweza jenge nyumba ya ndoto zako taratibu.

Nafikiria pia kufanya kitu cha namna hii nikiwa nashughulikia swala la kujenga fully fledged house kwa ajili ya watoto wangu. Mbeleni huko First borne wangu atavimba humu wakati akijipanga kujenga ya kwake.
 
Hongera kijana umetoa somo.
Ila kwa bati gge 32 wamekuliza maana gge 30 ni 18,500/= Ars.
Kitu cha muhimu ni kusimamia, omba likizo simamia mwenyewe usilizwe kwenye vifaa na cementi.
Mafundi wengi sio waaminifu, usiposimamia utajengewa chini ya kiwango.
 
Wakuu, poleni na janga hili la corona. I hope mnachukua tahadhari zote ili kubaki salama. Basi leo nimeona vema nishee namna nilovokamilisha ujenzi wa kijibanda changu. Najua kuna mtu ntakua nmemsaidia na kumtia moyo kwamba kwa kidogo alichonacho, inawezekana kuepukana na adha za ma faza house.

Nyumba nimejenga ni ndogo ila inanitosha. Ni vyumba viwili vya kulala, sebule, choo na korido fulani ambapo ndo kuna jiko kupikia. Kiwanja nilinunua 25 kwa 25 nilinunua mwaka juzi 2018 kwa sh milion4.5 locationi ni madale mwisho. So nkaona kujenga nyumba kubwa itanichukua muda mrefu kulinganisha na kipato changu, so nkajenga nyumba hii ndogo pemben kabisa ya uwanza, na kuacha nafasi kubwa kwa ajili ya ujenzi wa nyumba kubwa hapo baadae. Nyumba hii imeanza kuchimbwa msingi tar 22 feb 2020 na baada ya siku 29 me nkahamia.

Baada ya kuezeka milangoni na madirisha nmewekaMa drill. Na nyavu za kukinga mbu. Bado cjaweka plasta. Na chini ni rough floor. Sijaweka ceiling board , namaanisha dari. Hii nmeweka chooni tuu. Milango ya mbao ni miwili wa chooni na wa sebuleni. Umeme pia bado ila nmeshalipia nawasubiri jamaa wakuje kuwasha.

So nyumba hii cjacomplicate saana. Nmejenga simple tuu. Maana kuna bandiko niliona humu jf jamaa alisema ujenzi ni ww na maamuzi yako unatakaje. Unaweza jenga kwa m10 ramani ile ile ambayo mwingne kajenga kwa m20.

Gharama za ujenzi.
Vifaa vya ujenzi vyote vilinunuliwa siku moja. Tar 22 feb 2020. Lengo la kununua kwa siku moja ni kupunguza gharama za usafiri kununua kimoja kimoja. Nilinunua na nikaweka hapa kwa jirani yangu.

Vifaa vyote vilinunuliwa maduka ya madale mwisho. Actually kabla sijanunua nilienda maduka ya town tegeta kule, nkaulizia bei baada ya kupiga tathmin nkagundua cjakwepa kitu. Nei ni zile zile tuu. So nkaona bora ninunue madale ntasave kidogo kweenye usafiri. So gharama ni kama ifuatavyo.

Bati geji 32 @ 18,500 = 740,000
Cement 37 @13,500 = 499,500
Mbao papi 18 @ 10,000 = 180,000
Mbao kenchi 40 @ 5,800 = 232,000
Mbao zege 15 @ 7,500= 112,500
Misumari nchi 4 kg 10 @ 3,000 = 30,000
Misumari bati kg 9 @ 6,000 = 54,000
Misumari nchi 3 kg 2 @ 3,000 = 6,000
Koa 2 @ 3,500= 7,000
Nondo 10 @ 18,000 = 180,000
Sink la choo 1 @ 18,000
Bomba 2 nchi 4 @ 13,000 = 26,000
Bomba nusu nchi 1.5 @ 7,500 = 3,500
Pitrap 1 @ 2,500
Elbow 2 @ 3,500 = 7,000
Usafiri 40,000
Kuchimba shimo la choo 230,000
Mchanga tipa 4 @55,000 = 220,000
Kokoto tipa 1 @ 150,000
Tofali 1650 @ 1025 = 1,691,250
Grill madirisha 4 @ 150,000= 600,000
Grill mlango 1 @ 200,000
Grill dirisha choo 1 @ 30,000
Mlango wa sebule 150,000
Nyavu za mbu na zile zingne nilisahau kurekodi. Lets say 100,000

Fundi 1,300,000 ( alifanya kila kitu)
Saidia fundi 29 days @10,000 = 290,000
Chakula mchana 29 days @ 3,000= 87,000
Jumla niliyopata kwa gharama zote hizo juu ni
7,200,000


Sent using Jamii Forums mobile app
nice
 
Back
Top Bottom