Nimejenga ujenzi rahisi kwa Milioni 7 tu

Nimejenga ujenzi rahisi kwa Milioni 7 tu

Anza na ramani ya msingi (floor plan). Kama unamudu chora mwenyewe. Hii namaanisha unataka vyumba vingapi, ukubwa gani, milango, madirisha nk. Usihangaike sana na muundo wa paa. Fundi bora akiona jengo ataamua iweje.

Ukipata ugumu wa kuchora washirikishe mafundi ujenzi wa kawaida (anaweza kukuchorea bure au akakutoza gharama kidogo).

Hii ina maana utaweka mahitaji yako vema kwa kufahamu eneo linalohitajika. Mfano: chumba chako cha kulala, urefu wa kitanda sm. 190(180 godoro ongeza 30 za miguu). Fikiria kabati la nguo, meza ndogo, labda na kiti nk. Hapa utaepuka kujenga eneo lisilohitajika.

Nakuhimiza usiogope.

Ushauri: Ni bora kujenga nyumba ndogo ukaikamilisha (ukaifikisha kiwango cha kuitumia) kuliko hekalu ambalo usishangae unaishia lenta au kuezeka lkn milango na madirisha ukayaona yako mbinguni.

Sent using Jamii Forums mobile app
Asante sana mzee nimekuelewa vizuri sana. Nafanyia kazi
 
hongera huo ndio uanaume, picha tafadhali!!!!. Nimepata kawivu ka maendeleo...nilikuwa na pesa kama hiyo ila imepukutika kwa kujihudumia nilipokuwa naumwa.....nimeudhika sana, kuanza moja kuitafuta tena ni neema za kiMungu sasa!. Hongera sana kwa mara nyingine
Maisha yana changamoto sana,
 
Hongera sana. Mtu kama huna nyumba nyingine unahamia hivyo hivyo. Na ujenzi wa ukiwa ndani ni kwenda na malengo tu.
Muhindi na mm nataka nikujengee nyumba kalii ya vioo ufukweni mwa bahari,
 
Back
Top Bottom