Nimeibiwa ATRIUMS hotel Sinza.

Hii si ile pembeni ya kona baa...haiuzi bia wala kilevi cha aina yoyote...inapokea wateja wa haraka na wa pole pole
 
Mkuu unawakilisha kundi kubwa sana la watanzania. You just jump to conclusions without any critical analysis whatsoever.Tubadilike ndugu yangu.

Tubadilike kuacha uongo kwanza. Hii nyuzi inaonesha ni uongo.
 
Nilikuwa Dar Es Salaam kwa muda wa week moja, nilikaa Atriums Hotel na nikaibiwa night ya nne, niliibiwa chumbani usiku wa saa 3 wakati nikiwa restaurant nakula hapo hapo hotelini... Niliibiwa digital camera 2, na simu aina ya HTC, na pesa taslim usd 2300.., mbaya zaidi mmiliki wa hotel anaitwa Erik Shingongo alifika hapo hotelin baada ya kupigiwa sim na meneja wake ndugu Sunday nilieripoti wizi huo muda huo huo. Shigongo aliniambia kuwa anawajua wezi nimpe muda wa saa 3 atarudisha vitu vyangu, baada ya masaa 3 kupita alikuja tena akiwa na maaskari 3 toka kituo cha polis kijitonyama na wakanitaka kutoa maelezo., na wakati huo, ikiwa saa 7 usiku shigongo aliniambia kuwa tayari kesha washika wezi wanne ambao ni wafanyakazi wa hotelini hapo HIVYO nitulie nitapata mali zangu.Nimesubiri bila mafanikio, nikapewa maelekezo ya kumwona RCO wa osterbay, kamanda Wambura ambae alitoa maagizo ya kuwepo mkutano kati yangu na shigongo na meneja wake bwana sunday, mkutano ufanyike ofisin kwa rco ili tuweze kukubaliana namna ya kurudisha vitu nilivyoibiwa. Shigongo hakutokea, meneja wake alifika na akiwa amepewa na maagizo na Shigongo kuwa msimamo wa hotel ni kutolipa au kutoa fidia ya aina yeyote, kuwa wao kama hotel wanaona ilikuwa ni kosa langu kwenda hotelin ATRIUMS. na pia alisema hakuna wa kumfanya lolote Tanzania hii hata nikiripoti kwa RPC, RCO akaridhia na akaniambia hana la kufanya na sheria haimpi nafasi ya kumbana shigongo.
hiyo ndo ilikuwa final na kesi ikafungwa, Tanzania ya watanzania raia hana haki, hadi polis wanaubariki wizi na kuutetea, pale ATRIUMS ni kichaka cha kufuga wezi, mwizi namba moja akiwa Erik Shigongo. namba 2 meneja wake na namba 3 team yake ya wafanyakazi, Kuweni makini msiumie kama mimi.

Chacha Mwita nina wasiwasi na wewe yawezekana ulikuwa na kitu kutoka hapo Corner Bar ukakiacha ndani ya room ukaenda kununua chakula,ulipo rudi ukakuta umeibiwa ndo maana Shigongo anajibu hivyo baada ya kukuambia namjua mwizi.Wewe ukabali matoke na siri unaijua wewe.Vumilia kama MALIMA.....teteteteteteh.Ukuwa na AK-47?au sime?Pote pole sana Mura
 
Erick Shigongo nae ni mwizi tu, kumbuka maisha yake ya KIgali alitoroka Jela!
 
Nilikuwa Dar Es Salaam kwa muda wa week moja, nilikaa Atriums Hotel na nikaibiwa night ya nne, niliibiwa chumbani usiku wa saa 3 wakati nikiwa restaurant nakula hapo hapo hotelini... Niliibiwa digital camera 2, na simu aina ya HTC, na pesa taslim usd 2300.., mbaya zaidi mmiliki wa hotel anaitwa Erik Shingongo alifika hapo hotelin baada ya kupigiwa sim na meneja wake ndugu Sunday nilieripoti wizi huo muda huo huo. Shigongo aliniambia kuwa anawajua wezi nimpe muda wa saa 3 atarudisha vitu vyangu, baada ya masaa 3 kupita alikuja tena akiwa na maaskari 3 toka kituo cha polis kijitonyama na wakanitaka kutoa maelezo., na wakati huo, ikiwa saa 7 usiku shigongo aliniambia kuwa tayari kesha washika wezi wanne ambao ni wafanyakazi wa hotelini hapo HIVYO nitulie nitapata mali zangu.Nimesubiri bila mafanikio, nikapewa maelekezo ya kumwona RCO wa osterbay, kamanda Wambura ambae alitoa maagizo ya kuwepo mkutano kati yangu na shigongo na meneja wake bwana sunday, mkutano ufanyike ofisin kwa rco ili tuweze kukubaliana namna ya kurudisha vitu nilivyoibiwa. Shigongo hakutokea, meneja wake alifika na akiwa amepewa na maagizo na Shigongo kuwa msimamo wa hotel ni kutolipa au kutoa fidia ya aina yeyote, kuwa wao kama hotel wanaona ilikuwa ni kosa langu kwenda hotelin ATRIUMS. na pia alisema hakuna wa kumfanya lolote Tanzania hii hata nikiripoti kwa RPC, RCO akaridhia na akaniambia hana la kufanya na sheria haimpi nafasi ya kumbana shigongo.
hiyo ndo ilikuwa final na kesi ikafungwa, Tanzania ya watanzania raia hana haki, hadi polis wanaubariki wizi na kuutetea, pale ATRIUMS ni kichaka cha kufuga wezi, mwizi namba moja akiwa Erik Shigongo. namba 2 meneja wake na namba 3 team yake ya wafanyakazi, Kuweni makini msiumie kama mimi.

Pole sana kwa kuibiwa ki-malima malima ndugu yangu, and I can understand your frustration kwa tukio hili.
Sakata zima linaonyesha kuwa wizi ulikuwa an inside job, na wafanyakazi wanahusika, wangefahamuje kuwa kuna vita vya gharama na kuvitoa Kama si watu wandani ya hiyo Atrium Hotel.
Asante kwa kutujulisha Hilo kwani I have always suspected kuwa huyo Shigongo is a shady character na tabia aliyoionyesha ina confirm kuwa integrity Yake ni questionable.
Nilikuwa na wageni toka nje, na nitawa caution kwa hili sakata ki alitoa aibu.
Watanzania tunajaribu kuinuana lakini katika kibiana, Shigongo hapa lazima awekwe kwenye net kuwa Atriums ni pango la wezi.
 
Kuna vitu huyu jamaa hasemi, naamini hoteli hiyo ni standard hotel, kuna maelekezo juu ya ku declare valuables na naamini vyumba vina safe deposits na kama havina, kuna tangazo reception kuhusu pesa ndio maana mmiliki kamtoleo nje na kama haya ni kweli, nenda popote, imekula kwako!. Pole zake kuibiwa!.

ataachaje pesa reception wakati yeye anakula kuklekule hotelini kwenye restaurant ya hotel hajatoka nje, usimtetee huyu mlokole feki anatumia jina la Mungu kuficha maovu yake.
 
Kumbe erick anajifanya anamjua mungu ili afiche mabaya yake. mwangalieni anataka ubunge awamu ijayo ni kirusi hicho.
 
,
we nae mtu unaskia ana street university nawewe unaenda kulala kwake na mali?lazima wakufanyie praktiz
 
Pole sana, Hawakuchukua Sime au Panga??

Au wewe haukuwa na SMG ama Malima??
 
Mkuu pole sana,mimi nilshaibiwa hotelini dar na haki ya mungu siku hizi najiadhari kinoma,yaani niliibiwa nilipoenda kuoga asubuhi,na milango ilikuwa imefungwa kama kawaida ina maana ni wafanyakazi wa hoteli hiyo
 
We inaelekea huwa hulali hotelini so hujui haya mambo. Chumba kinatakiwa kiwe na sehemu maalum ya kutunzia vitu vya thamani, yaani kasafe fulani hivi. Kukabidhi mapokezi ni hotel za uswahilini, pale Atriums ni buku 70 halafu ni jirani sana na kona bar kama jamaa aliingia na MDUDU wanaweza kuwa wamem ADAM MALIMA. Shigogo my brother, its too LOW to pretend you are above the Law while you belong in group of very corrupt individuals in the country. Kumbuka ulikotoka Erick, umewadhalilisha sana akina dada katika magazeti yako ili uuze na umetajirika, nchi za watu ungefilisiwa. Watendee haki washkaji zako kina Ridhiwani wasilazimike kupindisha sheria kattika vitu vidogo kama hii ishu.
Shigongo kasahau alivyokuwa anauza kabumba pale makoroboi Mwanza,kisa hivyo vijisenti,pia kwa kufanya alivyofanya anaiharibia soko hoteli yake,kwani kwa uwezo alionao angeweza kumlipa huyo mteja wake ili asiharibie jina la hotel yake,mi nilifikiri jamaa kaelimika na anajua misingi ya biashara kumbe buure kabsa,kumpata mteja ni rahisi lakini kumrudisha tena ni kazi kubwa
 
aliyeeniibia ni mfanyakazi wa hotelin hapo anaitwa Daudi, ni mpishi, nilitoa order kwake ya kula nikiwa mapokezi na nikampa muda kamili wa kula, na wakati huo kwa bahati mbaya aliona cash iliyokuwa kwenye wallet wakati nafungua kulipa bills zangu, kwa maelezo ya mlinzi, baada ya hapo Daudi alimpigia sim mfanyakazi wa zamani wa hapo hotelini anaeitwa Brayton, ambae aliachishwa kazi kwa ajili ya wizi vyumbani. huyo Brayton alifika hapo pale tu nilipoingia restaurant kula, aliongozana na Daudi hadi chumbani kwangu na kisha Daudi akamfungilia mlango wa nyuma jikoni akatokea huko, lilikuwa tendo la kama dakika 10 tu. Mazingira yaliochangia mie kuibiwa ni ugeni tu, nilikuwa na mke wangu wa ndoa ambaye sio raia wa Tanzania, tumekaa hapo siku 4 bila tatizo, niliamua kuwa na cash sabab nilihofia kadi yangu ya bank kutofanya kazi nchini, ni cash ambayo niliichukua airport Amsterdam nikiwa njiani kwenda DSM. Baada ya shigongo kuonyesha hana nia ya kutorudisha mali zetu, na mie sina haki mbele ya polis wetu kama Mtanzania ndipo mke wangu akapiga sim ubalozi wao kulalamika, ofisa wa ubalozi(sweden) ndie aliyetupa mwongozo wa kuonana na RCO wambura ambaye aliifunga kesi kuwa hana uwezo wa ku deal na Shigongo, akatupa na mifano mingi wa watu wengi ambao wameshaibiwa hapo ATRIUMS na hakuna linalotendeka. kuweni makini na hiyo Hotel wakuu. mbaya zaidi, karatasi niliyopewa kusign inn yenye masharti juu upotevu hotelini hapo, Shigongo aliichana ilipotakiwa na police. Aliichana kwa maksudi tu ili kuuwa ushahidi unaombana yeye kumlipa mteja! Ni mbaya saana wakuu.
 
ataachaje pesa reception wakati yeye anakula kuklekule hotelini kwenye restaurant ya hotel hajatoka nje, usimtetee huyu mlokole feki anatumia jina la Mungu kuficha maovu yake.

hiyo karatasi ya ku declare inambana yeye, na aliichana, meneja wake kaileta polisi vipande tu ikiwa inaonyesha jina langu, sahihi yangu, maelezo yote kuhusu kuwa na mali chumbani kayachana. bila hata aibu.
 
Pole sana kwa kuibiwa ki-malima malima ndugu yangu, and I can understand your frustration kwa tukio hili.
Sakata zima linaonyesha kuwa wizi ulikuwa an inside job, na wafanyakazi wanahusika, wangefahamuje kuwa kuna vita vya gharama na kuvitoa Kama si watu wandani ya hiyo Atrium Hotel.
Asante kwa kutujulisha Hilo kwani I have always suspected kuwa huyo Shigongo is a shady character na tabia aliyoionyesha ina confirm kuwa integrity Yake ni questionable.
Nilikuwa na wageni toka nje, na nitawa caution kwa hili sakata ki alitoa aibu.
Watanzania tunajaribu kuinuana lakini katika kibiana, Shigongo hapa lazima awekwe kwenye net kuwa Atriums ni pango la wezi.

ATRIUMS ni pango la wezi, kamanda akiwa Shigongo mwenyewe, aliwaweka wafanyakazi wake 3 ndani, pamoja wezi 2 plus meneja wake, wezi wake anawajua wote sabab yeye ndio boss wao, naamin hata camera zangu ni yeye anayezitumia kwa sasa hivi.
 
Nazidi kupata ufahamu ni kwanini alitemwa kwenye mchakato wa ubunge huko kwao sengerema. Tuwe makini aishie kujiongoza yeye na familia yake, kama kweli alidiriki kunena matamshi hayo ya dharau na uzalilishaji.
 
Back
Top Bottom