Historia fupi ya DJ Sweet Francis Bundala

NGAYANIMO

Member
Joined
Feb 17, 2026
Posts
43
Reaction score
60
HISTORIA FUPI YA DJ SWEET FRANCIS BUNDALAIMG-20260217-WA0000.jpg

Sweet Francis jina kamaili ni Francis James Bundala,mwaka 1964 alianzisha bendi iliyoitwa The Screemers na Dj Sweet Francis akiwa mwimbaji(singer) hapo ndipo alipopewa jina la SWEET baada ya kusikia sauti yake na jinsi alivyokuwa akiimba iliwakuna sana na wakawa wanasema "YOUR VOICE IS SO SWEET " na ndiyo hapa akawa anaitwa Sweet. Hiyo ni hapa Dar.Bendi The Screamers ilidumu muda mfupi.

Mwaka 1965 alianzish a bendi nyingine ya watu 5 wakaiita The Hot Five wakawa wanapiga bugi kila Jumapili mchana hapo Arnatoglo hall Mnazi mmoja.

Wakawa wanashindana na bendi ilikuwa inaitwa The Flamming Star.
Mwaka 1967 June The Hot Five ikavunjika. 1967 Sept. Dj Sweet Francis na aliyekuwa Solo guitarist wakaanzisha bendi nyingine wakapata watu wengine 3 ambao walianza kuwafundisha ambao walikuwa mpiga bass, mpiga rythym na drummer. Bendi wakaiita The TONICS. Mwimbaji- Sweet, Solo- Michael Jackson, Rythym- Green Jackson. Bass- John Morand na Drums- Charles Alowasa.

Baada ya mazoezi makali mwezi November1967 wakaapata mkataba wa kupiga muziki kila siku hapo Splendid Hotel iliyokuwa inamilikiwa na mtaliano aliyeitwa MOSKA mtaa wa Samora zamani ukiitwa Independence Avenue.

Siku moja wakati wanapiga muziki jamaa mmoja ambaye hawakuwa na mazoea naye akaja kwenye stage akaomba apige bongos wakamruhusu, wakati Dj Sweet Francis anaimba na yule jamaa akawa amapiga bongos vizuri sana Dj Sweet Francis akawaambia wenzake kuwa anafaa kuwa drummer lakini wenzake walimkatalia na baada ya kuwasihi sana walikubali kwa sharti kuwa amfundishe kupiga drums mpaka ajue.

Baada ya kumfundisha kwa muda mfupi akaona ameelewa na baada ya kumpa nafasi kwenye stage alipiga drums na wenzangu wakamfurahia, huyo alikuwa anaitwa Adam Salehe Mwambile (R.I.P.) na tangu siku hiyo Dj Swett Francis akamwambia kuazia leo utaitwa ADDY SALLY, ilikuwa mwezi April 1968, hilo ndiyo lilikuwa chimbuko la ADDY SALLY.

May 1968 mkataba ulimalizika hapo Splendid wakaamua kwenda mikoani.Wakati wote huo Dj Sweet Francis alikuwa mfanyakazi wa NPF sasa ni NSSF.

Dj Sweet Franacis aliamua kuacha kazi maana alivutiwa sana na muziki. July 1968 walifika Arusha wakiwa wanamuziki 5 na fundi mitambo aliyejulikana kwa jina Joseph Magali.

Yule drummer wa kwanza .walimwacha baada ya kumwona Dj Addy Sally anafaa zaidi. March 1970 Dj Sweet Francis walirudi Dar. May1970 Dj Sweet Francis na Addy waliacha bendi kwa kutoelewana na Michael Jackson ambaye ndiye aliyekuwa kiongozi wa Bendi.

July 1970 Dj Sweet Francis alienda Mombasa na kuanza kuimba na Sunshine club. Mwezi Sept.1970 Dj Sweet Francis alimwita Dj Addy Sally Mombas akawa anapiga drums Central night club, May 1971 wakarudi wote Dar.

Wakati huo The Tonics wakiwa Nairobi waliwaita Dj Sweet Francis na Addy Sally huko, Dj Sweet Francis alikataa ila Dj Addy Sally akaenda.

Dj Sweet Francis akawa anaimba mara moja moja Simba grill Kilimanjaro Hotel wakiwa na bendi kutoka Spain iliyoitwa Los Valdos na hotel ikiwa ya chini ya raia kutoka Israel aliyejulikana kwa jina la LEVY na meneja mkuu wa hotel akiitwa FERGUSON raia wa Canada.
Kwa vile Africana hotel ilijengwa kutokana na faida ya pesa za Kilimanjaro hotel hivyo mmiliki alikuwa mmoja na mwaka 1971 ilianzishwa Gogo Disco baada ya kuhamisha disco kutoka Summit, Kilimanjaro hotel kwenda Afrikana.

Bokha Wilson alikuwa msanii wa Cabaret Simba grill pia kuwa Dj. Summit akahamishiwa Gogo disco hotel Africana. August 1972 Bokha Wilson akarudishwa Simba grill na Dj Sweet Francis akapelekwa Africana Hotel kuwa Disc Jockey Gogo Disco Theque.

Wote waliotajwa hapo mwanzo wameshatangulia mbele ya haki isipokuwa Dj Sweet Francis na Bhoka Wilson hatuna taarifa zake, miaka ya 80 alikuwa Ujerumani. baada ya kuwa Dj wa Gogo disco.
Mwisho wa mwaka wa 1972 alikuja Dj. Mactwist akaanza kupiga disco Sea view hotel, nalo likaitwa Sansui disco, Dj Mactwist hakudumu sana na badala yake Dj.Addy Sally akawa Dj hapo Sansui disco. Mwezi Nov.1973 Dj Sweet Frncis akapata mkataba mwingine wa kupiga disco Lusaka Zambia katika Club Lagondol.

Sept.1978 Dj Addy Sally alienda Lusaka kuwa Dj Club 2000 disco, huko Dj. Addy Sally alipata umaarufu sana kutokana na ujio wa James Brown, kwa kuwa mipigo ya drums nyimbo za James Brown Addy alikuwa anapatia sana. James Brown alifanya show Intercontinental Hotel na Addy Sally akampigia drums.

James Brown alimfurahia sana Addy Sally na siku ya pili James Brown akaamua kutembelea Disco la Addy Sally na ndipo Addy Sally alipopata umaarufu sana Lusaka. Dj Sweet Francis alienda Lusaka Jan.1979 kumtembelea Addy na kukutana na hizo sifa na Addy Sally akampa picha aliyopiga na James Brown ambayo Dj Sweet Francis anayo mpaka leo na mwisho wa Jan.1979 Dj Sweet Francis akarudi Dar. na Addy Sally akaendelea kupiga Disco hapo Club 2000, Lusaka.

Mwezi May 1979 Dj Sweet Francis alienda Bandari Grill ghorofa ya 6 New Africa Hotel, Makassy Orchestra walikuwa wanapiga hapo , Dj Sweet Francis akawa amekaa kwenye meza wakiwa wanne ila mmoja walikuwa hawafahamiani, baada ya bendi kupata mapumziko, Mzee Makasy alipita karibu ya meza waliyokuwa wamekaa Dj Sweet Francis na wenzake alipomuonana akamuomba wakirudi kwenye stage Dj Sweet Francis akaimbe wimbo wa kireno aliokua akiuimba Simba Grill.

Dj Sweet Francis alipanda kwenye stage na kuanza kuimba, cha ajabu kila mtu aliufurahia sana huo wimbo na walimshangilia sana na aliporudi mezani kwake, yule jamaa ambaye hakumjua alisimama akampa mkono akasema " Kumbe hapa tumekaa na mwanamuziki mzuri hivi, (akaendelea) Sikia kijana mimi najenga hotel hapo mtaa wa Uhuru na karibu kumalizika, hivyo ikiwa tayari wewe nataka uanze muziki hapo. Dj Sweet Francis akamkubalia, Hotel ikawa tayari Nov.1979 na kabla ya Dj Sweet Francis hajajiunga na Keys Hotel alipiga Disco kwa muda mfupi Mbowe Hotel na hapo ndipo alipomfundisha Dj.Jerry Kotto na Dj Sweet Francis akaanza kupiga Disco Keys Hotel Dec.1979.

Baada ya Addy Sally kurudi toka Lusaka, mwezi April 1980 wakawa pamoja hapo Keys Hotel akiwa vyombo vya Disco vipya kabisa vikiitwa M3. waliendelea pamoja hapo Keys Hotel lakini kufika Dec.1980 Dj Sweet Francis walishindwa kuelewana na Addy, ikabidi Addy aondoke.

Jan.1981 Dj Sweet Francis akawa na Dj. Seydou na baada ya muda kidogo Dj.Seydou akaondoka baada ya mzee Ndesamburo (R.I.P) kununua vyombo vya Disco na baada ya hapo Dj Sweet Francis akapiga Disco na Dj Johnson Pantaleo (R.I.P) na ndiye Dj Sweet Francis aliyemuacha Keys hotel,
June 1981 ndio ukawa mwisho Dj Sweet Francis wa kupiga disco.

Mwezi Sept.1981 Dj Sweet Francis alienda Ujerumani na nchi zingine za Ulaya, alirudi Dar. Sept.1983 baada ya mapumziko 1993 Oct. akaanza tena kuwa Cabaret singer hapo International Pub, Kijitonyama nyuma ya Sayansi na Teknolojia mpaka June-August 1994. Sept 1994 Simba Grill Kilimanjaro Hotel. Nov.2003--June 2004 Cine Club.

Hii ndiyo historia yake Deejay Sweet Francis Bundala ya katika tasnia ya muziki.HISTORIA FUPI YA DJ SWEET FRANCIS BUNDALA

Hii ndiyo historia yake Deejay Sweet Francis Bundala ya katika tasnia ya muziki.

Ukwaju wa kitambo
07675422027
 
Attachments

  • IMG-20260217-WA0000.jpg
    IMG-20260217-WA0000.jpg
    93.1 KB · Views: 21

Similar Discussions

Back
Top Bottom