Nimeibiwa ATRIUMS hotel Sinza. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nimeibiwa ATRIUMS hotel Sinza.

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Chacha wa Mwita, Mar 20, 2012.

 1. Chacha wa Mwita

  Chacha wa Mwita Senior Member

  #1
  Mar 20, 2012
  Joined: May 17, 2008
  Messages: 166
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Nilikuwa Dar Es Salaam kwa muda wa week moja, nilikaa Atriums Hotel na nikaibiwa night ya nne, niliibiwa chumbani usiku wa saa 3 wakati nikiwa restaurant nakula hapo hapo hotelini... Niliibiwa digital camera 2, na simu aina ya HTC, na pesa taslim usd 2300.., mbaya zaidi mmiliki wa hotel anaitwa Erik Shingongo alifika hapo hotelin baada ya kupigiwa sim na meneja wake ndugu Sunday nilieripoti wizi huo muda huo huo. Shigongo aliniambia kuwa anawajua wezi nimpe muda wa saa 3 atarudisha vitu vyangu, baada ya masaa 3 kupita alikuja tena akiwa na maaskari 3 toka kituo cha polis kijitonyama na wakanitaka kutoa maelezo., na wakati huo, ikiwa saa 7 usiku shigongo aliniambia kuwa tayari kesha washika wezi wanne ambao ni wafanyakazi wa hotelini hapo HIVYO nitulie nitapata mali zangu.Nimesubiri bila mafanikio, nikapewa maelekezo ya kumwona RCO wa osterbay, kamanda Wambura ambae alitoa maagizo ya kuwepo mkutano kati yangu na shigongo na meneja wake bwana sunday, mkutano ufanyike ofisin kwa rco ili tuweze kukubaliana namna ya kurudisha vitu nilivyoibiwa. Shigongo hakutokea, meneja wake alifika na akiwa amepewa na maagizo na Shigongo kuwa msimamo wa hotel ni kutolipa au kutoa fidia ya aina yeyote, kuwa wao kama hotel wanaona ilikuwa ni kosa langu kwenda hotelin ATRIUMS. na pia alisema hakuna wa kumfanya lolote Tanzania hii hata nikiripoti kwa RPC, RCO akaridhia na akaniambia hana la kufanya na sheria haimpi nafasi ya kumbana shigongo.
  hiyo ndo ilikuwa final na kesi ikafungwa, Tanzania ya watanzania raia hana haki, hadi polis wanaubariki wizi na kuutetea, pale ATRIUMS ni kichaka cha kufuga wezi, mwizi namba moja akiwa Erik Shigongo. namba 2 meneja wake na namba 3 team yake ya wafanyakazi, Kuweni makini msiumie kama mimi.
   
 2. The Hunter

  The Hunter JF-Expert Member

  #2
  Mar 20, 2012
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 1,049
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Pole bana, ndo yule jamaa anaejinadi kufundisha watu ujasiria mali?!!.. pole ndugu yetu siku nyingine nenda hotel zenye kutambulika na zenye ulinzi imara.
   
 3. Arabii

  Arabii Member

  #3
  Mar 20, 2012
  Joined: Dec 23, 2011
  Messages: 30
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Pole sana, da ndo ujacriamali wa shigongo huo.
   
 4. Jestina

  Jestina JF-Expert Member

  #4
  Mar 20, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 4,807
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  duh pole,hivi hotelini sio kama guesthouse kuwa unatakiwa uache vitu reception kama unatoka??????kama ndio hivyo usiwalaumu....kama sivyo,then kata rufaa mkuu they should be made accountable for the loss.......
   
 5. Donnie Charlie

  Donnie Charlie JF-Expert Member

  #5
  Mar 20, 2012
  Joined: Sep 16, 2009
  Messages: 6,581
  Likes Received: 848
  Trophy Points: 280
  pole sana kamanda ila si ustaarabu kuacha pesa kiasi hicho hotelini, naamini kilichowatamaanisha hao ni pesa tu na hivyo vingine ilikuwa kama nyongeza tu.
   
 6. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #6
  Mar 20, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,874
  Likes Received: 6,228
  Trophy Points: 280
  ukiwa hotelini valuables zako beba, sasa unaachaje pesa chumbani?

  Tena usd mbona zinafit vyema kwenye wallet?

  Halafu ukiona mtu anauza magazeti yamejaa ngono, kufumaniwa uchawi nk sio wa kumuamini,hata hoteli zake zikimbie....
   
 7. idawa

  idawa JF-Expert Member

  #7
  Mar 20, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 18,540
  Likes Received: 10,465
  Trophy Points: 280
  shigongo huyu mwenye magazeti ya udaku..halafu jamaa kila anachoongea lazima amtaje mungu. hii ngumu kuamini.
   
 8. kanyasu

  kanyasu JF-Expert Member

  #8
  Mar 20, 2012
  Joined: Feb 9, 2009
  Messages: 235
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Pole sana lakini jofunze kuweka fedha bank mambo ya kutembea hotel na dola 2300 ni uzembe.
   
 9. Monstgala

  Monstgala JF-Expert Member

  #9
  Mar 20, 2012
  Joined: Aug 25, 2009
  Messages: 1,082
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 145
  Mkuu, pole sana ila chumba cha hoteli hasa za kwetu (tz) si salama hivyo kiasi cha kuacha vitu kwa muda wa zaidi ya robo saa. Ni wazi wafanyakazi wa hapo wamekufanyia huo unyama kwa kujua sheria ya kuacha valuables reception itawalinda. Shigongo ni opportunist, ili mradi anapata faida basi wanaoumia kwa "ujasiriamali" wake si lolote.
   
 10. mzurimie

  mzurimie JF-Expert Member

  #10
  Mar 20, 2012
  Joined: Oct 16, 2011
  Messages: 6,151
  Likes Received: 1,604
  Trophy Points: 280
  uliweka pesa kwenye safety box nasema zile zinazo funguliwa kwa vinamba unayoseti mwenyewe?

  bila hivyo ni tabu sana, ni njama ya watu wote wa hapo hotelin labda huyo Eric anawatuma mwenyewe wawaibie wateja

  ni no go area hiyo hoteli wadau.

  pole
   
 11. mzurimie

  mzurimie JF-Expert Member

  #11
  Mar 20, 2012
  Joined: Oct 16, 2011
  Messages: 6,151
  Likes Received: 1,604
  Trophy Points: 280

  ndio yeye ni mwizi duh aibu sana
   
 12. Kipis

  Kipis JF-Expert Member

  #12
  Mar 20, 2012
  Joined: Jul 23, 2011
  Messages: 493
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Wakuu angalieni sana hoteli zingine wanafunga camera maalumu ambazo hata mteja huwezi kuziona. Hiyo yote ni kutengeneza mazingira ya kutokea vitu kama hivyo. Waswahili wanasema "asifuye mvua.....!!
   
 13. Dingswayo

  Dingswayo JF-Expert Member

  #13
  Mar 20, 2012
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 4,011
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Ilikuwa Nashera ya Morogoro, sasa Atriums ya Dar, sasa hotel gani yenye usalama? Hili ni doa kwa hiyo hotel.
   
 14. S

  Shansila Senior Member

  #14
  Mar 20, 2012
  Joined: Jan 28, 2012
  Messages: 189
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Pole sana,hiyo hotel ni ya kuchinjia vya pori(hotel ya wazinzi),hivyo uhuni na umafia wa kila aina lazima uwepo!Next time nenda hotel zenye security na pia angalia visitors register,ukiona wageni wengi wanatoka Dar kwenda Dar ogopa!Next time nenda Landmark,Blue Pearl na zingine za hadhi hiyo.Na chukua ushauri wa wadau kuwa:bank your money,handover your valuables at reception & trust nobody but yourself!
   
 15. n

  nndondo JF-Expert Member

  #15
  Mar 20, 2012
  Joined: Feb 1, 2010
  Messages: 1,250
  Likes Received: 535
  Trophy Points: 280
  Jamani ndugu zangu, hebu acheni kuwa watu wakusukumwa na kila mtu akiwemo huyu mkunga, kama uliibiwa nenda kaweke mwanasheria acha ubahili persue hiyo kesi hata miaka 100 people are getting away with murder, yaani unaweka na kupokea hela za wateja halafu unasema huwajibiki na wao kuibiwa hotelini kwako? hata mgeni anayetutembelea majumbani kwetu tunawajibika juu ya upotevu wa mali zao na usalama wao wakiwa ndani kwetu, kwa hiyo ukiwa hapo hotelini ukaingiliwa na kuumizwa ama kuuawa bado hutaki kuwa responsible?, hivi kweli kwa nini tuna simplify maisha yetu hivi? mnataka kuniambia kuna authority inayotoa kibali shigongo afungue hoteli lakini asiwe responsible for mali na maisha ya wateja wake? sasa hii ni hoteli ama machinjio? Nakataa kabisa hakuna mahali penye sheria kama hizi, ni sisi watanzania na upumbavu wetu kama tunaoufanya hapa tunaohalalisha ushenzi wa watu wenye vijisenti kama hivi, hebu weka wanasheria waulize, kwa hiyo hao askari hapo wanafanyanini? ama wanamlinda yeye mwenyewe na vitu vyake? tusijibweteke hela ulizoibiwa na mali ni kubwa sana weka nusu ya hizo mpeleke mahakamani hata kama anamamilioni ashughulikiwe hii haikubaliki
   
 16. Ulukolokwitanga

  Ulukolokwitanga JF-Expert Member

  #16
  Mar 20, 2012
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 8,418
  Likes Received: 3,905
  Trophy Points: 280
  We inaelekea huwa hulali hotelini so hujui haya mambo. Chumba kinatakiwa kiwe na sehemu maalum ya kutunzia vitu vya thamani, yaani kasafe fulani hivi. Kukabidhi mapokezi ni hotel za uswahilini, pale Atriums ni buku 70 halafu ni jirani sana na kona bar kama jamaa aliingia na MDUDU wanaweza kuwa wamem ADAM MALIMA. Shigogo my brother, its too LOW to pretend you are above the Law while you belong in group of very corrupt individuals in the country. Kumbuka ulikotoka Erick, umewadhalilisha sana akina dada katika magazeti yako ili uuze na umetajirika, nchi za watu ungefilisiwa. Watendee haki washkaji zako kina Ridhiwani wasilazimike kupindisha sheria kattika vitu vidogo kama hii ishu.
   
 17. LUPITUKO

  LUPITUKO JF-Expert Member

  #17
  Mar 20, 2012
  Joined: Sep 19, 2011
  Messages: 275
  Likes Received: 112
  Trophy Points: 60
  Mkuu bila kutafuna maneno wewe ni mzembe! Sijapenda ulivyoibiwa ila inamaana wewe ni mara ya kwanza kulala hotel? Mbona sheria za hotel zipo wazi dunia nzima kwamba valuables tembea nazo or kabidhi reception! Wewe uliachaje chumbani ukaenda kula? Bt more so walijuaje wewe ni pedejee lazima ulionesha mazingira ya kujifanya uko njema wakakutime. Kwa hilo Shigongo humuwezi coz sheria zipo waziiii!
   
 18. mopaozi

  mopaozi JF-Expert Member

  #18
  Mar 20, 2012
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 3,290
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  We hujamalizia vyote uliibiwa pia na laptop 3 za 5m,blackberry 3 za 5.5 m pete mbili za shaba za 2.5m,tsh 1.5m,na mabegi ya nguo matatu hawawezi kukulipa kwakuwa ulipoingia ulipewa masharti yao kuwa vitu vya thamani uviache reception hukuacha,na pili wameandika kabisa kulala at ur own risk na pia kamera zimekurekodi ukiingia na dada mweupe mrefu usiku ambaye hoteli haimtambui kwakuwa uliingia kama single na si double!!
   
 19. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #19
  Mar 20, 2012
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Pole sana mwaego !
   
 20. k

  kaeso JF-Expert Member

  #20
  Mar 20, 2012
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 551
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Wameku-adam malima, pole sana!
   
Loading...