Nimedisko kisa kibomu (kibuti) . Nifanyaje?

Nimepata bahati mbaya Kwenye UE nimedakwa na kibomu na kuitwa offic. Nimedisko nipeni ushauri.. Usitukane.. Ni bahati mbaya. Asante
pole sana ni hali ya kawaida usijute maana uliyataka mwenyw ulishindwa kupig chabo mpk uingie na kibuti
umeniuuzi kama nini maana me ni mpiga chabo mzuri il kamwe siingii na kibuti katk paper

so....hakunaa namna apo ni kuomba tena mwakani
 
Kuna rafiki yangu mmoja alisoma PCB alipata nafasi SUA, alikua na akili wala si za kubabaisha, baada ya mwaka mmoja SUA alirudi flat, kwa kweli tulisikitika sana lakini alitumia cheti chake cha six kuomba UDSM alipata na maisha yakaendelea.
 
mkuu ungeomba ushauri wa kupiga chabo na kuingia na nondo kwenye pepa haya yasinge kukuta.....mm katika hayo maswala nina phd na soon natoa kitabu cha jinsi ya kupiga chabo bila kukamatwa.....

na nina rekodi za kutosha za kupiga chabo katika vyumba vya mitihani vilivyoshindikana na wasimamizi wanaaa africa mashariki na kati...

ili hayo yasikukute tena ni pm upewe mbinu adimu zilizomkalisha chini prof mnaa tz nzima
 
Nimepata bahati mbaya Kwenye UE nimedakwa na kibomu na kuitwa offic. Nimedisko nipeni ushauri.. Usitukane.. Ni bahati mbaya. Asante
Najaribu kuielewa hali ulonayo kwa sasa,kwanza kadhia ya kukamatwa na kombora hilo mbele ya wanafunzi wenzio na pili kudisco ila wacha nkwambie kitu mshikaji wangu huo sio mwisho wa maisha na maisha hayajawahi kwenda straight na hayatokaa yaende straight,unaanguka mara saba unanyanyuka mara nane.
Fanya taratibu za kuomba chuo kingine then endelea na shule.
 
Back
Top Bottom