Nimechukia sana Simu za Samsung, bora TECNO tu

Nimechukia sana Simu za Samsung, bora TECNO tu

Mkuu acha kufananisha Samsung na vitu vya ajabu. Hivi uko serious kweli? Kwanza inatia mashaka mtu kuhama tecno hadi flagship ya Samsung. Siku nyingne ukitaka kununua kitu km huna uzoefu omba msaada kwa wazoefu. Hapa natype na Samsung ya 4 kumiliki na sioni pa kwenda.
Kitu Super Amoled+ display, acha masihara mkuu ila nlikuwa nachomekea tu.
Jmn mnisaidie,nahitaji Samsung, duh mpk naogopa kupata fake!
Nilitumia kitambo,baada ya kuibiwa nikatumia tecno duh nataka nirudi
 
Mnaonunua simu kariakoo, makumbusho mnaambiwa mpya wengi mnapigwa.

Sio kwamba ni feki bali zinajulikana kama refurbs.

Yaani simu original zilizokua na matatizo mbalimbali zikatengenezwa kwa kubadilishwa parts zenye shida.

Refurbs hazina ubaya ila tatizo ni kwamba refurbs zote au asilimia 99 zinatoka china.

Mchina anakusanya simu zilizoharibika ana repair na parts za hovyo, kuanzia vioo, camera, battery, na component nyinginezo lengo ni kutumia gharama ndogo kadri awezavyo kisha zinakuwa packed kwenye mabox yake pamoja na chargers, earphone manual, full sealed ukiikuta kariakoo unaambiwa mpya.

Ukitaka samsung, mpya isiyo na longolongo nenda kwa samsung stores au authorised dealers wale wanazo brand new, ila tu bei zimesimamia ukucha inabidi uvumilie kwenye bei.

Chukua hii.
Asante aisee kwa kunielewesha,nilikuwa najiuliza ni kitu gani hiki "refurbs"
 
Yeah weka
Cat S41
cat-s41-0.jpg
 
Mie mtumiaj wa Samsung na niko tayar kwa lolote na muda wowote, kizur kina gharama.
 
Nunua online kama vile kutoka aliexpress.Hakuna kazi ngumu kama kununua/kupata simu original bongo.Ni heri upewe kipande cha shamba ulime kwa jembe la mkono kuliko kufanya kazi ya kupata simu original Bongo.Nyingi ni fake,copy na refurbished lakini wanazipack vizuri kuliko simu original zenyewe!Na mbaya zaidi wanaziuza bei ya simu original
Duh[emoji144][emoji144]
 
Samsung simu zao zipo katika category 3 kubwa

1.Note series ni special kwa kipato kikubwa

2.S series ni special kipato cha kati

3.A series (J series) watu wa kupato cha chini (kwa hiyo hera yako unaweza kupata A series na hazina ubora kivile) angalau kama ukipata J series kidogo ni ngumu ila ni za zamani kidogo
Na Z series?
 
Jmn mnisaidie,nahitaji Samsung, duh mpk naogopa kupata fake!
Nilitumia kitambo,baada ya kuibiwa nikatumia tecno duh nataka nirudi
Mkuu ukitaka simu original inabidi ununue kwa dealer wa kuaminika, hasa anayeagiza mwenyewe au wakala wa kampuni, afu pia jaribu kununua simu ambayo haijakaa sana sokoni tangu itoke, vingnevyo tafuta mtaalamu akusaidie kununua (kukagua).
Pia km una access ba Arusha feki siyo nyingi km Dsm.
 
"SAMSUNG IS AS GOOD AS LONG AS IT HASN'T A BROKEN SCREEN"[emoji13]

Ikipasuka ni msiba wakati vioo vya tecno ni elfu 50 tu your are back in business.
Kwasisi walevi hazitufai kabisa nilikua na A50 haikukaa week 2 kioo kikaenda kwao...ikabidi nikate glass nakuweka nyingine.

Nataka nirudi kwenye xiaomi au oppo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom