Unaongelea Huawei aina ganiTatizo la Itel,Huawei, Tecno na Infinix ni kukwama kwama, inakera sana
Kibaha sehemu gani?Me A50 yangu nimepasua kioo cha kamera kwa nje mkuu, hivi kinarudishika au ndo kwisha habari yake?
Kwamathias msikitiniKibaha sehemu gani?
Ndo maana unaambiwa kula urefu wa kamba yako, hapo wewe uliforce kumudu usichokimuduMwaka jana mwezi wa 9 nilinunua simu ya Samsung S9+, niliachana na matumizi ya Tecno na Infinix. Baada ya muda kwa bahati mbaya simu ilianguka, na kupasuka kioo.
Ilianza kunisumbua sana, hatimaye ikazima moja kwa moja. Inaonekana hata kioo chake hakiko imara.
Shida nilipokwenda kubadili kioo, Mungu wangu sikuamini , nilijua mafundi wanataka kunipiga, nimezunguka wee mpaka nikachoka, lakini bei ni ileile.
Mwisho nilipata mahali laki tatu na nusu, fundi 20 jumla 370,000/= . kwa usawa huu jamani mi naitoa wapi? Nimeichukia sana, sina hamu nayo tena. Kama ningejua mapema nisingenunua bora ningeendelea tu na hii TECNO yangu
Mwezi wa 10 nilimchukulia mtu kioo cha S9 kilikua kipo fresh kabisa kwa 400,000, hadi saaa hivi anadunda nacho vizuriYah vya Kariakoo ni feki kweli. Haziwezi kuwa true Amoleds.
Mnaonunua simu kariakoo, makumbusho mnaambiwa mpya wengi mnapigwa.
Sio kwamba ni feki bali zinajulikana kama refurbs.
Yaani simu original zilizokua na matatizo mbalimbali zikatengenezwa kwa kubadilishwa parts zenye shida.
Refurbs hazina ubaya ila tatizo ni kwamba refurbs zote au asilimia 99 zinatoka china.
Mchina anakusanya simu zilizoharibika ana repair na parts za hovyo, kuanzia vioo, camera, battery, na component nyinginezo lengo ni kutumia gharama ndogo kadri awezavyo kisha zinakuwa packed kwenye mabox yake pamoja na chargers, earphone manual, full sealed ukiikuta kariakoo unaambiwa mpya.
Ukitaka samsung, mpya isiyo na longolongo nenda kwa samsung stores au authorised dealers wale wanazo brand new, ila tu bei zimesimamia ukucha inabidi uvumilie kwenye bei.
Chukua hii.