Nimechukia sana Simu za Samsung, bora TECNO tu

Nimechukia sana Simu za Samsung, bora TECNO tu

khadijaa

Member
Joined
Oct 17, 2020
Posts
82
Reaction score
204
Mwaka jana mwezi wa 9 nilinunua simu ya Samsung S9+, niliachana na matumizi ya Tecno na Infinix. Baada ya muda kwa bahati mbaya simu ilianguka, na kupasuka kioo.

Ilianza kunisumbua sana, hatimaye ikazima moja kwa moja. Inaonekana hata kioo chake hakiko imara.

Shida nilipokwenda kubadili kioo, Mungu wangu sikuamini , nilijua mafundi wanataka kunipiga, nimezunguka wee mpaka nikachoka, lakini bei ni ileile.

Mwisho nilipata mahali laki tatu na nusu, fundi 20 jumla 370,000/= . kwa usawa huu jamani mi naitoa wapi? Nimeichukia sana, sina hamu nayo tena. Kama ningejua mapema nisingenunua bora ningeendelea tu na hii TECNO yangu
 
Kioo cha samsung kitu quality sio kama kioo cha tecno ........kabla hujanunua unatakiwa uelewe na gharama za ziada pia kama utapata majanga....na sio Samsung tu ni simu zote zenye vioo vya uhakika achana na hizi screen za wachina kioo ndo bei ya simu kama ilivyo kioo cha tv hizi za makampuni makubwa ndo bei ya tv yenyewe
 
Mambo mengine ni ya kujitakia, mm natumia simu kubwa tu (ila sio brand ya Samsung) imepasuka kioo balaaaa! Michirizi kama mwanamke mnene aliyetoka kujifungua, lakini ngoma bado inadunda. Sometimes hadi naionea huruma infact angekuwa ni binadamu katika hali hii ningeshamzika
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom