Nimechukia sana Simu za Samsung, bora TECNO tu

Nimechukia sana Simu za Samsung, bora TECNO tu

Mwaka jana mwezi wa 9 nilinunua simu ya samsung S9+, niliachana na matumizi ya Tecno na Infinix. Baada ya muda kwa bahati mbaya simu ilianguka, na kupasuka kioo.

Ilianza kunisumbua sana, hatimaye ikazima moja kwa moja. Inaonekana hata kioo chake hakiko imara.

Shida nilipokwenda kubadili kioo, Mungu wangu sikuamini , nilijua mafundi wanataka kunipiga, nimezunguka wee mpaka nikachoka, lakini bei ni ileile.

Mwisho nilipata mahali laki tatu na nusu, fundi 20 jumla 370,000/= . kwa usawa huu jamani mi naitoa wapi? Nimeichukia sana, sina hamu nayo tena. Kama ningejua mapema nisingenunua bora ningeendelea tu na hii mitecno yetu
Pole sana.
 
"SAMSUNG IS AS GOOD AS LONG AS IT HASN'T A BROKEN SCREEN"[emoji13]

Ikipasuka ni msiba wakati vioo vya tecno ni elfu 50 tu your are back in business.
Nimekata nayo tamaa, nilienda mliman city, wanauza laki sita na nusu, karikoo na laki tatu na nusu, nahisi vya kariakoo ni feki
 
Mambo mengine ni ya kujitakia, mm natumia simu kubwa tu (ila sio brand ya Samsung) imepasuka kioo balaaaa! Michirizi kama mwanamke mnene aliyetoka kujifungua, lakini ngoma bado inadunda. Sometimes hadi naionea huruma infact angekuwa ni binadamu katika hali hii ningeshamzika
Aisee!!!
 
Kama mtu ulikua unatumia tecno na infinix kisha ukahamia kwenye simu za samsung huwezi rudi nyuma tena, labda kama uchumi umekaa vibaya kidogo. Waliowahi kutumia hizi simu zote watakua wmenielewa.
Muhimu ni utunzaji ila samsung ni bab kubwa.
Sijasema sio nzuri, iliponishinda ni hapo kwenye kioo , bei ya simu mpya nyingine hapana kwa kweli
 
Samsung ni kioo sisi watumiaji tunalielewa hilo tu....na tuko tayari..
Ndio shida ya kudandia gari kwa mbele,mm mwenyewe siipendi Samsung kwa sababu ya hiyo. Kioo unanunua simu kali Tecno au infinix!!!🤪
 
True !! Cmu kauziwa fake tena copy kabisa alafu kioo alichotaka kununua pia fake
Labda kioo, kwa simu hapana sio fake, kwa sababu kuna kioo mahali nilikuta laki sita na nusu na kwingine laki tatu na nusu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom