Nimeanza maisha mapya kama Vegan

Nimeanza maisha mapya kama Vegan

Kwenye hii dunia kila mtu aishi anavyotaka, binafsi siwezi kuacha kula nyama...ni tamu sana. Hapa penyewe nimetoka kula ugali na kuku wa kienyeji.

Kuna rafiki yangu mmoja aliposti status ngamia akiwa anachinjwa kwa chini akaweka maneno kuwa hiyo video imemuumiza na hatokula nyama tena. Siku moja nikaenda kumtembelea nikakuta kapika ugali nyama, nikamuuliza mzee vipi, si ulisema umeacha kula nyama? Akanambia "Naachaje kula nyama mzee!!?"😀😀😀
 
That's it 👌🏾 kila mtu aishi maisha anavyotaka.
 
Habari 👋🏾

Siku ya leo nikiwa natimiza miaka kadhaa nimekuwa VEGAN rasmi. Hatua hii nimekwisha ianza muda toka 28 January, hivi sasa naendeleza nadhiri hii rasmi katika mfumo wa maisha yangu.

Nimekuwa nikijiuliza utajiita vipi mwenye upendo, heshima au mtu unayejali hisia na kuheshimu wengine ikiwa umeshindwa kuheshimu uwepo wa viumbe wengine kama wanyama, ndege na wengineo?

Kwa kujali na kuona umuhimu wa kila kiumbe nimekuwa nikivijali viumbe vyote mfano, huwatengea waramba sukari kiasi chao pasi ya kuwapatia bugdha, uhifadhi mayai ya kuku na kutotoa wengine kuendeleza uzao wao, hutembea na wanyama mbalimbali katika maeneo kadhaa waweze kijihisi umiliki nk.

Leo nimepanda miti 28 maeneo yayonizunguka na miti 21 maeneo ya umma katika shule 2, hospitali, eneo la jeshi, kituo cha wasiojiweza na watoto waishio mazingira hatarishi na katika ofisi za wilaya.

View attachment 1766453

Nikiwa kama kijana anayezingatia maisha halisi leo ni wazi sitotumia tena bidhaa zinazotokana na wanyama na viumbe mbalimbali. Hili linaambatana na masuala kadhaa katika mfumo wangu wa maisha ninaoendelea kuufuata ikiwa ni pamoja na;-

  • Sishiriki mapenzi (Sex)
  • Situmii vinywaji kemikali (Processed Drink's)
  • Situmii bidhaa zenye sukari ongezwa (Candy's)
  • Situmii bidhaa zinafanywa majaribio kwa wanyama
  • Nimejiweka mbali na uovu na negativity ya aina yoyote
  • Sifungamani na upande wowote

Nahijisi mwenye furaha na amani, najiona mshindi. 😊

Sergio
Kabla sijakuunga mkono kwa uamuzi wako naomba kujua faida zake kimwili na kiroho pia...
 
Kabla sijakuunga mkono kwa uamuzi wako naomba kujua faida zake kimwili na kiroho pia...
Faida ni nyingi hakika maradhi ya sukari, shinikizo la damu, inflammation, matatizo ya ngozi, hali ya umakini, kutokuwa/kupunguza stress and so many more. Kiroho ni nguvu zaidi baina ya roho, nafsi, nature na muumba hakuna doubt wala vikwazo.
 
Back
Top Bottom