Nimeandaa milioni 1, nataka kujenga chumba na Sebule

Nyuki Mdogo

JF-Expert Member
Oct 31, 2021
4,138
10,540
Habari wa nzengo (salaam kutoka Jijini Mwanza)

Mimi ni kijana mpambanaji. Nimekua katika hustles kwa muda mrefu sasa naona milango ya baraka inafunguka na mimi sitaki kuchezea nafasi. Mwisho wa mwezi uliopita nilibahatika kununua kiwanja kwa bei ya kugalaliza vibaya sana.

Size ya kiwanja ni 25*23 hatua zangu za miguu.

IMG_20220529_173623_915.jpg
IMG_20220529_173623_915.jpg


Kiwanja kina msingi wa vyumba viwili, sebule na choo & bafu. Wana ndugu, nimehamasika sana kujenga nyumba ya mwendokasi; chumba na sebule. Budget yangu ni milioni 1. Baadhi ya raw materials kama mchanga na maji ni vya bure maana nachota kando ya mto.

Tofali nanunua za choma. Fundi kanishauri nijenge kwa kutumia Molam.

Naombeni maoni na ushauri
 
Habari wa nzengo (salaam kutoka Jijini Mwanza)

mimi ni kijana mpambanaji. Nimekua katika hustles kwa muda mrefu sasa naona milango ya baraaka inafunguka na mimi sitaki kuchezea nafasi.

Mwisho wa mwezi uliopita nilibahatika kununua kiwanja kwa bei ya kugalaliza vibaya sana.

size ya kiwanja ni 25*23 hatua zangu za miguu.
View attachment 2254960View attachment 2254960

Kiwanja kina msingi wa vyumba viwili, sebule na choo&bafu.

wana ndugu, nimehamasika sana kujenga nyumba ya mwendokasi; chumba na sebule.

Budget yangu ni milioni 1.

Baadhi ya raw materials kama mchanga na maji ni vya bure maana nachota kando ya mto.

Tofali nanunua za Choma

Fundi kanishauri nijenge kwa kutumia Molam.

Naombeni maoni na ushauri
Mkuu hongera sana. Wewe anza tu ujenzi utakapoishia utaendeleza Mungu ataendelea kukufungulia milango ya fedha
 
Kwa nini hadi uje uulize JF...

Tafuta fundi na ufanye hesabu ya vifaa vitavyohitajika mfano idadi ya tofali, mifuko ya simenti, mbao, nondo, hela ya mafundi...

Ukishakuwa na hesabu hiyo, linganisha na pesa uliyonayo...
 
  • Thanks
Reactions: Cyb
Kaa chini piga mahesabu kukadiria idadi ya tofali zitakazotumika, zidisha kwa bei ya kila tofali hadi hapo site. Jumlisha pesa ya funndi na vibarua, chakula, nondo za lenta, mbao za lenta iwe za kukodi au kununua halafu jipime kwa urefu wa kamba yako.

Ukiona kamba ni fupi piga hadi level ya madirisha, piga lenta kuzuia kubomoka kwa ukuta, kisha rudi kuchakalika tena na ukipata unarudia unaanzia utakapokuwa umeishia- level ya madirisha au lenta ya juu kabisa juu ya madirisha
 
Back
Top Bottom