cheusimangala
JF-Expert Member
- Feb 27, 2010
- 2,585
- 497
Ndugu zangu,nimewajua freemasons muda kidogo hata kabla mtandao haujawa sehemu ya mawasiliano kwa watanzania.Mwanzoni nilikua nafahamu kwamba ili uwe freemason ni LAZIMA uwe TAJIRI MKUBWA na mtu mzito katika jamii.Nilijua kwamba Freemasons hawakufanyi tajiri lakini ni mtandao unaowafanya watu wazito duniani kama kina Bill Clinton,Jay z,Obama Queen Elizabeth na wengine kama hao kuwa Powerful pindi wanapokua members maana wote tunajua umoja ni nguvu sasa imagine umoja wa watu wenye nguvu duniani unavyoweza kuwarahisishia member wake kuwa untouchable na pia kwa pamoja kuweza kuicontrol dunia.Mtu kama Kanumba au Richard Mziray wana pesa gani ya kuwafanya wawe kundi moja na jay z na bill clinton ambao wanasemekana ni mafreemason?
Kinachonichekesha ni kwamba tokea watanzania tujue ufreemason basi kila kitu ni cha mafreemason kila mtu ni freemason yaani hadi waendesha maguta na wachoma kuku eti nao ni mafreemason kisa wanaweka swaga za vidole za kifreemason wakati ni utamaduni wetu kuiga iga kila kitu anachofanya gangster wa marekani,nakumbuka enzi Nelly anaweka kiplaster usoni kila mjanja wa kibongo naye aliweka bahati mbaya enzi zile wabongo walikua hawajaujua ufreemasson maana ile pia ingeambiwa ni sign ya freemason.
Wabongo naona mnakuja kasi sana na ulimbukeni wa kujifanya kuujua sana ufreemason ila taratibu tu tusije tukakolewa na hii imani hadi tukafikia kuwachoma jirani zetu kwa kuwahisi wanamuabudu Shetani kisa labda baba na watoto wao wanavaa t.shirt kama zile za Kanumba.Sina imani na wabongo linapokuja swala la kuamini mambo ya kipuuzi ndo maana wazee wetu walichomwa moto eti kisa wana macho mekundu hivyo ni wachawi,mngewanunulia majiko ya umeme waache kupuliza kuni wakati wa kupika muone kama wangekua na hayo macho mekundu.
Sasa hivi Cheusie nikipata kautajiri ka ghafla kasikoeleweka chanzo chake watu wataanza yule ni freemason,huoni hata avatar yake iko kifreemasson kabisa kumbe mim labda ni muuza madawa ya kulevya,jambazi au fisadi.Sasa hamuoni ufreemason unaweza kuwa kivuli cha majambazi,wauza unga na mafisadi kujilia vyao bila bugtha maana bora kama mim ni muuza unga au jambazi lakini jamii yangu ikaniona kuwa mim ni freemason si salama kwangu maana ufreemason sio uvunjaji wa sheria.
Bado najichunguza kujua kama Kibongo bongo na mim ni freemason au la.