Uchaguzi 2020 Nimeamua kura yangu asubuhi na mapema Lissu atapata

Jun 17, 2020
75
268
Mwanzo Mimi nilikuwa namkubali Magufuli lakini hizi hapa ni sababu ambazo zinanifanya nimpe Rais wangu Lissu kura

1: Mpaka sasa hivi hamna aliyejibu hoja za Lissu kwa ufasaha!

2: Magufuli anachuki ya waziwazi tena inaonekana ni Mtu katili kwa vitisho anavyovitoa kwamba tusipochagua CCM na watu wake, hatatuletea maendelea hii kauli inakera tena inaudhi sana cjui kama yeye unajua! Alafu anaotuambia ni watu wazima wenye akili zetu! Anatulazimisha tuchague jambazi ilimradi yupo CCM? Sisi ni watoto?! Hizo hela anatoa mfukoni mwake! Kwa kauli hii kura Yangu hapati!

3: Tumeona viongozi wengi wa upinzani wakitekwa na kuuliwa na wengine kuuliwa hadharani( mawazo), hajawahi kutoa tamko lolote hadharani la hata kukemea lakini yule wa iringa katoa tamko hadharani, hizi chuki za waziwazi kwa upinzani, Kura Yangu hapati!!!!

4: Kitendo cha kuwaengua wapinzani peke yao, Hamna hata mbuge au diwani wa CCM hata mmoja aliyeenguliwa huu uonevu wa waziwazi kwa wananchi, wananchi tunaumia sana, kutuletea Mtu eti kapita bila kupingwa na jimbo lina watu zaidi 100,000 ni upuuzi wa hali ya juu! ( Magufuli hapati kura Yangu)

5: Magufuli ndiye kiongozi wa serikali alitakiwa awe mfano kwa wengine lakini amekuwa yeye wa kwanza kuvunja maadili ya uchaguzi NEC haifanyi chochote NEC ipo kwa ajili ya upinzani tu wala CCM , wananchi tunaona yanayofanyika!

6: Upinzani upo mioyoni mwa watu akina mbowe ni wawakilishi ttu, wanavyoonewa ndivyo mnavyotuonea wananchi, tuna makovu mengi sana tuliyoumia miaka 5, CCM mnasema mmefanya Maendeleo lakini wananchi hawana Amani, hawapo guru!

6: Suala la vitambulisho wengi hawakumuelewa lissu,mliojaribu kujibu mnatetea matumbo tu! Kuna watu vijijini wanafanya biashara kwa msimu tu sio siku zote, mfano mm Nina ndizi zangu shambani, nikipata mkunga wangu mmoja upo tiyari naenda nauza, alafu nasubiria tena, lakini nadaiwa 20,000 kwa ajili ya kitambulisho, mfano mkulima ana mchungwa wake mmoja, machungwa yanazaa kwa mwaka Mara moja, na ni ndani ya mwezi mmoja tu! Unanidai kitambulisho cha mwaka! Hapa ilitakiwa uwekwe utaratibu mzuri utakaomfaidi kila mmoja! Hamna wa kuijibu hii hoja

7: Upendeleo kwenye vyombo vya habari, sio kwamba vyombo vya habari vinashindwa kuriport habari ya upinzani ni kwa sababu vinatishwa sana vinaogopa,Hamna Uhuru tena

8: Kama kweli CCM inajiamini imefanya makubwa kwenye nchi hii , mbona inatumia nguvu nyingi sana mpaka na tunatishiwa hadharani, mimi naona CCM inapita kuburudisha tu (fiesta) wala sio kampeni,wananchi tunataka Sera sio wakata viuno majukwaani

9: Kiukweli wananchi wana hali mbaya mtaani,hela Hamna, vyitu vimepanda bei! Hamna nyongeza ya mshahara, ajira Hamna , alafu tunafarijiwa na ndege! Kura Yangu siwezi kuwapa CCM!

Tundu Lissu karibu ikulu ututee, maana hawa walio madarakani hata sheria ambazo wamejitungia wenyewe hawajui kuzifuata, inashangaza sana, mpaka Mkurugezi wa uchaguzi kitabu chake cha maadili ya uchaguzi hajawahi kukisoma!! Anatoa tu matamko wakishirikiana na mlinda mlango wa CCM( Polepole), Tundu una kazi, kweli unaacha kutoa Sera unaanza kuwapa NEC semina? Wewe ulitakiwa uwe mwanasheria wa nchi hii, maana hata aliyeko sijui ana kazi gani? Ni kuchukua kodi zetu tu!, kabla hujaenda Dodoma wakulipe posho ya Semina ya Jana!.

Wananchi tumuunge Mkono, Tundu Lissu, ndiye mzalendo wa kweli wengine wote ni wanafiki, nje wana maneno laini lakini mioyoni mwao ni umbwa mwitu!! Wananchi tunapenda Maendeleo lakini hatutaki kupelekeshwa kisa tu unatupa Maendeleo, tunahitaji kuwa na Amani, kuwa huru sio kila mara tunaona Ndugu zetu wanatekwa, wanauawawa , wanapigwa risasi, na hatuoni hatua yoyote ikichukuliwa kisa ni wapinzani, alafu Mtu mmoja anasema tumenunua ndege, tumejenga reli, tumejenga hospitali nk, je! Hivyo ni bora kuliko utu?

Hivyo ni bora kuliko damu ya mawazo, Azory, sanane, tundulissu, na wengine? Awamu ya tano hebu jipambanue vizuri! Msione watu wanafuata Tundu Lissu bila wakata viuno, yale ndiyo mapenzi yenyewe kwa mtu anayekubalika!! Leo ninaishia hapo!

Lakini ukweli ndo huo kura Yangu, familia Yangu ipo kwa mheshimiwa lissu!!!
 
Mnajishaua humu JF tu. Wakati hata wake zenu watampigia JPM the end of the day. Jiandaeni kisaikolojia
 
Lissu hana hoja, ni kubabwaja tu uko, af mnadanganya watu kuwa kajaza kumbe hamna kitu, mnatumia picha za zaman, kama CHADEMA Wameshindwa kujiendeleza na hella zao za Ruzuku hawajui zinaenda wapi watawezaje kuendeleza nchi sasa
 
Lissu hana hoja, ni kubabwaja tu uko, af mnadanganya watu kuwa kajaza kumbe hamna kitu, mnatumia picha za zaman, kama CHADEMA Wameshindwa kujiendeleza na hella zao za Ruzuku hawajui zinaenda wapi watawezaje kuendeleza nchi sasa
Haya nenda kachukue mgao wako wa T-shirt na kofia uwahi kwenye lorry kabla halijaondoka kuelekea uwanjani kusomba watu.
 
Nakukumbusha,kura yako ni moja tu,endeleeni kualikana muwe wengi,msiwasahau na wake zenu maana hao ndo watampekeka Magufuli madarakani😂
 
Lissu hana hoja, ni kubabwaja tu uko, af mnadanganya watu kuwa kajaza kumbe hamna kitu, mnatumia picha za zaman, kama CHADEMA Wameshindwa kujiendeleza na hella zao za Ruzuku hawajui zinaenda wapi watawezaje kuendeleza nchi sasa
duh ila kanda ya Ziwa ilikuwa balaah...sikutegemea wananchi wamchukie JPM kiasi kile
 
Mimi nimeamua kuipigia sisiemu....
lakini nikifika kwenye sanduku la kura nita pose kidogo nitajiuliza kisha nitapiga kwa chadema....
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom