Nimeachiwa mtoto ndani ya basi

Nimeachiwa mtoto ndani ya basi

Nawashukuru sana wakuu kwa kunipa moyo, mmenitia nguvu sana.
 
Utata sana...lakini kama ana miaka miwili si anaweza kuongea? - Anajijua jina lake? Ukimsikiliza kwa makini unaweza ukajua/kumuelewa akiongea. Au tafuta mtu mwenye mtoto wa umri huo akusaidie kumsikiliza! Unaweza pata some tips kumuhusu.

Ana afya njem kabisa? Lakini ni muhimu akapimwa vipimo vyote muhimu ili kujua afya yake kwa ujumla
 
Hongera kwa kupata mtoto. Fanya taratibu za kumuasili huyo mtoto.
 
Nilikuja dar kikazi kwa takribani siku 4, sasa jana nikawa narudi mkoani kwangu. Wkt nipo Ubungo nimekaa kwenye dar express akaja mama mmoja mtu mzima mweupe amebeba mtoto, akaketi pembeni yangu, nikamsalimia nikapiga kimya.


Akaniomba nimbebee mtoto akajisaidie, nikakubali. Muda ukawa unazidi kwenda yule mama harudi! hadi basi linajaa hajarudi, mara kakaja kadem kamoja kakaketi kwenye ile siti ya yule mama nikapigwa na butwaa! nikamueleza kwamba ile siti ina mtu, akanionyesha tiketi yake ikabidi nimuamini kwamba kweli ile ni siti yake

Wkt basi linataka kuondoka ikabidi nimpe taarifa konda, tukashuka na konda na baadhi ya abiria hadi kituo kdg cha polisi ubungo, polisi hawakuniamini sana, wakadhani nafanya usanii nilipotaka kumuacha pale mtoto, ikabidi nipige copy vitambulisho vyangu na niache mawasiliano yangu niondoke na mtoto.

Wamama ndani ya basi wakawa wanapokezana kukabeba na kukalisha, ni katoto ka kiume, ka-handsome, baba, mama na girlfriend wangu nao hawaniamini, wanadhani ni mwanangu! Dah!

Makubwa, ukiona wanakusumbua huko nyumbani kwenu tuwasiliane nije kukachukua nilee mwenzenu. Nahis mambo ya kukandamizwa na kuzaa siwezi tena.
 
Mlee tu huwez jua huko mbele yatatokea nin
 
Hahahahhahaha lol.....wotewote hunipi ati...ila akikataa kula niite nije kumuimbia😉😉😉😉

Umeona riziki hiyooo !! MashaAllah TZ bhanaa ina neema nyingi za ajabu kulikoni !!! ( Madini, Mazao, gesi, hifadhi ,hata watoto unapewa bila uchungu,nk ) Mungu mwema na atusamehe sana huyo mama ana roho ya jiweeee?
 
Mkuu fuata taratibu kabisa za kupata uhalali wa kuishi na huyo mtoto. Kwanza kabisa ungepata barua ya utambulisho toka kwa mkuu wa kituo ubungo akieleza kuwa umeachiwa mtoto hivyo ukifika unakoishi unatakiwa kwenda kuripoti polisi ili uende ustawi wa jamii wa wilaya yako ili upata maelekezo ya kuishi na huyo mtoto. Usije ukabugi stepu tu ukawa katika kundi la wahalifu wa biashara ya binadamu.
 
Umeona riziki hiyooo !! MashaAllah TZ bhanaa ina neema nyingi za ajabu kulikoni !!! ( Madini, Mazao, gesi, hifadhi ,hata watoto unapewa bila uchungu,nk ) Mungu mwema na atusamehe sana huyo mama ana roho ya jiweeee?

Ungemuona huyo mama mwenyewe usingeamini mkuu, ana sura ya upole kama malaika.
 
Back
Top Bottom