Nimeachiwa mtoto ndani ya basi

Nimeachiwa mtoto ndani ya basi

Haiwezekani mama amlee mtoto kwa miaka 2 then amtelekeze kirahisi namna hii. Kuna bond kubwa sana inaundwa kati ya mama na mtoto kwa muda wote huo. Kama ni gharama huyo so called mother tayari amemaliza, umri huo mtoto anakunywa uji tu. Kunakasoro sehemu.
Watoto huwa wanatupwa wakizaliwa tu.
 
Fuata utaratibu kisheria umlee kuliko kukaa tu kwani ikitokea mtu ajitokeze na kusema ameibiwa mtoto utahusika ktk kusumbuka mara polis na mahakaman ndo zitakuwa starehe zako.
 
Kuna wamama/wazazi wengine akili zao wanazijua wenyewe.Pengine kweli maisha yamembana na unaweza kuta hana mahali pa kuishi.Cha msingi ni huyu Bwana kufuata utaratibu tu.Aende ustawi wa jamii na kujitambulisha rasmi.Hakuna ugumu wowote katika swala hili wala msimtishe sana.
 
Asante mkuu, sikajui hata jina, sijui nikape jina lingine?
miaka 2 haongei? kama haongei mpe jina tu kulingana na dini yako. Vipi hasumbui kumlilia mama yake? pole jamani yaani naumia sana kwa ajili ya huyo mtoto.
Invisible na paw, hatuwezi kuanzisha mchango kwa ajili ya kumsaport Amicus Curiae japo kidogo kutoa ni moyo
 
hongera mkuu.....polisi hawana msaada wowote pale jambo kama hilo linatokea ilishawahi nitokea nikaenda polisi wakachukua maelezo kilichofuata nikapewa mtoto maana wao hawana mahali pa kuweza kuwatunza nilikaa na mtoto baada ya mwezi mmoja nilipata simu kutoka kituo cha police wakitaka niende na mtoto nilikwenda nikamkuta baba alikwisha toa maelezo na alikuwa na picha ya mtoto sijui police walivyofanya upelezi wao nikamkabidhi yule mtoto kwa yule baba inasemekana mama na baba waligomba miezi kadha iliyopita mama akaamua kuondoka na mtoto sasa haiieleweki ilikuwaje hadi kumtelekeza labda alishindwa malezi....baada ya kukabidhiana nilikwenda kufahamu kwa yule baba nakawa namtembelea mara kwa mara kwa sasa yupo darasa 6
Real BlackWoman and that's Power of kindness.... wema wako hautopotea. Ubarikiwe mema.
 
Huyo n zawad kutoka kwa mungu huwez jua mungu kakupangia nini,fanya kwa unyenyekevu and god wil pay u tirelesly
 
watu na bahati zao aisee!
wenzako wanaenda mwananyamala kuhonga mamilioni ili waibiwe mtoto wewe bureeeeee bila kesi bila dhambi umpe nini Mungu wako zaidi ya kumrudishia sifa heshima na utukufu Amen
 
Nilikuja dar kikazi kwa takribani siku 4, sasa jana nikawa narudi mkoani kwangu. Wkt nipo Ubungo nimekaa kwenye dar express akaja mama mmoja mtu mzima mweupe amebeba mtoto, akaketi pembeni yangu, nikamsalimia nikapiga kimya.

Akaniomba nimbebee mtoto akajisaidie, nikakubali. Muda ukawa unazidi kwenda yule mama harudi! hadi basi linajaa hajarudi, mara kakaja kadem kamoja kakaketi kwenye ile siti ya yule mama nikapigwa na butwaa! nikamueleza kwamba ile siti ina mtu, akanionyesha tiketi yake ikabidi nimuamini kwamba kweli ile ni siti yake

Wkt basi linataka kuondoka ikabidi nimpe taarifa konda, tukashuka na konda na baadhi ya abiria hadi kituo kdg cha polisi ubungo, polisi hawakuniamini sana, wakadhani nafanya usanii nilipotaka kumuacha pale mtoto, ikabidi nipige copy vitambulisho vyangu na niache mawasiliano yangu niondoke na mtoto.

Wamama ndani ya basi wakawa wanapokezana kukabeba na kukalisha, ni katoto ka kiume, ka-handsome, baba, mama na girlfriend wangu nao hawaniamini, wanadhani ni mwanangu! Dah!

Mkuu, pole sana.
 
Nimetokwa na machozi ya furaha! Mlee huyo mtoto.
 
Fuata utaratibu kisheria umlee kuliko kukaa tu kwani ikitokea mtu ajitokeze na kusema ameibiwa mtoto utahusika ktk kusumbuka mara polis na mahakaman ndo zitakuwa starehe zako.

ameshareport police hapo tayari amekwenda hatua moja kuna muda unapewa baada ya huo muda ndio unaweza kufanya utaratibu wa kuadopt
 
Pole nyingi zikiambatana na hongeza kwa kukubali hiyo zawadi ya kuanza mwaka, ila jitahidi apate malezi mazuri kwani mungu atakulipa kwa kazi hiyo.
 
Back
Top Bottom