Mwenye siti ya dirishani ndani ya basi ana haki zipi?

Farolito

JF-Expert Member
Sep 10, 2018
11,634
26,373
Wakuu,

Unaweza kuona kama swali dogo hivi ila ni la msingi sana,kama hujakutana na mgogoro wake basi kuna siku utakukumba tu

Siku kadhaa zilizopita nilipanda basi kwenda mahali fulani,kilichofanya niulize swali ni tukio hili;

Upande wa kushoto dirishani alikaa Mdada umri wa kati tu(25-30).Mimi nilikaa siti ya za upande wa kulia lakini ni kama tulikuwa usawa mmoja tu.

Gari ilianza kuondoka bila shida,tatizo lilianza baada kama ya saa mmoja hivi spidi ikiwa kali ndipo yule dada akafungua dirisha lake ili hewa iingie kwa ajili yake,sasa mara baada ya kufungua haikupita hata dakika moja zikaanza kelele kutoka nyuma yake(siti za nyuma yake na zingine za upande wangu) zikimtaka afunge kioo, alisikia lakini hakufunga,baada ya muda mfupi mmoja wa wanaume waliokuwa siti ya nyuma akafunga kile kioo, Yule Dada akafungua tena,hapo akaambiwa "wewe dada funga hilo dirisha upepo ni mkali sana kuna watoto huku nyuma" yule dada akajibu hata mimi najisikia vibaya nahitaji hewa iingie.

Mzee mmoja wa siti ya nyuma akalifunga lile dirisha kwa nguvu aliporudisha tu mkono dada akafungua tena,mzee akafunga dada akafungua tena huku wale waliokuwa wakilalamika nyuma wakishuhudia,hapo ikainuka vita Kali balaa kelele za nyuma zikazidi kumshambulia yule dada"huyu dada hana adabu kabisa tunawambia haelewi,kuna watu wana watoto wa miezi sita huku nyuma upepo mkali sana,yule dada akajibu namimi najisikia vibaya kwahio nifanyeje?

Kelele zilipozidi akaja konda wa kwanza"Dada funga hilo dirisha huwezi kusumbua watu wote hawa mtu mmoja"alikuwa anaongea huku anafunga hilo dirisha, (kwa maoni yangu huyu konda alikosa busara)dada akamjibu mimi najisikia vibaya nahitaji hewa ndio maana nimefungua,alipoondoka Konda kuelekea nyuma yule dada akafungua tena dirisha.

Yule konda aliporudi kutoka nyuma akakuta dirisha limefunguliwa tena"we dada naona ni mkorofi tutakushusha"dada akamjibu sawa nishusheni ila mnirudishie nauli yangu yote.

Kelele za kumtaka afunge dirisha hazikwisha, huku wale kinamama wenye vichanga wakimshambulia"wewe hujawahi kuzaa ndio maana huna huruma, huyu hana mtoto ndio maana mjeuri"yule dada akajibu nimeshazaa ila namimi nina matatizo ndio maana nimefungua dirisha.

Kelele zilipozidi akaja konda mwingine (kwa maoni yangu huyu ana busara) akawambia dada ukifungua dirisha lako upepo unawaathiri zaidi walionyuma yako kwahio kama unashida ya hewa naomba nikuhamishie siti nyingine ambayo utaweza kufungua,kule nyuma kuna vichanga"

Siku sikia alijibu nini ila nadhani dada aligoma pia kuhamishwa yule konda akamwacha akaondoka zake.

Basi zoezi la mzee wa siti ya nyuma kufunga na dada kufungua likaendelea baadae mzee akachoka ikabidi aache tu ila lawama za wale kinamama zinaendelea pamoja na wale wanaume wa nyuma(hawa wote lilikuwa lile kabila fulani kubwa kanda ya ziwa) basi wakawa wanasapotiana na kumshutumu yule dada kwa maneno mbalimbali baadae kukawa kimya huku dirisha likiwa wazi mpak mimi niliposhuka kituo fulani nadhani na yule dada alishuka pia pale.

Sasa nauliza wadau,hivi haki za mtu mwenye siti za dirishani ni zipi?Je huyo dada alikuwa sahihi au alikosea?Je ni mhudumu ndio anapaswa kufungua ili kuepusha migigoro kama hii?

Karibu.
 
Wakuu,

Unaweza kuona kama swali dogo hivi ila ni la msingi sana,kama hujakutana na mgogoro wake basi kuna siku utakukumba tu

Siku kadhaa zilizopita nilipanda basi kwenda mahali fulani,kilichofanya niulize swali ni tukio hil...
Siku nyingine panda basi zenye A/C😄😄😄😄

Anyways ukifungua kioo upepo haukupati we uliyekaa firishani ila wa nyuma yako ndio wanaumia, hata kwenye manyunyu ni hivyohivyo.
 
Huyo dada busara atakuwa katoka Lile kabisa la wababe Tena single mama ilitakiwa arejeshewe nauli yake.

Alichofanya ni kiburi na dharau tu sababu ya malezi mabovu na Sio afya thus aligoma kuhama siti.

Ukimstudy lazima atakuwa na element za uchawi.

Huyo ni kukata Kofi moja akili ikae sawa
 
Kuna siku bwana natoka zangu dom nikadaka usafiri pale four ways zile Bus za saa nne ,nikakaa na dada mmoja product ya Meatu😂

Yule dada kila muda namwambia fungua dirisha hewa ni nzito humu, anafungua,nikilala anafunga tena,Msukuma yule alinichosha nikahama seat
 
Huyo dada busara atakuwa katoka Lile kabisa la wababe Tena single mama ilitakiwa arejeshewe nauli yake.
Alichofanya ni kiburi na dharau tu sababu ya malezi mabovu na Sio afya thus aligoma kuhama si...
Umkate kofi awamu ya Rais Samia 😂 ,Mkuu usidhani hao waliomuacha ni mafala,kupiga mtu hasa mwanamke ni kesi kubwa
 
Ipo hivi ndugu Mtanzania.

(Msafiri kafiri) abilia aliyekata upande wa dirishani hana mamlaka na dirisha ila ana mamlaka na 💺 aliyokalia pamoja na kufungua kufanya anachotaka pasipo kukushirikisha wewe wa pembeni.

Ila ikitokea ukawa na matumizi ya dirisha sababu yupo eneo linalomuhusu, unaweza kumshirikisha sababu ya kero unazoweza kumpa huyo wa upande wa dirishani.

Hakupaswa kufanya huo utoto alioufanya, binafsi huwa supendi kukaa upande wa dirishani but first of all abilia anayekuja nampa sharti la dirisha.

Huyo binti hajakutana na wababe wewe, asee humo kwenye basi siku hiyo wote mlikuwa wenye wokovu mnamsubiri bwana kwa kuepuka 'z'ambi 😄!.
 
Issue kama hii haipaswi kutafuta mshindi, inahitajika busara tu kuweza kumaliza mzozo.

Kitendo cha huyo dada kukaidi kuhamia siti nyingine kama alivyoelekezwa na konda wa pili ni dalili ya ukorofi,malezi mabovu na ubinafsi.
 
Dada ana haki zake 😀😀😀sema angefungua kidogo tu kupunguza athari ya upepo kwa wengine..
Kuna watu tuna hizo shida kwenye mabasi aseeh tena jirani ukipiga kelele sana unaweza tapikiwa hadi basi😂😂😂😂😂
Kuna muda hata ac unaona haisaidii, unahitaji hewa safii ya huko njeee👍
 
Back
Top Bottom