Ulishawahi jutia kukosa namba ya mtoto mzuri ambae amekuvutia kwenye safari ndefu za mabasi?

Mtu Mbadi

Member
Feb 28, 2024
95
100
Binafsi mimi ilikuwa 2022 hiyo natoka zangu Dodoma kuelekea Kibondo Kigoma, basi apo mjini Dodoma nikapanda SATCO inayoelekea Bukoba ili nikashukie Nyakanazi theni niunge na Casablanca (Wenyeji wa hii mitaa wanazijua hizi basi moto wake) mpaka Kibondo.

Sasa picha linaanza kweny siti nilipata nikajikuta na Maza wa kihaya umri umeenda haswa nikasema hapa leo mpaka nifike ninapoenda sijui kama nitaongea na huyu mama, basi safari ikaendelea.

Sasa siti ya pemben yetu bana alikaa chalii flan na mtoto flani mkali kinoma, kijana wenu macho yangu yalitokea kuvutiwa nae haswa nikawa nawaza hapa lazima nichukue namba za huyu mtoto mzuri, siwezi kuwa mzembe kabsa,.. sasa ishu ikawa ninawaza niombe badirishana siti na yule chalii ahamie kwangu ili mimi nihamie pake? nikasema hapana manzi ataniona kama namshobokea.

Basi huku safari inaendelea nakumbuka wakati tumekaribia Singida yule manzi simu yake ilikuwa inakarbia zima chaji na alikuwa hana chaja akaniomba maana aliona muda nachaji simu yangu, basi nikampatia lakin system chaji ya pale alipokaa ikawa inazngua ikabidi aniombe nimchajishie pale kwangu, basi nikaipokea simu yake nikawa namchajishia pale kwangu.

Safari ikawa inaendelea huku nasema yaan hapa leo nisipopata namba za huyu mtoto mzuri ntakuwa mzembe sana, mind you huyu maza alikuwa hata halali njia nzima ili nipate hata upenyo wa kumuomba namba yule mtoto.

Basi safari ikaendelea mpaka simu ya yule mtoto ikajaa maana ilikuwa nazani betri linashida maana ilijaa kabla hata hatujafika kahama, nikampatia akashukuru pale na katabasamu ka uongo na kweli.

Kumbuka njian kuna sehemu tulikuwa tunashuka kula mahotelin lakini sasa yule maza sababu alikuwa amekaa pale karibu na yule manzi wakawa wakishuka wanaenda wote kununua misosi pamoja (Hii ilinikera sana nikaona huyu maza mbona kama ananibania rizki kijana wenu) yaani wakawa wanakuwa pamoja sababu walijuana wote wanaelekea sehem moja japo hawafahamian.

Sasa basi tukafika Nyakanazi ambapo mimi nilikuwa nashukia wakati nashuka yule maza ndo anaanza niongelesha mwanangu kumbe unashukia hapa, mimi ndio mama, yeye safari njema kwani unaenda wapi nikamjibu Kigoma huko yeye sawa safari njema, mimi sasa muda huo ananiongelesha naona kama anazidi kunichawia nikose nafasi ya kuchukua namba ya huyu binti, nikamuaga yule manzi kiaina nikashuka.

Basi kijana wenu nikasema daah ndo nishakosa namba hivo, nikashuka mpaka chini sasa kwa bahati nzuri yule manzi alikuwa dirishan upande nilioshukia akawa ananipungia mkono na kuniongelesha ikabidi nisogee kumsikiliza ananitakia safari njema nikasema hapa hapa ndo pakuchukua namba, nikamjbu pale nikamuuliza wewe huko unakoenda ndo home akasema ndio anaenda mara moja lakin atarudi chuo (Alikuwa anasoma Udom), basi nikamwambia naomba namba zako ukirudi Dom tuwe marafiki mtoto akanipa namba pale moyo wangu ukawa na amani kama yote, kufupisha stori yule manzi baada ya kurudi zangu Dom nikaanza mpanga mtoto akatiki nikawa najilia mbususu tamu kabisa ya kihaya mpaka pale tulipokuja kuachana sababu ya vimizinga vya hovyo kuzidi.

Vipi wewe mkuu una experience gani na hizi safari za Kweny mabasi na watoto wa kike?
 
Balaa na tatizo linaanzia kwenye "ya kihaya"
Kijana unapajua temeke kwa Wahaya wewe??
Kijana unapafahamu Mwananyamala kwa Wahaya wewee??
Anyway, ngoja nile kitu kali kwanza...... 🚭
 
Balaa na tatizo linaanzia kwenye "ya kihaya"
Kijana unapajua temeke kwa Wahaya wewe??
Kijana unapafahamu Mwananyamala kwa Wahaya wewee??
Anyway, ngoja nile kitu kali kwanza......
Kaka nilicheza game zote na soksi, siwezi muamin mtu ambae nimempata kweny mazingira hayo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom