Nimeachiwa mtoto ndani ya basi

Nimeachiwa mtoto ndani ya basi

Inasisimua na kutia huruma kwa mtoto ambaye ametelekezwa mikononi mwako... Nakushauri kaka mlee kama vile wakwako hadi hapo mama au ndugu wa mtoto watakapojitokeza ila nakusihi jitahidi kumfanyia ibada kupata kibali mbele za Mungu. Hatuwezi jua ametokea wapi.... Wengi wamesema ni baraka umeletewa, lakini pia kuna wakina Zinduna.

Mungu akubariki kwa moyo wa upendo ulio nao.

Tuzidi kuombeana kheri mkuu!
 
Imewahi kunitokea dar. Ni njia nzuri zaidi kuliko kuwatupa chooni ama kuwatelekeza majalalani. Ila kwa kufanya hivyo mi siku hizi simsaidii mwanamke yeyote kubeba mtoto. Mi nilitelekezewa kwenye daladala. Niliteseka sana na mtoto huyo

Kwahyo ulifanyaje?au ulimpata mama yake?
 
Aisee! Inamana huyo mtoto hana baba? Ndugu wengine n.k? Naamini kwa kupitia uzi huu usishangae kujitokeza ndugu wa huyo mtoto!!
 
aisee pole sana....na hongera kwa moyo wako!
fanya mpango umuasili kabisa huyo mtoto ikiwa wewe na mchumbako mtakubaliana (nadhani itakuwa mkishaoana, si ndo iko ivo wakuu)
 
Nimekaacha kwa wazazi wangu, nakatafutia dada wa kukalea(yaya), mama amesisitiza kakae nyumbani umri wake usogee kwanza ndio kahamie kwangu

Unabahati kubwa sana mkuu! Mark my words. Embu fikiria kati ya watu woote na possibilities zooote ikakudondokea ww! Ur very lucky. Ningempenda sana huyo kiumbe. sana na nakushauri nawe iwe hivyo hivyo!
 
dah, pole sana. ila bora kakuachia wewe kuliko angetoa mimba au angemtupa dampo. hapo ana uhakika mtoto atalelewa atamtafuta ukubwani.
 
Nilikuja dar kikazi kwa takribani siku 4, sasa jana nikawa narudi mkoani kwangu. Wkt nipo Ubungo nimekaa kwenye dar express akaja mama mmoja mtu mzima mweupe amebeba mtoto, akaketi pembeni yangu, nikamsalimia nikapiga kimya.


Akaniomba nimbebee mtoto akajisaidie, nikakubali. Muda ukawa unazidi kwenda yule mama harudi! hadi basi linajaa hajarudi, mara kakaja kadem kamoja kakaketi kwenye ile siti ya yule mama nikapigwa na butwaa! nikamueleza kwamba ile siti ina mtu, akanionyesha tiketi yake ikabidi nimuamini kwamba kweli ile ni siti yake

Wkt basi linataka kuondoka ikabidi nimpe taarifa konda, tukashuka na konda na baadhi ya abiria hadi kituo kdg cha polisi ubungo, polisi hawakuniamini sana, wakadhani nafanya usanii nilipotaka kumuacha pale mtoto, ikabidi nipige copy vitambulisho vyangu na niache mawasiliano yangu niondoke na mtoto.

Wamama ndani ya basi wakawa wanapokezana kukabeba na kukalisha, ni katoto ka kiume, ka-handsome, baba, mama na girlfriend wangu nao hawaniamini, wanadhani ni mwanangu! Dah!

inawezekana kabisa malipo yakawa ni hapa hapa duniani,hebu kumbuka katika pita pita zako hujawahi kususa mimba?hujawahi kusema hautambui ujauzito ni wako?kama hujawahi kususa mimba then heri ya mwaka mpya
 
hiyo baraka mtu wangu, ila hakikisha unakamilisha taratibu zote za kumuadopt maana hii serikali hata haielewekagi aisee. Kuandikisha polisi tu bado utaratibu wa kisheria wa kumuadopt mtoto haujakamilika, malizia maana hii inaonekana baraka lakini usipoihalalisha kuwa baraka safi inaweza kukutia matatizoni akijitokeza mtu na madai yake. Si unajua watu wanachungulia fursa siku hizi?
 
aisee pole sana....na hongera kwa moyo wako!
fanya mpango umuasili kabisa huyo mtoto ikiwa wewe na mchumbako mtakubaliana (nadhani itakuwa mkishaoana, si ndo iko ivo wakuu)

Paloma i love this boy like my own, he's handsome and cool, nimeuchukua ushauri wako.
 
Cute-Black-Babies_large.jpg
 
Back
Top Bottom