Nilikuja dar kikazi kwa takribani siku 4, sasa jana nikawa narudi mkoani kwangu. Wkt nipo Ubungo nimekaa kwenye dar express akaja mama mmoja mtu mzima mweupe amebeba mtoto, akaketi pembeni yangu, nikamsalimia nikapiga kimya.
Akaniomba nimbebee mtoto akajisaidie, nikakubali. Muda ukawa unazidi kwenda yule mama harudi! hadi basi linajaa hajarudi, mara kakaja kadem kamoja kakaketi kwenye ile siti ya yule mama nikapigwa na butwaa! nikamueleza kwamba ile siti ina mtu, akanionyesha tiketi yake ikabidi nimuamini kwamba kweli ile ni siti yake
Wkt basi linataka kuondoka ikabidi nimpe taarifa konda, tukashuka na konda na baadhi ya abiria hadi kituo kdg cha polisi ubungo, polisi hawakuniamini sana, wakadhani nafanya usanii nilipotaka kumuacha pale mtoto, ikabidi nipige copy vitambulisho vyangu na niache mawasiliano yangu niondoke na mtoto.
Wamama ndani ya basi wakawa wanapokezana kukabeba na kukalisha, ni katoto ka kiume, ka-handsome, baba, mama na girlfriend wangu nao hawaniamini, wanadhani ni mwanangu! Dah!