Nimeacha nyumba yangu kwasababu ya ndugu

Nimeacha nyumba yangu kwasababu ya ndugu

Vimefanya hivo kwa makubaliano na mwana mke au vimembaka tu?........kama kwa makubaliano mwenye tatizo ni mke, kua nalaya sio vijana.
Shida inaonekana ni mwanamke ndo alikuaga anavipa k maana mume wake kutwa yuko bize mpka saa 5 usiku na vijamaa vinashinda nyumbani muda wote ila mke alishagafukuzwa siku nyingi
 
Mbona wakati wana changia ada zako uende shule hukulalamika, acha ubinafsi wa kijinga heshimu ndugu zako. Nyie mkipata vipesa kdgo kupita ndugu zenu mnaona ndugu ni washenzi sijui nyie watu wa mikoani mko je buana.
Lakini piah huwezi jua
Kwa asilimia kubwa unapokuwa kwenye safari ya mafanikio wasindikizaji huwa ni wachache lakini wapongezaji ni wengi
 
Mkuu inamaana kwa wakati huo atakua Hana watoto? Kwa mfano wewe una mke na watoto 5 mtoto wa kwa ana miaka 24 wa mwisho 14 ukipata ugonjwa mke na watoto wako watakukimbia kwenda wapi ?
Si mpaka uwe nao hao watoto wa umri huo mzee
 
Omba mungu akupe afya njema vinginevyoo pale muhimbili utajuta kutengana na ndugu

Marafiki watachoka

Mke atachoka

Vimada vitasepa na ngia namba tano

Walevi wenzio watakuona binchwa komwe......

Ndugu ni sehemu ya roho yako hata Mungu analijua hili heshimu ndugu kadri uwezavyo pesa zako hata usipo wapa wataishi mkuu usijidanganye fala wew......
Kwakuwa kuna kuumwa ndo ubebe mzigo unaokuzidi uwezo?
Undugu ni kusaidiana na kuna nyakati kweli unaangalia kuwa huyu mtu anahitaji kusaidiwa,,, ila kuna zingine ni kuleana kindezi..
Na ndugu wa dizaini hii wa kukutegemea kila kitu from A to Z usitegemee kuwa watakusaidia ikifika kwenye 18 yako, hawa wengi ni wapenda raha ndo maana wameshindwa hata kujiongeza kutafuta hata nusu ya suluhu ya matatizo yao..
 
Nieipehii!
Ndugu anatakiwa aje na plan baada ya siku tatu tunajadiliana vizuri mipango yake ni nn Kisha nampa fact kuwa kazi ndio kipaumbele mda wa kula na kugalagala Amna ikiwezekana na chumba anayolala anaweza toa pesa kidogo , ghalama za chakula na mengineyo.

Hizi mambo nazielewa nakumbuka miaka hiyo nyumbani walikuwa wanakuja watu hadi wanafikia 18 ukicheki matumizi hadi sio poa kilo 5 za Mchele na unga zinakata mlo mmoja alafu watu wapo tu wao ni kuoga na kujipaka mafuta na kuulizia tunapika nn .
Nimependa hii
 
Ki ukweli watu wa D'salaam mtalaumiwa bure kuwa sio wakarimu lakini ukweli lazima usemwe. Dar kama huna shughuli maalumu ya kufanya unakuwa mzigo kwa ndugu maana kila kitu ni kununua. Kuanzia chakula, maji, umeme mapaka takataka unazilipia kwenda dampo.

Kijijini hakuna hizo gharama ndio maana tunaonekana wakarimu kwa jamaa zetu wa Dar. Kongole mkuu
 
Ungeishi kama mzungu, kabla ya mgeni kuja atoe taarifa na atakaa mda gani. Mimi siangalii makunyanzi, nawaambia naishi kwa budget.
 
Hivi viumbe vinavoitwa ndugu ni wapumbavu washenzi ndugu wote ni nyoko.

Nimepangisha nyumba yangu yenye vyumba 3, sitting room na jiko nimekuja kupanga chumba na sebule. Maamuzi haya nimeyafanya baada ya nyumba kujaa ndugu hadi nikawa sina amani na nyumba yangu. Ndugu wanakuja kukaa miezi alaf hawachangii chochote wananitegemea mie kwa kila kitu hadi nepi za watoto wao kama mie ndo niliwazaa.

Nikaona isiwe shida nimetafuta sehem nimepanga kachumba kamoja na kasebule kadogo niwakomoe. Kwa maisha ya sasa unaendaje kwa mtu unakaa miezi huna shughuli za kufanya?

Ninewakomoa toka nihamie huku hakuna ndugu anayenipigia simu hata kuniuliza hali yangu asa sijui wamenifuta undugu [emoji23][emoji23] anyways bora wasinitafute maisha bila ya ndugu ni matam sana kwa wiki hizi 3 naona kama vile nipo peponi.

Najipongeza kwa uamuzi niliochukua lakin pia najilaumu kwa kuchelewa kuchukua uamuzi huu.
Ukifa hao hao ndo watakao kuzika na kulia juu ya kaburi lako. Watch out!!!
 
Nimesomeshwa na wajomba. Wajomba hawanisumbui kwa lolote wapo na maisha yao na wala hawalalamiki. Njoo sasa upande wa kwa baba, walitutelekeza mzee alipofariki hawakutujua kwa heri wala kwa shari leo Mungu ameonesha njia kila siku simu kila siku ugeni usioisha wakiwa na matatizo kiafya wanakuja niwauguze, wao hawanunui hata panadol. Kumbuka hawa ni watu ambao hawakutujali kwa lolote ukiwapigia simu walikua wanatoa ahadi ukipiga tena simu siku aliyoahidi hawapokei simu!
Asee kumbe
 
Vijana wengi hawajui namna ya kuishi vizuri ugenini

Ukiishi Kwa watu (ugenini) hakikisha unawahi kuamka na kusaidia kazi za nyumbani mathalani Usafi wa Uwanja/ kunyeshea Maua/ kusaidia kazi za Jikoni n.k

Enzi za utoto wangu nimewahi kuishi Kwa ndugu miezi 2 hivi ama 3, lakini sikuwahi kuchokwa kwasababu nilikuwa najituma kufanya kazi hadi zile wanaita kazi za Kike nilifanya ikiwemo kudeki nyumba/kufagia uwanja kukatia mifugo nyasi n.k

Inapofikia Likizo imeisha ya kurudi Shule, ilikuwa hadi mwenyeji wangu hatamani niondoke maana alikuwa anaona nilivyokuwa nikimsaidia kazi za pale nyumbani
Nikipata wageni wa hivi walah nafurahi ...kwa kuwa hata mm nilikaa kwenye nyumba za watu nilijituma haswaa..ila kuna vile vichefu chefu aisee akiamka sa tatu anakunywa chai baada ya hapo ni TV hadi jioni hasaidii kasi yoyote..basi nakereka pyeee
 
Sio kwa Mbowe kuna mshua mmoja anaishi na kijiji kabisaa na anajivunia huwa anasema yeye hakupata nafasi ya kushikwa mkono ila hilo halimfanyi kuacha kushika wengine mkono kwa nafasi aliyonayo
Kama kwangu tu ila wageni wanaraha zao sometimes nyumba inachangamka na nilichonotice huwa wanakuja na baraka zao hatujawah kukosa kabisa riziki zinapunguka tu badae tunakuwa sawa
 
Mbona wakati wana changia ada zako uende shule hukulalamika, acha ubinafsi wa kijinga heshimu ndugu zako. Nyie mkipata vipesa kdgo kupita ndugu zenu mnaona ndugu ni washenzi sijui nyie watu wa mikoani mko je buana.
Wewe una uhakika gani mkuu kama ndugu zake ndio wamemchangia ada!?
Je kama alipambaniwa na wazazi wake peke yake??
 
Nimekuelewa, kiukweli ukiwa na wageni unakosa uhuru flani na nyumba yako, ila unazungumziaje watu ambao wanajiweza kiuchumi, Wana biashara kibao, wanaishi kwenye ghorofa, vyumba vya wageni vipo, ila hawataki ndugu hata mmoja awatembelee, hata wale ndugu ambao hawana stress, wa kuja kukaa wiki 2 kwa dharura/ au kusalimia na kuondoka, hawawataki 😁 Evelyn Salt
Hiyo ni zaidi ya roho mbaya na uchoyo..hivi unajiskiaje mtu akafanikiwa akiwa katokea kwako?utajiskiaje maisha yakienda kombo na mtoa msaada ni mtu ambae ulimkataa kukaa nae?basi tu ni vile watu hawajui wageni wanakero zao ila wanabaraka zao nyingi tu..ukiwa na chance ya kusaidia saidia unapoweza mtu afike malengo..
 
Back
Top Bottom