Nimetofautiana na jirani yangu, naombeni ushauri

Ugumu unauleta wewe Mkuu
Ati miti iniozeshee mabati yangu au iifanye nyumba yangu kuwa na nyufa,kisaaa,!!!!Miti ndio inaleta thamani ya kiwanja chake...Aseee!!!kwangu mimi hio ni sawasawa na mende kuangusha kabati
Mimi jirani yangu ana mti mkubwa saaana wa mzambarao siku majani yakianza kudondoka na kunichafulia Ua wangu tu,Fasta kibarua anakweya juu na panga na kukata matawi yoote
Huyo jirani yangu mwenye huo mti alishanitishia polisi mara kuniroga mara aniletee barua ya wito kwa balozi hadi kachemka mwenyewe
Kwasasa kashanizoea
Pole sana stickvibration
 
Ningekuwa mimi na wewe akili zetu tungemnyoosha mbona

Upo sawa kabxaa.Nahisi Nahuja hana machungu na nyumba yake wala na familia yake
Na hizi mvua za sasa Radi za kufkia tu hususan ktk miti ya mikaratusi na michongoma
Kama ni mimi nisingepunguza matawi ningeng’oa hadi mizizi
Niangamize familia yangu nyumba yangu kisaaa,!!!

To hell,!!!!
 
Mjumbe/balozi ni shost yake, na ndie kampa kazi ya kuangalia hicho kiwanja mtu asikate mti hapo!!!!
Basi mkuu kama vipi tafuta pesa mvue hicho kiwanja maana naona ndio suluhisho.

Kwasababu hata akiikata akajenga hamtaishi kwa ujirani mwema.

Ila naona kama kutakuwa hamna breakthrough, tafuta hizi herbcides kati ya glyphosate na triclopyr. Fata maelekezo ua miti hiyo, bora miti au uhai wa binadamu?
 
Nilishajiridhisha siku nyingi kuwa hapa JF ni kisima cha faraja na pia kuna maudhi madogo madogo. Nina tatizo na jirani yangu kiasi kwamba nimekosa ufumbuzi hadi nimefikia maamuzi ya kuwaomba ushauri wanaJF.

Ni kwamba kuna jirani yangu ambaye yeye hajajenga bado (ni uwanja/kiwanja) tu. Katika kiwanja chake hicho amepanda miti ya aina ya mikaratusi imekuwa mirefu sana. Miti hiyo amepanda hadi mpakani kabisa na kwangu. Kunapokuwa na mvua na upepo mkali miti inainama hadi inakwaruza bati la nyumba yangu.

Nimemuomba sana akate miti minne ambayo ndio hatarishi lakini yeye majibu yake siku zote ni kwamba, hawezi kukata miti yake kwa kuwa ndio inayokipa kiwanja chake thamani siku akitaka kukiuza. Nilimuliza ni vipi athamini hela kuliko uhai wangu na nyumba yangu akasema kwa hilo nitamsamehe labda akate mti mmoja tu.

Naomba mnisaidie je hili suala nilipeleke kwenye mamlaka ipi ya serikali? Nakiri kuwa negotiation na mediation vimekwama kabisa.

Petro E. Mselewa nisaidie mkuu na wengineo wengi
Baba watoto anasemaje?
 
Ningekuwa ni mm ningeenda kutafuta mashine ya kukatia miti/mbao then nasubir usiku mnene uingie naenda kuikata hyo miti yote na kurejesha mashine kwa mwenye nayo usiku kwa usiku,kesho asbh akniuliza nitamwambia sifaham chochote na nilikuwa safarini na familia yangu (nitamuonyesha na tiketi kama ushahidi)

Aaaaagh! Mahakamani,kwa balozi na kwenye mabaraza ya ardhi au kata ni kupotezeana muda!
Hhhhhhhhhh! Sio kwa maamuzi hayo
 
Ningekuwa ni mm ningeenda kutafuta mashine ya kukatia miti/mbao then nasubir usiku mnene uingie naenda kuikata hyo miti yote na kurejesha mashine kwa mwenye nayo usiku kwa usiku,kesho asbh akniuliza nitamwambia sifaham chochote na nilikuwa safarini na familia yangu (nitamuonyesha na tiketi kama ushahidi)

Aaaaagh! Mahakamani,kwa balozi na kwenye mabaraza ya ardhi au kata ni kupotezeana muda!
Yaani unaamua kuukuza mgogoro!

Vv
 
Back
Top Bottom