Mke wa Jirani yangu ananipa chakula kila apikapo

Yofav

JF-Expert Member
Mar 12, 2021
3,956
6,887
Habari wakuu,

As the head above explains, Imekuwa kama inataka kuwa kawaida tu sasa kila nishindapo nyumbani kuna mke wa jirani yangu ikiwa atapika mchana na kujua kuwa nipo basi ni lazima atanigongea mlango baada ya chakula kuiva.

Me ni bachela ndiyo na huwa sipendelei sana kupika kutokana uvivu na ikitokea nimepika basi nimekaanga mayai au kuchemsha so, mara nyingi nikiwa home nashinda zangu ndani na huwa naorder vyakula restaurant kikifika napigiwa simu tu natoka nachukua na kurudi ndani kula.

Tabia hii ya kupewa chakula na jirani yangu imeanza kunikera kwani huwa nafikiria kwamba kila siku ananipa yeye tu alafu mimi sipikagi wala hivyo sitiweza kumpatia na yeye wakati mwingi kama fidia sasa si nitakuwa kama namnyonya?

Natamani niwe nakataa ila sina njia yenye busara maana kuna siku nilimuambia nimeahakula akaniambia weka tu utakula hata baadae, Je.. nitumie njia gani ya kuwa ninakataa chakula chake bila kumfanya ajisikie vibaya?
 
Mke wa mtu sumu, vijana msijione wajanja. kuna mbaba mmoja tajiri hadi aliweka walinzi kwasababu ya tuvijana hutu, ukiona mke wa mtu anakufuatafuata kimbia, bom litakalotegwa litakupata wewe peke yako, yeye hadhuriki kwasababu mtegaji anajua umuhimu wake kuendelea kulea watoto wake. ndo maana mnalongwa mapema hata ujana hamuuli.
 
Nafikiri wabongo wengi nusu ya ubogo wao umejaa tamaa na fikra za ngono.
Umepewa chakula unaona nongwa, unhenyimwa (angekimwaga) pia ungeona nongwa.
Kama vipisiukatae tu...🤨
wala sio hivyo, huyo mke ni kwamba anataka mechi, ipo wazi. mke asiyetaka icho kitu hawezi hata kugusa mlango wa bachela hovyo. wengi tu tulishalishwa na wake za watu na kuoshewa hadi vyombo na wake za watu ila mapenzi yalipozidi, ilibidi tujisalimishe kwa waume zao tukisingizia mkewe anatusumbua ila hatujamla kume alikua mke wetu. na hapo ndipo mahusiano yaliisha kwa namna alivyokuwa ameganda jamaa alikuwa anakuja kujua muda si mrefu na adhabu yake nisingeweza kustahimili kwa namna nilivyomfahamu yule gaidi.
 
Kama ni bachelor unashinda nyumbani Kwa nini?
Tafuta shughuli ili urudi nyumbani ushakula na usiku Sana

Uwe unarudi Mida ya mumewe ...
Tatizo litaisha
Huwezi ukanipangia kuhusu ratiba zangu kisa kupewa chakula
 
Back
Top Bottom