Nimetofautiana na jirani yangu, naombeni ushauri

Sema kwa kuwa ni jirani yako, kama na yeye atakuwa na mpango wa kujenga hapo ni vyema mkayaongea kabla ya kufika kwenye vyombo vya sheria... maana huenda baadae mmoja wenu akawa msaada kwa mwingine hapo baadae... ujirani mwema
Yeye anakiuza hicho kiwanja hataki kujenga hapo. Kuhusu ujirani ni kweli ni vema kuishi kwa amani, ndio maana nimekuwa nikijishusha sana kwake kumuomba lakini hataki kabisa!!!!! Mwishoe nimeona niombe msaada wa ushauri kwenu wanaJF, nashukuru nimepata mwanga.
 
Ilo eneo usiku si linatishaa,anaanzaje kupanda miti kwenye eneo la makazi ya watu
Changamoto kwakweli,mpeleke mahakamani tu
 
Hiyo ya kukata miti siwezi ni mirefu sana inatakiwa kukatwa kwa ufundi ili isiangukie nyumba. Kuhusu kumtandika makofi sina nguvu za kumpiga ni mwanamme. hahahahah mimi ni mwanamke. Kumlaza selo ni ngumu ni POLISI
Duh kumbe ni Police ndio maan ana dharau!!

Basi fanya kupeleka suala lako kwa mjumbe ili mmalizane kisheria zaidi. Akileta ujuaji nitafute nikupe mwanasheria makini ufungue kesi kotini
 
Yeye anakiuza hicho kiwanja hataki kujenga hapo. Kuhusu ujirani ni kweli ni vema kuishi kwa amani, ndio maana nimekuwa nikijishusha sana kwake kumuomba lakini hataki kabisa!!!!! Mwishoe nimeona niombe msaada wa ushauri kwenu wanaJF, nashukuru nimepata mwanga.
Basi huyo mpige kwa sheria tu.. "Polluter Pay Principle"
 
Yaani huyo kaka ni jeuri sana (mkurya). Ananijibu kwa kiburi eti "hiyo miti ndio thamani ya kiwanja changu, sina mpango wa kujenga hapo, hicho kiwanja kiko sokoni. Labda nikate mti mmoja tu." Kiwanja kizima kimejaa mikaratusi, na kiko katikati ya nyumba za watu!!!!:(:(:(:(:(:(:(:(
Pole sana,pia mikaratusi ( ucalptus if I am not mistaken) huwa inafyonza maji sana refer to land reclamation to different countries!
 
Ugumu unauleta wewe Mkuu
Ati miti iniozeshee mabati yangu au iifanye nyumba yangu kuwa na nyufa,kisaaa,!!!!Miti ndio inaleta thamani ya kiwanja chake...Aseee!!!kwangu mimi hio ni sawasawa na mende kuangusha kabati
Mimi jirani yangu ana mti mkubwa saaana wa mzambarao siku majani yakianza kudondoka na kunichafulia Ua wangu tu,Fasta kibarua anakweya juu na panga na kukata matawi yoote
Huyo jirani yangu mwenye huo mti alishanitishia polisi mara kuniroga mara aniletee barua ya wito kwa balozi hadi kachemka mwenyewe
Kwasasa kashanizoea
 
Duh kumbe ni Police ndio maan ana dharau!!

Basi fanya kupeleka suala lako kwa mjumbe ili mmalizane kisheria zaidi. Akileta ujuaji nitafute nikupe mwanasheria makini ufungue kesi kotini
Mjumbe/balozi ni shost yake, na ndie kampa kazi ya kuangalia hicho kiwanja mtu asikate mti hapo!!!!
 
Yaani huyo kaka ni jeuri sana (mkurya). Ananijibu kwa kiburi eti "hiyo miti ndio thamani ya kiwanja changu, sina mpango wa kujenga hapo, hicho kiwanja kiko sokoni. Labda nikate mti mmoja tu." Kiwanja kizima kimejaa mikaratusi, na kiko katikati ya nyumba za watu!!!!:(:(:(:(:(:(:(:(
Kwani Mkuu,huna mume ambaye atakuwa anajibizana naye huyo Mkurya...watu wa kanda ya ziwa wakiona mahali anaishi mwanamke peke yake huwa wanamdharau sana hata kama atakuwa na mafanikio!
 
Kweli kabisa anza kupeleka malalamiko yako kwa ofisi za Serikali za Mitaa, Diwani, Afisa Mtendaji n.k na baada ya kote huko ikishindikana, Kata MITI hiyo okoa maisha yako na ya familia,halafu kama kesi utapambana nayo baadae
Ahsante kwa ushauri mkuu mohammedbsr
 
Ugumu unauleta wewe Mkuu
Ati miti iniozeshee mabati yangu au iifanye nyumba yangu kuwa na nyufa,kisaaa,!!!!Miti ndio inaleta thamani ya kiwanja chake...Aseee!!!kwangu mimi hio ni sawasawa na mende kuangusha kabati
Mimi jirani yangu ana mti mkubwa saaana wa mzambarao siku majani yakianza kudondoka na kunichafulia Ua wangu tu,Fasta kibarua anakweya juu na panga na kukata matawi yoote
Huyo jirani yangu mwenye huo mti alishanitishia polisi mara kuniroga mara aniletee barua ya wito kwa balozi hadi kachemka mwenyewe
Kwasasa kashanizoea
Ukiwa muoga sana utaonewa mnoo
 
Back
Top Bottom