Kwa alivyowekeza jirani yangu kapata faida au hasara?

Kazanazo

JF-Expert Member
Aug 16, 2023
687
1,360
Mwaka 2018 mimi na jirani yangu tuliuziwa plots kwa bei ya 350,000(laki tatu na nusu) kila mmoja kwa maana kiwanja kimoja kimetoka viplot viwili. Kwa wakati huo mfuko wa cement ulikuwa unauzwa kwa sh10,500/= ambapo kwa laki 3 na nusu(350,000) nilikuwa napata wastani wa mifuko 34 hivi.

Baada ya miaka 6 yaani 2024, jirani akaniuzia kile kiplot chake alidai ni kidogo anataka kununua kiwanja kamili akataka nimpe lak9 (900,000) nikampa tukamalizana.

Kwa sasa(2024) cement mfuko ni sh18,500 kwa laki 9 nikama wastani wa mifuko 49 ya cement ambapo ukilinganisha na kipindi kile(2018) ni tofauti ya mifuko 15. Hii ina maana amepata faida ya kama 277,500/= (15×18,500) kwa miaka 6.

Je, tuseme kuwa aliwekeza kwa sense kwamba ardhi inapanda thamani, kwa ongezeko hili la 277,500/= kwa miaka sita ni faida au hasara kama muekezaji?

NB: Tunasema ardhi inapanda thamani ila mimi nafikiri pesa ndio inashuka thamani
 
Inflations hesabu hazipigwi hivo kaka,
Ukipigia hio hesabu kwa bei ya soda utaona jamaa kapata utajiri wa kutisha,
Ukipigia kwa bei ya sukari utaona kapata hasara,

Hesabu za inflation na profit and loss hazitegemei bidhaa moja
Hebu tupige kwa hesabu za soda tuone

Sorry ila nataka kufahamu zaid
 
Thamani ya ardhi hupanda kwa sababu tofauti.

Moja kubwa kabisa ni kukuwa kwa mji, mji unavyokuwa huduma muhimu kuwepo basi thamani itapanda tu.
Kigamboni kuna maeneo yalikuwa yanauzwa laki kadhaa mpaka kufika 2000 na kitu hivi, sasa hivi ni milioni 20+ huko. Jirani hapa mtu kafika milioni 100 kwa eneo tupu kasema hauzi.
Sasa madon wanakuja kununua vibanda, wanahamisha wanajenga, juzi kati tu upande wa pili mtu kauza milioni 150, nyumba ile kwa kipindi alichojenga yeye plus uwanja hakumaliza milioni 30, leo anauza 150.
 
Nakubaliana na wewe kuwa inategemea na kukua kwa mji

Mfano kama jirani angeweza kuuza kwa bei alioniuzia kwa kipindi cha miaka miwili au mmoja(kama mji ungekuwa fasta) angepata faida

Ila mfano mwingine ni hizi nyumba za urithi unakuta bei alionunulia kiwanja na kujenga nyumba marehem kwa kipindi hicho na bei wanayokuja kuuza watoto kwa kipindi cha sasa unaeza kuta ni sawa tu au imezid kidogo kwa kuangalia thamani ya pesa ila wao wataona wamepata mpunga mrefu
 
Thamani ya ardhi hupanda kwa sababu tofauti.

Moja kubwa kabisa ni kukuwa kwa mji, mji unavyokuwa huduma muhimu kuwepo basi thamani itapanda tu.
Kigamboni kuna maeneo yalikuwa yanauzwa laki kadhaa mpaka kufika 2000 na kitu hivi, sasa hivi ni milioni 20+ huko. Jirani hapa mtu kafika milioni 100 kwa eneo tupu kasema hauzi.
Sasa madon wanakuja kununua vibanda, wanahamisha wanajenga, juzi kati tu upande wa pili mtu kauza milioni 150, nyumba ile kwa kipindi alichojenga yeye plus uwanja hakumaliza milioni 30, leo anauza 150.
Dah mkuu katika majuto yangu ya maisha ni kutokununua kiwanja kigamboni mapema daah nmekaa miaka minne kwa urassa akat nko chuo since 2012 ile hela nilionunulia san lg ilioshikwa ndani ya wiki 2 na watu wa jiji na sijaiona tenaa si bora ninge hold kiwanja kibada au kisiwani am sure bei ilikua mlalo sanaa daah majuto mjukuuu matokeo yake nimenunua mwaka huu ila ni mbaliii kuja kutoboa posta town lisaa sijui na kule patakua town ln.
 
Dah, pole mkuu, kigamboni sasa hivi imekuwa ya moto mnoo.
 
Tufafanulie kidogo iyo concept mkuu
Is a concept that a sum of money is worth more now than the same sum will be at a future date due to its earnings potential in the interim.
Yaan,kiasi cha hela ulichonacho kwasasa kuna thamani kubwa kuliko kiasi hikohiko cha hela ukiwa nacho mbeleni.
Mfano:shilling 10,000 ukiwa nayo mkononi sasa,thamani yake ni kubwa kuliko shilingi 10,000 ukiwa nayo mkononi baadaye (wiki,mwezi au mwaka ujao)...

Hii kutokana na mfumuko wa bei wa vitu/ interest rate...
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom