Nilishajiridhisha siku nyingi kuwa hapa JF ni kisima cha faraja na pia kuna maudhi madogo madogo. Nina tatizo na jirani yangu kiasi kwamba nimekosa ufumbuzi hadi nimefikia maamuzi ya kuwaomba ushauri wanaJF.
Ni kwamba kuna jirani yangu ambaye yeye hajajenga bado (ni uwanja/kiwanja) tu. Katika kiwanja chake hicho amepanda miti ya aina ya mikaratusi imekuwa mirefu sana. Miti hiyo amepanda hadi mpakani kabisa na kwangu. Kunapokuwa na mvua na upepo mkali miti inainama hadi inakwaruza bati la nyumba yangu.
Nimemuomba sana akate miti minne ambayo ndio hatarishi lakini yeye majibu yake siku zote ni kwamba, hawezi kukata miti yake kwa kuwa ndio inayokipa kiwanja chake thamani siku akitaka kukiuza. Nilimuliza ni vipi athamini hela kuliko uhai wangu na nyumba yangu akasema kwa hilo nitamsamehe labda akate mti mmoja tu.
Naomba mnisaidie je hili suala nilipeleke kwenye mamlaka ipi ya serikali? Nakiri kuwa negotiation na mediation vimekwama kabisa.
Petro E. Mselewa nisaidie mkuu na wengineo wengi