Niliyoyashuhudia nilipofunguliwa macho

Ila kutumia majini ruksa sio??
 
Qur'an 2🙁30-31)
 
Al baqarah (30-31) imetajwa mbona
 
Wow😍 Allah akulipe kheir kwa kushare nasi wosia huu mzuri wenye Manufaa, nimeguswa hapo uliposema “Amka usiku ongea na Mola wako kwa kumaanisha Moyoni na Mdomoni, wallahi ibada za usiku zina nguvu mnooo, Mungu anajibu muhimu Subra tu🤲🏽 and Lastly khs Waganga umemaliza kila kitu♥️♥️
 
Kwanini kabla ya Uislam na Waarab tulikuwa hatuna majini tuliamini mizimu yetu tu na tulifanikiwa? Hizi dini za kuletewa bwana, aliyetuletea inabidi akamatwe haraka sana.
 
Mimi bwana siku zote nina mashaka na dini ya Kiislam, sina imani nayo hata kidogo.
 
Kwanini kabla ya Uislam na Waarab tulikuwa hatuna majini tuliamini mizimu yetu tu na tulifanikiwa? Hizi dini za kuletewa bwana, aliyetuletea inabidi akamatwe haraka sana.
Majini yalikuwepo hata katika ukristo,mfalme sauli alienda kwa mwanamke wa kike kutaka kupata ufumbuzi kutoka kwa pepo

1 Samweli 28:6-8
[6]Lakini Sauli alipouliza kwa BWANA, BWANA hakumjibu, wala kwa ndoto, wala kwa Urimu, wala kwa manabii.
And when Saul enquired of the LORD, the LORD answered him not, neither by dreams, nor by Urim, nor by prophets.
[7]Ndipo Sauli akawaambia watumishi wake, Nitafutieni mwanamke mwenye pepo wa utambuzi, nipate kumwendea na kuuliza kwake. Watumishi wake wakamwambia, Tazama, yuko mwanamke mwenye pepo wa utambuzi huko Endori.
Then said Saul unto his servants, Seek me a woman that hath a familiar spirit, that I may go to her, and enquire of her. And his servants said to him, Behold, there is a woman that hath a familiar spirit at Endor.
[8]Basi Sauli akajigeuza, na kuvaa mavazi mengine, kisha akaenda, yeye na watu wawili pamoja naye, wakamfikilia yule mwanamke usiku; akasema, Tafadhali unibashirie kwa utambuzi, ukanipandishie yeye nitakayemtaja kwako.
And Saul disguised himself, and put on other raiment, and he went, and two men with him, and they came to the woman by night: and he said, I pray thee, divine unto me by the familiar spirit, and bring me him up, whom I shall name unto thee.
 
Mfano uliotoa ni kwa ajili ya hizi dini za mashaka au kimchongo, hizi dini zote zinaabudu majini sisi tukiabudu mizimu yetu wanasema ni ushetani. Sasa nani ni shetani kati yao na sisi?
 
Kwahiyo kwa haya hii inathibitisha kuwa majini ni mapepo.
Kwa wakristu hakuna jini mzuri wote ni mapepo tu.
Na hapo ndipo tofauti ya hizi dini mbili kuhusu majini.
Jini hana nafasi kwa Mkristo safi
 
Etugrul Bey Arsis akijibu niite kaka kasema kabla ya kumjibu Qareen na Arsh Arsis ajibu kiufasaha Umm Subiyan na Abu Subiyan, Arsh na Kurs ni nini na watumishi wa Kurs na awataje watumishi wa Arsh ataje tofauti ya Arsh na Kurs kisha atajibu kuhusu Qareen na Arsh.
Kasema atakujibu iwapo utamjibu maswali yake kwenye Audio Arsis
 
Sasa ndio jiulize kwanini mfalme Sauli alitaka msaada kwa majini/mapepo
Kwanza mfalme Sauli ni kabla ya Kristo.
Pia ktk haya hiyo mfalme Sauli alikengeuka Mungu wa Israel akamuacha, baada ya kuona hapati msaada kwa Mungu wa Israel ndipo akakimbilia kwa muonaji (mganga)
Kwa ujumla hatua hiyo ilikuwa ni kufuru mbele za Mungu.
Hata sasa kutegemea habari zozote kwa mapepo na majini ni kufuru mbele za Mungu.
Ndio maana tumekatazwa kupiga bao.
Jini halikai ndani ya mkristo safi ila ni rahisi kukaa kwa muislamu safi.
Tusilazimishe mambo, hizi ni dini mbili ni tofauti( ukristo na uislamu) haziingiliani hata chembe.
Ni mpumbavu anayejaribu kuzilinganisha au kuzifananisha hizi dini mbili.
Mapokeo ya dini hizi mbili hayaelekeani.
 
Sawa boss,wenye hekima zetu tunakuelewa

Kukubali ukweli wakati mwingine ni jambo zuri sana,usiogope ukweli
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…