Niliyoyashuhudia nilipofunguliwa macho

Gazeti la Mwananchi
 
Majini wanatumia vifaa ila mpaka apewe na binadamu.

Pia jinn huwa wanawasiliana na mtu kichwani anamwambia andika hivi hivi SEMA hivi sio lazima apande kichwani mtu atokwe ufahamu.
 
Akili ni nini kwa mujibu wa Qur'an?
Asante kwa swali lako, Kwanza ni vema kutambua Qur an sio kamusi kwamba utakuta inatoa maana ya maneno moja kwa moja mfano ukute eti kwenye quran kumeandikwa akili ni '.................' hilo hakuna ila quran inatoa dondoo ambazo zinaweza kutupa maana ya akili.
Quran ilipoitaja akili ilikuwa inajua inaongea na watu ambao tayari wana lugha yao ambayo wanaelewa maana ya akili, Ijapokuwa tafsiri ya neno huweza kubadilika kulingana na muktadha na uelewa wa mfasiri kama vile ambavyo sisi waswahili unaweza uliza watu kumi kuwa mnajua maana ya akili wakakujibu ndio ila ukisema kila mtu mmoja aelezee atatoa maelezo yake tofauti ila maana alisi inabaki vilevile.
Kwa kiswahili Neno “akili” ni uwezo wa mtu wa kufikiri, kuelewa, na kufanya maamuzi. Hii ni pamoja na uwezo wa kupanga, kutatua matatizo, na kujifunza vitu vipya.
Tuje kwa mujibu wa Quran sasa, Katiaka quran neno akili limetumika katika aya hizi

1. Al-Imran 3:190 "إِنَّ فِي خَلْقِ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَاخْتِلَافِ اللَّيْلِ وَالنَّهَارِ لَآيَاتٍ لِّأُو۟لِي ٱلْأَلْبَابِ"
"Hakika katika uumbaji wa mbingu na ardhi na utofauti wa usiku na mchana kuna ishara kwa wenye akili."

2.Al-Mulk 67:10 "وَقَالُوا لَو كُنَّا نَسْمَعُ أَوْ نَعْقِلُ مَا كُنَّا فِي أَصْحَابِ السَّعِيرِ"
Na walisema: ‘Kama tungelisikia au kuwa na akili, tusingekuwa miongoni mwa watu wa moto.’"
Hizo ni baadhi ya aya zenye matumizi ya neno akili sasa kupitia dondoo hizo tunaweza sema kwa mujibu wa quran akili ni:-
1. inamaanisha uwezo wa kufikiri, kuelewa, na kufanya maamuzi. Hii ni pamoja na matumizi ya hekima na busara katika maisha ya kila siku.

2.Ni uwezo wa binadamu kufahamu, kuelewa, na kufanya maamuzi sahihi katika mambo ya kiroho na ya maisha ya kila siku. Ni sehemu muhimu ya kuelewa na kutekeleza maagizo ya Mungu.

Karibu kwa maswali zaidi mkuu.
 
Mkuu kwa kuwa hiyo ni life experience basi wewe endelea na episode tu huenda tukajifunza jambo, Kuna mambo umeyaeleza yanaendana na vitabu vya dini na kuna mambo hayaendani na vitabu but all in all wewe tiririka tu.
 
Kama unasema Adamu wapo wengi maana yake Waliumbwa Adam wengi, Huoni kuwa hiyo haibadilishi kauli ya kuwa mtu wa kwanza kuumbwa ni Adamu?
maana kama kuna adamu wengi basi yeyete katika hao adamu walioumbwa awe atakavyokuwa ila itabaki mtu wa kwanza kuumbwa ni adamu nafikiri logically nipo sahihi.
Ningetegemea useme kuwa adamu sio mtu wa kwanza kuubwa kisha utuambie kwa mujibu wa quran mtu wa kwanza kuumbwa ni.......... kisha utupe ushahidi, Lakini hoja ya kusema kuna Adamu wengi sio hoja kuwa adamu sio wa kwanza.
Mimi nasubiri useme kwa mujibu wa quran Nani ni binadamu wa kwanza ? na yeye adamu aliyetajwa katika baqarah ni wangapi ? huyo wa kwanza anaitwa nani? na katajwa wapi katika quran?
Tikienda kwa njia hii tutaelimishana vizur kuliko maneno mengi yasiyo na majibu.
 
Hoja kuwa Arsis ni kiumbe gani haina shaka hiyo huyu ni jinn kwa ambaye anaelewa kidogo kuhusu viumbe hivi utajua kuwa ni jinn.
Na ukifuatilia vizuri story zake utagundua kuna mahali imesemwa kabisa kuwa ni JINN
Mimi natilia mkazo tu mkuu majini wengi sturborn ndio maana hapo Arsis hawezi endelea mpaka tukiri aya ya kuwa Adam Ni binadamu wa kwanza haipo kwenye quran
Kama angiwa ni binadamu angemwaga elimu tu alafu mwishoni wenyewe tungekiri kuwa Adam sio wa kwanza kuumbwa.
 
Pole mkuu umejaribu kupata tiba yoyote ? kama ndio ni tiba gani?
hospital nimezunguka sana, hakuna kilicho eleweka, nikapelekwa kwa watu wa kiroho na kwenyewe ni watu wa pesa, nikaona ni ufala nitulie tu. natamani kuona hiyo siri niliofichwa na hapo ndo kipengele huanza.
 
Wewe lete mkasa tusome ndo unakiweza hufurahia, elimu huna wala huyo Arsis wako, hakuna wajinga humu wa kupotoshwa na elimu sio 😀
Dada, ni wapi umeagizwa hivyo na members humu?

Be humble, ni topic yake Jamaa, muache aitawale apendavyo na Tuache members tunaotaka kuendelea kumsoma, Tumsome kwa Amani.

You can’t control what’s not Yours.
 
Umesema kuna majini wazuri na majini wabaya, je mgawanyiko huo upo pia kwa Malaika ikiwa ona maana kuwa kuna Malaika wazuri na Malaika wabaya?
Chifu hakuna malaika wazuri wala wabaya inategemea aliyewatuma, amewatuma kwa kazi gani
 
Hizo za bibia nimekwambia ndsio umeyaakinisha usemi wangu, kua Waislam hakuijui Qur'an, mnatumia biblia kua ndio tafsirri ya Qur'an.

Hilo ni kosa kubwa sana, mnatakiwa muisome Qur'an kama ilivyom Qur'an haikuja kuiyakinisha biblia. Qur'ana imekuja kuweka kuweka wazi ukweli , imewajia haki.

Hata ukiukwepa mjadala wa Adam, hujafanya kitu, kwa sababu ni mengi sana mnayatafiri kutoka kwenye biblia, mmejazwa uongo na nyinyi mnausambaza bila kujijua. Nyinyi na mashehe zenu.

Arsis: Hilo la Adam kua mtu wa kwanza ni la fikra zako wewe Kwa kua umeshakua brain washed kwa miaka, Halipo kwenye Qur'an. Siwezi kuilingania dini ya Allah kwa kuongeza langu kwenye Qur'an, mbalo halipo kabisa, kwa kulitoa kwenye bibllia.

Hicho ndicho ninachokisisitiza. Waislam kama tumeshaamini vitabu vyake, tuisome Qur'an kama ilivyo, biblia sio katika vitabu vya Allah. Qur,an ni ni nyepesi sana kuielewa. Ukiangaza kuingiza yasiokuemo unajifanyia mwenyewe ugumu, unaishia kuilingania na kufundish biblia bila kujijua,

la Adam unalikwepa, jibu la Hawa basi. Kua mkweli wa nafsi yako, mmemtoa wapi? kama huwezi kujibu, mimi nasema, mmemtoa kwenye biblia pia. kama unapinga hilo sema wewe umemtoa wapi? Muulze na Shehe wako kamtoa wapi?

Nakupa nyingine mpya, hizo umerusha lakinoi hazikwepeki. Sarah, Waislam mmemtoa wapi na hata majini wakiisikia wanayakinisha hili na kutetemeka kwa ubira wake.kumtungia visa chungu nzima?

Hii elimu ipo ndani ya Qur'an ni kubwa na pana sana, mnatakiwa mtulizane kuisoma.Muulize mashehe wenu,mfanye na tafiti zenu, muache kuisambaza biblia bila kujijua.

Fundisheni Qur'an kwa walimwengu wote, ni kitabu bora ambacho hakina shaka ndani yake na hakikuletwa kwa ajili ya wanaojiita Waislam tu, muongozo kwa kila mmoja wetu na atakaeusoma lazima aongoke na apate hamu ya kuujua Uislam ni nini. Hata babu zako ilikua hivyo.

Arsis.


.
 
Umwagaji damu kwa maana mauji ufisadi, lkn naona unalinganisha adam na damu,sio sawa

Je majini hawana damu?
Jitahidi sana kusoma ili uelewe kwanza kabla ya kutafuta majibu.

Nimeandika; Damu (Adamu?!)

Unatambua lugha za uandishi?


Kingine, huo unaosema umwagaji Damu na ufisadi vyote ni tafsiri na sifa za binaadam/Bin- Adamu.

Kama majini yameumbwa kwa moto, hiyo Damu wataitoa wapi?

Damu ni nini?




Ni kweli kwamba Islams tunasoma na kutengeneza tafsiri zaidi kwenye Quran kuliko Quran yenyewe.
 
hospital nimezunguka sana, hakuna kilicho eleweka, nikapelekwa kwa watu wa kiroho na kwenyewe ni watu wa pesa, nikaona ni ufala nitulie tu. natamani kuona hiyo siri niliofichwa na hapo ndo kipengele huanza.
Pole sana, Kwanza anza kubadilisha mfumo wa maisha yako kama kuna mambo unafanya hayampendezi Mungu acha kabisa, Maaswi yanampa nguvu shetani. Hii ni katika tiba za kitabia .
Pili kuna tiba za kimaumbile yaani hakikisha mazingira yako na wewe mwenyewe unakuwa msafi muda wote safisha mwili, ondoa najsi na uchafu katika mazingira yako.
Tatu, Anza kufanya ibada mimi sijui wewe ni dini gani ila nacho kuambia anza kufanya ibada mkuu hasa muombe Mungu msamaha kwa makosa unayoyajua na usiyo ya jua omba sana msamaha narudia sana kuna siri katika kuomba msamaha wa makosa yetu sisi waislamu tunasema kuleta istighfar.
Mwisho, tumia chumvi unapooga ya mawe au kawaida, tafuta majani ya mkunazi ogea , tafuta majani ya mbaazi twanga ogea na mizizi yake kausha ogea mengine kunywa.
Mwisho toa sadaka tafuta mtoto yatima mpe sadaka kisha mwambie akuombee dua.
Usichoke mkuu matatizo ni sehemu ya maisha yetu ila usikate tamaa na rehma za mola wako
 
Mbona hujadaut uelewa wa Arsis kuhusu Uyaudi?
Simba; hakuna nchi inaitwa Uyahudi, si zamani au sasa. Kuna wayahudi' ambao ni kizazi cha Yuda.

Kusema uyahudi ni kama upo Dodoma mjini useme kuna uhindini, ni kisehemu ambacho wanaishi wahindi. Hili lipo sana Tanzania, Dar kuna Uzunguni. Kuna uhindini na siku hizi kuna uswahilini. kwingine Tanzania kuna Uarabuni. Kuna Ungindoni.

Kuna China Town huko New York, haimaanishi upo Uchina.

Natumai umeielewa hio mifano ya kufafanua kuhusu uyahudi.
Simba.
 
Umesema kuna majini wazuri na majini wabaya, je mgawanyiko huo upo pia kwa Malaika ikiwa ona maana kuwa kuna Malaika wazuri na Malaika wabaya?
Simba; haupo kwa malaika, kwa sababu malaika hajapewa matamanio na maamuzi, wanafanya walichoamrisha na muuma wao wetu.

wazuri na wabaya ni sifa za watu na majini.
Simba.
 
Mwaga elimu.
Simba.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…