Niliyoyashuhudia leo Muhimbili

Niliyoyashuhudia leo Muhimbili

Za kuambiwa changanya na zako, ni lini uliwaona wameshika hatamu wakafanya haya haya!?
Kuna vitu ni rahisi kuvielewa, lakini inashangaza kuona ni vigumu kueleweka!! Kusema tu "haya haya" maana yake ni mabaya (hatuyataki). Sasa ni kipi tunachong'ang'ania kuwa na walewale wanasababisha "haya haya"?! Nitoe mfano: Kipindi hiki cha corona, mtu akiumwa akaenda hospitali, asipopata tiba, ni wazi atarudi nyumbani, na kwa hakika hata kujifukizia atajifukizia. Na akijifukizia, asipopona bado akiambiwa arudi hospitali (hata kama mwanzo hakupata tiba) atarudi tu. Tupo na wale wale wanaotufanyia "haya haya" miaka yoote, lakini wanakuja "wenye kutuhubiria tiba mbadala" hatutaki kujaribu, tunajisemea (au tunasemewa na wale wale wanatufanyia "haya haya") kuwa hata hao "wanaojitapa kuwa wa tiba mbadala" watafanya "haya haya". Khaa Watz!!!
Mkuu watz ni waoga wa mabadiliko na wabinafsi .

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu usiwalumu madaktari na manesi, kuna wengi wamepoteza maisha, wengine wanaumwa na wengine wamejiweka karantini wenyewe.

Hakuna mtu mpumbavu anayeweza kuhatarisha maisha yake kukusaidia wewe wakati akipona huduma nzuri sifa zote unapeleka kwa mungu wa Chato.

Kama vipi nenda kwa mungu wa Chato akufukize
 
Hao wa presha za kushuka unawakorogea kahawa kikombe kimoja na ikibidi unamchochea na konyagi ndogo mpaka jasho

Unaweza kwenda na matatizo ya kapresha ka kushuka unarudi na kacorona
 
Hawana PPE hawataki kufa na kuacha wapendwa wao wanaangaika
Madaktari wamesikiliza maneno ya mitandaoni kuwa Hali ni mbaya kwanini wasiogope?.
maana huku mitandaoni kila mgonjwa anaepelekwa hospital wanasema ana corona kila mtu akifa wana sema ana corona kwanini wasiogope.
TUBADILIKE SISI KWANZA.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hao wa presha za kushuka unawakorogea kahawa kikombe kimoja na ikibidi unamchochea na konyagi ndogo mpaka jasho

Unaweza kwenda na matatizo ya kapresha ka kushuka unarudi na kacorona


Uwiiii🤣🤣🤣🤣! Dah .🙌🙌🙌🙌..u made my nite aisee .mie had nahis kushikwa vichomi kwa kucheka🤣
 
Madaktari wamesikiliza maneno ya mitandaoni kuwa Hali ni mbaya kwanini wasiogope?.
maana huku mitandaoni kila mgonjwa anaepelekwa hospital wanasema ana corona kila mtu akifa wana sema ana corona kwanini wasiogope.
TUBADILIKE SISI KWANZA.

Sent using Jamii Forums mobile app

Wewe husiyejitambua. Madaktari wajua hali halisi kuliko hii mitandao.
 
Tatizo ni kwamba haitatokea tukaongea lugha moja

No no usiseme haitatokea
It will when the conditions are met, kuongea lugha moja is absolutely Possible


I'm on that good kush and alcohol
 
Salamu wote. Corona imetuletea tafrani kubwa. Leo nimempeleka Muhimbili mgonjwa mwenye presha ya kushuka.

Alikuwa mahututi, hawezi hata kuongea. Kufika mapokezi dr mmoja (jina lake sikufanikiwa kulijua) aligoma kumpokea akidai kwamba twende hospitali ya Temeke au Mwananyamala.

Nikamuuliza dr kwa hali ya mgonjwa ilivyo huoni kama akichelewa kupata tiba yanaweza kutokea mengine. Jibu alilonipa nilichoka. Alijibu kwamba mgonjwa bado hajazidiwa na hawezi kumtibu hivyo tuondoke.

Sikuwa na jambo lingine la kufanya zaidi kumpeleka mgonjwa hospitali ya private. Siku hizi ukimpeleka mgonjwa hospitali nyingi (za serikali) akiwa mahututi, ma-dr na ma-nesi wanaogopa kumuhudumia, wanahukumu kwamba kila mtu ameambukizwa Corona.

Wizara ya afya imeshindwa kutoa huduma bora kwa wakati. Wagonjwa wengi wanakufa kwa kukosa matibabu.

Hayo nimeshuhudia kwa macho yangu leo tarehe 30 Machi, 2020 hospitali ya MUHIMBILI saa 7 mchana.

Sent using Jamii Forums mobile app
Siku nyingine unamrekodi na unamtupia mtandaoni tu ili tumuone sura yake usije ukawa unalalamika kumbe umekutana na wakala wa shetani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom