Niliyoyashuhudia leo Muhimbili

vamda

JF-Expert Member
Aug 1, 2012
864
534
Salamu wote. Corona imetuletea tafrani kubwa. Leo nimempeleka Muhimbili mgonjwa mwenye presha ya kushuka.

Alikuwa mahututi, hawezi hata kuongea. Kufika mapokezi dr mmoja (jina lake sikufanikiwa kulijua) aligoma kumpokea akidai kwamba twende hospitali ya Temeke au Mwananyamala.

Nikamuuliza dr kwa hali ya mgonjwa ilivyo huoni kama akichelewa kupata tiba yanaweza kutokea mengine. Jibu alilonipa nilichoka. Alijibu kwamba mgonjwa bado hajazidiwa na hawezi kumtibu hivyo tuondoke.

Sikuwa na jambo lingine la kufanya zaidi kumpeleka mgonjwa hospitali ya private. Siku hizi ukimpeleka mgonjwa hospitali nyingi (za serikali) akiwa mahututi, ma-dr na ma-nesi wanaogopa kumuhudumia, wanahukumu kwamba kila mtu ameambukizwa Corona.

Wizara ya afya imeshindwa kutoa huduma bora kwa wakati. Wagonjwa wengi wanakufa kwa kukosa matibabu.

Hayo nimeshuhudia kwa macho yangu leo tarehe 30 Machi, 2020 hospitali ya MUHIMBILI saa 7 mchana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Duh pole sana….kuna umuhimu wa uelewa juu ya huduma ya kwanza... Presha ya kushuka kuna huduma ya kwanza mngempa maana hata kwenda hospital kipindi hiki ni kujiexpose kwenye magonjwa...…...

Poleni sana hope mlipata huduma nzuri huko mliko mpeleka.
 
Madaktari wamesikiliza maneno ya mitandaoni kuwa Hali ni mbaya kwanini wasiogope?.
maana huku mitandaoni kila mgonjwa anaepelekwa hospital wanasema ana corona kila mtu akifa wana sema ana corona kwanini wasiogope.
TUBADILIKE SISI KWANZA.

Sent using Jamii Forums mobile app
Unaposema sisi unamaanisha nini? Hao madaktari siyo sisi? Tunaoandika hapa siyo sisi? Wanaokataliwa kupokelewa siyo sisi??
 
Back
Top Bottom