Niliyoyashuhudia leo Muhimbili

Niliyoyashuhudia leo Muhimbili

Kazi ya wazua taharuki mtandaoni hiyo...pole sana kiongozi,hope atapona
 
Kila siku online watu wanasema thank you doctors and nurses mnaotupigania kwenye hili janga ila madokta wa bongo na nurses mnaokimbia wagonjwa wote f***k you na serikali yenu.
 
Halafu utawapigia kura watu hawahawa
Hivi mkuu kweli katika hali ya kawaida tu, hawa wanafaa kuachiwa ile ikulu ya chamwino kweli na uwakabidih hazina kweli
chadema3.jpg
Chadema1.jpg
Chadema2.jpg
Chadema.JPG
chadema3.jpg
Chadema1.jpg
Chadema2.jpg
Chadema.JPG
 
Assumptions hizo, hawa tunawafahamu na kuwajua, wale wengine hatuwajui; kwanini tusiwajaribu tuone? Cause hata hiyo mikakati yao ambayo inasifiwa, ni mawazo ya hawa hawa tusiowajua, yaani wana copy tu na kupestia kwao.
Hawa wengine mbona wanajulikana tu kweupee....!!! Jinsi wanavyogeuza vyama vya siasa kuwa mali yao binafsi; Wanavyojisultanisha uongozi wa milele wa chama, na wanavyofisidi ruzuka za chama, huku wakiwapatiliza ama kuwafunga midomo wanaohoji matumizi yasiyofaa!
 
Hata Mimi mwanzo nilikuwa nawalaumu madaktali na manesi ila kwa sasa siwalaumu nimeshajua tatizo sio wao tatizo ni serikali haijawaandalia vifaa vya kujikinga na corona kipindi hiki ambacho corona imetapakaa

Kwa mfano hapo Amana nesi anajipitia tu na mavazi yake ya kawaida unakuta wagonjwa wa corona wanamuita aende akawahudumie hata ningekuwa mimi siwezi kwenda

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yule mzee aliyejificha chato alidhania kupambana na corona ni kazi rahisi

Sasa inabidi agawe mavazi ya kujikinga na corona kwa madaktali na manesi wote wa Tanzania nzima

Maana hata kama wewe unaumwa maralia doctor ataamini vipi kama wewe huna corona na atakutibia vipi wakati yeye amevaa tisheti na jinsi tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Salamu wote. Corona imetuletea tafrani kubwa. Leo nimempeleka Muhimbili mgonjwa mwenye presha ya kushuka.

Alikuwa mahututi, hawezi hata kuongea. Kufika mapokezi dr mmoja (jina lake sikufanikiwa kulijua) aligoma kumpokea akidai kwamba twende hospitali ya Temeke au Mwananyamala.

Nikamuuliza dr kwa hali ya mgonjwa ilivyo huoni kama akichelewa kupata tiba yanaweza kutokea mengine. Jibu alilonipa nilichoka. Alijibu kwamba mgonjwa bado hajazidiwa na hawezi kumtibu hivyo tuondoke. Sikuwa na jambo lingine la kufanya zaidi kumpeleka mgonjwa hospitali ya private. Siku hizi ukimpeleka mgonjwa hospitali nyingi (za serikali) akiwa mahututi, ma-dr na ma-nesi wanaogopa kumuhudumia, wanahukumu kwamba kila mtu ameambukizwa Corona.

Wizara ya afya imeshindwa kutoa huduma bora kwa wakati. Wagonjwa wengi wanakufa kwa kukosa matibabu. Hayo nimeshuhudia kwa macho yangu leo tarehe 30 Machi, 2020 hospitali ya MUHIMBILI saa 7 mchana.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mubimbili ni hosipitali ya rufaa ya taifa labda walikuambia umpeleke huko kwingine kwakua ndiyo utaratibu baada ya kuona hali ya mgonjwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Salamu wote. Corona imetuletea tafrani kubwa. Leo nimempeleka Muhimbili mgonjwa mwenye presha ya kushuka.

Alikuwa mahututi, hawezi hata kuongea. Kufika mapokezi dr mmoja (jina lake sikufanikiwa kulijua) aligoma kumpokea akidai kwamba twende hospitali ya Temeke au Mwananyamala.

Nikamuuliza dr kwa hali ya mgonjwa ilivyo huoni kama akichelewa kupata tiba yanaweza kutokea mengine. Jibu alilonipa nilichoka. Alijibu kwamba mgonjwa bado hajazidiwa na hawezi kumtibu hivyo tuondoke. Sikuwa na jambo lingine la kufanya zaidi kumpeleka mgonjwa hospitali ya private. Siku hizi ukimpeleka mgonjwa hospitali nyingi (za serikali) akiwa mahututi, ma-dr na ma-nesi wanaogopa kumuhudumia, wanahukumu kwamba kila mtu ameambukizwa Corona.

Wizara ya afya imeshindwa kutoa huduma bora kwa wakati. Wagonjwa wengi wanakufa kwa kukosa matibabu. Hayo nimeshuhudia kwa macho yangu leo tarehe 30 Machi, 2020 hospitali ya MUHIMBILI saa 7 mchana.

Sent using Jamii Forums mobile app
Naamini umeleta taarifa hiyo kishabiki tu na siyo kiuhalisia. Taarifa za uchochezi hazikusaidai kamwe kufikia lengo lako.

Unajua fika Muhimbili ni hospitali ya rufaa. Wagonjwa wanaopokelewa hapo wanapaswa kuwa walio na rufaa tu. Kuimarishwa kwa hospitali za Wilaya na Mikoa, Vituo vya afya na Zahanati nchi nzima, Muhimbili imebaki na jukumu lake la msingi. Hivyo basi, kama ni kweli ulimpeleka mgonjwa wako, ni kwa kimazoea, ndiyo maana umekwama.
 
Duh pole sana….kuna umuhimu wa uelewa juu ya huduma ya kwanza... Presha ya kushuka kuna huduma ya kwanza mngempa maana hata kwenda hospital kipindi hiki ni kujiexpose kwenye magonjwa...…...

Poleni sana hope mlipata huduma nzuri huko mliko mpeleka.
Mkuu tusaidie hii huduma
 
Niliwahi kuandika humu nilienda tu Zahanati ya karibu kupima Malaria na nilikuwa na kikohozi cha kawaida kutokana na hali ya hewa, Daktari niliyemkuta alikuwa ananiuliza maswali akiwa na jazba kama anahoji mwizi.

Madaktari wapo katika hali ya taharuki kwa kukosa vifaa vya kujilinda na mazingira wezeshi, sasa hivi kama kuna uwezekano wa kujitibia ukiwa nyumbani ni bora ukae na dawa zako za kutosha.

Watu wengi watapoteza maisha kwa hali za utata kwa magonjwa ya kawaida kwa sababu ya kukosa huduma.
 
Back
Top Bottom