Niliyoyashuhudia leo Muhimbili

Niliyoyashuhudia leo Muhimbili

Pole sana mkuu, sasa hivi kuna magonjwa mawili haya bado madaktari wetu yanawavuruga vichwa vyao sana,

Moja ni Changamoto ya upumuaji. Hii hupelekea mtu kushindwa kupumua hadi anakata roho.
Pili ni Changamoto ya kusimama. Hii hupelekea mtu kudondoka barabarani hadi anakata roho.

Sasa mnapopeleka wagonjwa hospitali waambieni wajikaze wasionyeshe dalili hizo mbili hapo juu kwenye hatua za awali wafikapo hospitali ili apatiwe matibabu.
Ni wazo zuri

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kada ya afya imevamiwa na mamluki
Umefafanua vizuri.
Ila kuna watu vichwa ngumu.
Mleta mada amesema mgonjwa wake alikuwa anaumwa presha ya kushuka.
Katika Hali ya kawaida wangempa hata huduma ya kwanza.
Lakini walimkataa kabisa .
Swali tujiulize kwanini walimuogopa kumpa hata huduma ya kwanza?

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umefafanua vizuri.
Ila kuna watu vichwa ngumu.
Mleta mada amesema mgonjwa wake alikuwa anaumwa presha ya kushuka.
Katika Hali ya kawaida wangempa hata huduma ya kwanza.
Lakini walimkataa kabisa .
Swali tujiulize kwanini walimuogopa kumpa hata huduma ya kwanza?

Sent using Jamii Forums mobile app
Kada ya afya imevamiwa na mamluki

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukweli ni kua lazima uanzie hospitali za chini kabla ya kwenda rufaa hata kabla ya corona sema wauguzi hawa kua serious kama saivi
 
Kwa uhaba wa vipimio vya Covid19,madaktari wetu wanapima kwa macho.
Too sad.
 
Hata hao wengine wakiingia mambo yatakuwa haya haya unayoyashuhudia sasa hivi

Sent using Jamii Forums mobile app

Za kuambiwa changanya na zako, ni lini uliwaona wameshika hatamu wakafanya haya haya!?
Kuna vitu ni rahisi kuvielewa, lakini inashangaza kuona ni vigumu kueleweka!! Kusema tu "haya haya" maana yake ni mabaya (hatuyataki). Sasa ni kipi tunachong'ang'ania kuwa na walewale wanasababisha "haya haya"?! Nitoe mfano: Kipindi hiki cha corona, mtu akiumwa akaenda hospitali, asipopata tiba, ni wazi atarudi nyumbani, na kwa hakika hata kujifukizia atajifukizia. Na akijifukizia, asipopona bado akiambiwa arudi hospitali (hata kama mwanzo hakupata tiba) atarudi tu. Tupo na wale wale wanaotufanyia "haya haya" miaka yoote, lakini wanakuja "wenye kutuhubiria tiba mbadala" hatutaki kujaribu, tunajisemea (au tunasemewa na wale wale wanatufanyia "haya haya") kuwa hata hao "wanaojitapa kuwa wa tiba mbadala" watafanya "haya haya". Khaa Watz!!!
 
Salamu wote. Corona imetuletea tafrani kubwa. Leo nimempeleka Muhimbili mgonjwa mwenye presha ya kushuka.

Alikuwa mahututi, hawezi hata kuongea. Kufika mapokezi dr mmoja (jina lake sikufanikiwa kulijua) aligoma kumpokea akidai kwamba twende hospitali ya Temeke au Mwananyamala.

Nikamuuliza dr kwa hali ya mgonjwa ilivyo huoni kama akichelewa kupata tiba yanaweza kutokea mengine. Jibu alilonipa nilichoka. Alijibu kwamba mgonjwa bado hajazidiwa na hawezi kumtibu hivyo tuondoke.

Sikuwa na jambo lingine la kufanya zaidi kumpeleka mgonjwa hospitali ya private. Siku hizi ukimpeleka mgonjwa hospitali nyingi (za serikali) akiwa mahututi, ma-dr na ma-nesi wanaogopa kumuhudumia, wanahukumu kwamba kila mtu ameambukizwa Corona.

Wizara ya afya imeshindwa kutoa huduma bora kwa wakati. Wagonjwa wengi wanakufa kwa kukosa matibabu.

Hayo nimeshuhudia kwa macho yangu leo tarehe 30 Machi, 2020 hospitali ya MUHIMBILI saa 7 mchana.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ndio maaana tunasema serikali imeshindwa kutimiza wajibu wake, watu hawaelewi pamoja na kupata taabu Yote hiyo mwezi wa kumi utampigia jiwe kura, Halafu mwakani utakuja huku kulalama

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom