Msaada Mwema Uliokaribia Kuniponza

Msaada Mwema Uliokaribia Kuniponza

Jero_pesa

Member
Joined
Dec 28, 2020
Posts
35
Reaction score
46
Eehe bhana eeh, kabla weekend haijaisha na kuingia kwenye hekaheka za wiki nyingine kusaka ugali, acha niwaachie kisa hiki.

Majuzi nilipata mchongo mkoa A. Ni mkoa ambao nilikuwa sijawahi kuishi hapo kabla. Mitaa niliyopata nyumba ya kuishi (getto) kuna uki-sure (mijengo mikali) fulani hivi. Ni mitaa ambayo watu wanaendelea kupimana mifuko kwenye ujenzi.

Kwa kuwa sina uenyeji kivile, siku ambayo siendi kazini huwa natulia ndani tu na mara moja moja hutoka ndani kuangalia na kushangaa jinsi mtaa unavyozidi kupambwa na mikali ya kila aina.

Siku moja kama ilivyo kawaida ya siku za weekend, saa kumi na mbili na nusu nikatoka nje huku nimevalia ki-pensi na T-shirt. Nilizunguka kidogo kisha nikashika njia ya kurudi nyumbani.

Mita kama mia mbili (200m) hivi kabla sijafika magetoni, nikamkuta mzee akiwa na pikipiki aina ya boxer. Mzee alionekana kutapatapa na pikipiki ile kwa kuwa ilimgomea kuwaka huku Giza zinazidi kutanda. Ilikuwa tayari ishafika mida ya - kamtu kale - mpaka mtu husika atakaposegea karibu uweze kumtambua.

Mimi "shikamoo mzee"

Mzee "marahaba babaa, una haraka?"

Mimi "siyo kivile, kwani kuna shida?"

Mzee "nisaidie kusukuma niwashe pikipiki, imezima na nahangaika nayo, sijui kwa sababu nimeipaki muda mrefu"

Kwakuwa sikuwa na haraka kivile, sikusita kumfata mzee alipo na kuanza kumsukuma ili pikipiki yake iwake aendelee na safari.

Sukumaaa, sukumaaa, sukumaaaa........ Bila mafanikio.

Mimi "kick starter kwani haifanyi kazi?"

Mzee "nimekanyaga sana haiwaki hata kidogo, kwa vile wewe kijana hebu jaribu huenda nguvu mimi zimepungua"

Anacheka kicheko kisicho na maana.

Nikajaribu kupiga kick kama mara kumi hivi bila mafanikio.

Mimi "hii pikipiki itakuwa na shida mahali, kwani imezima katika mazingira gani?"

Nilimuuliza vile mzee ili kujua kwa sababu ya pikipiki hii kuzima na kama ni tatizo la kujirudia na huwa analitatuaje.

Mzee "hii pikipiki nimeazima tu kwa kijana mmoja pale kanisani, hebu kwanza ngoja nimpigie nimuulize"

Akachukua simu yake akatafuta namba ya mtu husika, wakati huo mimi naendelea kuangalia hapa na pale.

Mzee "hallo Johnson, pikipiki imenizimia huku kwa akina (jina sikulishika) yaani hata sijui nifanyaje"

Aliendelea "kwani huwa una shida gani? Nimeomba msaada kijana wa watu anisaidie kusukuma na kupiga kick lakini hamna kitu"

Johnson "sijawahi kuona unashida hivi karibu, lakini zamani ilikuwa inanisumbua tatizo la ku-float, kwani uliongezea mafuta?"

Mzee "nimeweka kabisa mafuta ya elfu tano nilipofika sheli, nimekuja naendesha mpaka huku, nahisi labda kwa sababu nimeipaki muda mrefu"

Wakati mzee anaendelea kuongea na mwenye pikipiki, Johnson, akapita jamaa mwendesha pikipiki (bodaboda). Aliposikia mazungumzo yale akasimama na kutuuliza tatizo nini. Nikamwambia pikipiki ya mzee imegoka kuwaka. Akashuka kwenye pikipiki yake na kuweka pembeni.

Jamaa alipiga kick kadhaa, mwisho akapona holaaa, hamna kitu.

Jamaa "Kuna abiria namuwahi chap, wewe endelea kuangalia namna ya kumsaidia"

Jamaa akasepa.

Nikabaki na yule mzee. Wakati huo mimi nilikuwa nimegundua ufunguo wa pikipiki haukuwepo kwenye switch yake.

Basi mzee alivyomaliza kupokea maelezo ya Johnson nikamwambia nilichokiona.

Mimi "mbona ufunguo wake haupo"

Mzee "ufunguo wake upo mfukoni, Johnson aliniambia nikishachomeka funguo niutoe kwa sababu haushiki hapo utadondoka"

Aliendelea "Johnson anasema ina float kwahiyo tujaribu kufungua capulator na waya wa moto"

Mimi "Mimi siyo mtaalam wa pikipiki, naogopa tutaharibu zaidi"

Mzee "hapana, tufungue tu, kwa sababu hapa nitalala wapi, giza hili lote na nyumbani ni (.....)"

Alinitajia jina ambalo hata sikujua ni wapi kwa sababu ya ugeni wangu. Sikutilia maanani, hata hivyo nilielewa ya kwamba anakaa mbali.

Aliendelea pia "Kuna waya hapo umekatika nao tuuangalie, huwa anauunga ukiachia"

Mimi "hamna neno, lakini hebu funguo kwanza tuangalie mafuta yapo kiasi gani"

Mzee alinipa funguo. Lengo lilikuwa kuhakikisha pia kwanini switch iko kwenye OFF, ingawaje mzee amesisitiza kapewa maelezo ya kuchomoa kila anapoiweka ON.

Basi bhana, kuzuga ikabidi nianzie kwenye tank kwanza. Tia funguo, funguo haifungui tank la mafuta. Nikamuuliza kama ana funguo zingine alizofungulia wakati anaongeza mafuta.

Swali langu ni kama linazidi kumchanganya tu maana mpaka muda ule haelewi katembea na shetani gani😂

Wakati mzee anajing'ata ng'ata meno na kusaka misuko yake kama kuna funguo zingine (ilihali anatambua kabisa Hana), ghafla nikasikia jamaa mmoja anawashtua wenzie wake.

Jamaa "oyaaa, njooni chaaap, hii hapa"

Ghafla jamaa wawili mmoja wapo kipande cha dude wakafika...

Mimi wakati huo nimepigwa butwaa, ni kwamba wanakuja kumsaidia mzee kuiwasha ama kuna issue gani.

Jamaa "hii pikipiki unaipeleka wapi"

Mzee ndo kama akili imemruka hivi, nusu acheke nusu alie, lakini kwa vile ni mtu mzima akajifanyaa anachekaa

Mzee "Hahahahahaa hahaha ahaha ahahaaa....."

Huku wakati huo akijikomba komba hapa na pale kwa wale jamaa.

Wale jamaa kwa kweli walikuwa hawacheki hata kidogo. Yaani hata kutoa meno hakuna. Na mbaya zaidi jamaa walikaa kimyaa wakisubiri maelezo.

Mpaka hapo nilielewa kabisa kwamba mzee kashachanganya madesa. Lakini je, MIMI NACHOMOKAJE? Kwamba wale jamaa wataniacha tu? Maana tayari inaonekana pikipiki siyo yake.

Jamaa mmoja akatoa ufunguo akatia kwenye switch kuhakikisha, pikipiki ikawaka dashboard.

Akauliza tena "hii pikipiki mnaipeleka wapi"?

Mzee kwa kichecho na huzuni na majuto makubwa ikabidi akaanza kuomba radhi.

Mzee "nimechanganyaa kabisa uzee huu, hata hiyo pikipiki nimeazima tu na sijawahi kuikariri, nilivyofika pale nikaweka sasa nimerudi nakuta pikipiki nyingi nikachukua hii nikiwa najua ndiyo nimekuja nayo, sasa nimechanganyikiwa kabisa hata sielewi kwanini haiwaki nimemuomba tu huyu kijana anisaidie kuiwasha ttunahangaika naye, sasa nilipowaona nikakumbuka huenda nimechanganya ya kwangu nimeiachaaa"

Alitamka maneno mengi sana na kwa majuto makubwa mno. Wakati huo wale jamaa wako kimya tu.

Aliendelea

"Mimi ndiye mchungaji wa lile kabisa pale (huku akionesha na kidole uelekeo). Nimechukua pikipiki ya kijana wa kanisa nije huku nikaipaki hapa muda mrefu ndiyo maana nikajua tu kwamba imegoma kuwaka kwa sababu ya battery"

Maneno yake yalikuwa mengi tena yaliyojaa uchungu mkubwa na majuto juu yake.

Jamaa mmoja "unajua umetuhangaisha kiasi gani, halafu unaongea unafikiri sisi tunacheka"

Jamaa wa pili "hapana chief, huyu mzee ni kweli kachanganya tu madesa, hebu twende naye kwenye pikipiki tuliyoiacha pale"

Jamaa mwingine "kwahiyo na ulikuwa unamsaidia kutorosha pikipiki yetu"

Jamaa aliniuliza mimi. Kabla sijajibu akadakia jamaa mwingine.

Jamaa "huyu hana kosa, shida ni huyu mzee" twende naye kwenye ile pikipiki tuone kama ndiyo yake.

Tukaongozana mpaka kwenye boxer nyingine iliyofana karibia kila kitu na ile alichukua mzee. Zote zilikuwa nyeusi, hazina cover, hazina side mirror hata moja na zote ni namba D.

Jamaa "leta huo ufunguo"

Jamaa "si unaona, hii ndiyo yake, mwachieni tu aende zake"

Basi jamaa wakamtaka mzee awe makini siku nyingine. Aache kukurupuka kwa sababu kama watu wengine ambao siyo waelewa wangemzibua vibao na uchungaji wake.

Mimi nikaangana na mzee na wale jamaa huku wakiniuliza kama nafahamiana naye. Nikawaambia hapana, mmoja akasema, "acha kuwa mwema, mjini hapa"


MWISHO
 
Back
Top Bottom