SoC01 Nilivyotengeneza kipato kwa mtaji wa Tsh 50,000 tu

Stories of Change - 2021 Competition

Nominee

JF-Expert Member
Sep 5, 2017
459
1,240
Habarini wakuu.

Najua kuna wimbi kubwa sana la vijana wasio na ajira. Hata wanaothubutu kujiajiri nao bado wanapata changamoto mbalimbali na mitaji yao inapotea pasipo kufanya jambo la maana. Hebu soma kisa changu.

Ilikuwa ni mwaka jana(2020) mwezi wa saba nilipoamua kutoka mjini na kuhamia rasmi kijijini mikoa ya Kanda ya Ziwa. Sikuwa na ndugu huko kijijini nilipoelekea bali urafiki wangu na wanafunzi wenzangu tuliosomaga pamoja chuo ndio ulinisaidia kupata sehemu ya kufikia, pia mpenzi/mke wangu ni mwenyeji wa kanda hiyo.

Nakumbuka siku hiyo naingia pale kijijini nilikuwa nimebakiwa na elfu 50 tu mfukoni kama akiba. Nashukuru Mungu sikupata shida ya kula wala kulala kwani mwenyeji wangu alinisaidia hivyo vyote. Nilitumia siku takriban tano kuyasoma na kuyazoea mazingira.

Huku Kijijini ni wakulima wazuri wa karanga,dengu,mpunga,pamba,choroko nk.Na hapa kijijini debe moja(ndoo la lita ishirini) la karanga nyeupe ambazo hazijaondolewa maganda linauzwa kwa shilingi elfu saba au nane na debe moja la karanga nyekundu linauzwa kwa shilingi elfu tano au sita.

Kwa hiyo siku ya sita tangu nifike pale kijijini,asubuhi baada tu ya kuamka nikamuuliza mwenyeji wangu lilipo soko au gulio. Alinielekeza kuwa lipo umbali wa masaa matatu kama utaenda kwa baiskeli. Na bahati nzuri ni kwamba rafiki yangu alikuwa na baiskeli yake,kwahiyo nikaitumia hiyo kwenda huko sokoni.

Nilipofika sokoni nikaulizia bei ya kilo moja ya karanga zilizomenywa/zilizoondolewa magamba ni shilingi ngapi?,nikajibiwa kwamba kwa karanga nyekundu kilo ni sh.1700/= na karanga nyeupe kilo ni sh.2300/=
Ikabidi nimuite pembeni yule muuzaji na nikamdanganya kwamba nina karanga zangu nyumbani,je nikimletea atanunua kwa bei gani ya jumla?.Akanijibu kuwa "Hapa sokoni huwa tunanunua karanga nyekundu kwa bei ya jumla sh.1500/= kwa kilo moja,pia karanga nyeupe tunanunua kwa bei ya jumla sh.2000/= au 2100/= kwa kilo moja".

Basi nikamshukuru kwa maelezo yake na kumuahidi kuwa nitamletea karanga zangu,hatimae nikaondoka na kumfuata muuzaji mwengine ambaye nae alinipa maelezo yaleyale kama ya yule muuzaji wa kwanza. Kwahiyo nilirudi nyumbani nikiwa na taarifa zote kuhusu uuzaji wa karanga.

Nilipokuwa narudi nyumbani baiskeli ilipata pancha tairi moja,nikatumia shilingi mia tano kuziba na shilingi mia moja nikanunulia muwa vipande viwili.Safari ikaendelea.

Nilipitia kwenye baadhi ya familia za wanakijiji wa pale,nikaulizia kama wanauza karanga. Wakanijibu ndio wanauza. Pia nikauliza debe moja la karanga zilizo na maganda ukimenya unaweza kupata kilo ngapi?.Wakanijibu kuwa inategemea ni aina gani ya karanga kama ni 'Sukuma' au 'daki',pia inategemea kama zilikomaa vizuri ama la!!,ila inacheza kwenye kilo 6 hadi 8 kwa debe moja.
Basi nikaamua kununua debe sita za karanga nyeupe.Ambapo nililipa jumla ya shilingi elfu 42/=.Kwahiyo kwenye bajeti yangu nilibakiwa na elfu saba mia nne tu.

Nilipofika nyumbani nilitafuta kijana mwenye mashine ya kumenyea/kuondolea maganda karanga.Nilimpata na tukakubaliana kwamba atamenya kwa shilingi 800/= kwa kila debe moja.Kwakuwa mimi nilibakiwa na elfu saba mianne.Nilimlipa elfu nne mia nane ili amenye debe sita zote.Pia nilimpatia dada mmoja elfu 2 ili anisaidie kupepeta baada ya kuondolewa maganda.Mfukoni sasa nikawa nimebakiwa na shilingi mia sita tu.

Nashukuru Mungu baada ya karanga kuondolewa maganda tukapata jumla ya kilo 35 kwa debe sita zote.Nikazichukua na kurudi nazo nyumbani.

Siku ya pili yake asubuhi nikazibeba na kuzipeleka sokoni ambapo baada ya kuuza nikapata elfu 70/=(kilomoja ya karanga nyeupe niliuza elfu mbili kwa bei ya jumla).Kwahiyo faida nilipata elfu 20/=.

Nilirudi nyumbani nikiwa na furaha sana.Kadiri siku zilivyosonga nilizidi kutengeneza pesa,sinunui tena gunia moja,bali magunia mengi.Nikafungua na saloon ya kike kwa ajiri ya mke wangu,nikafungua na miradi mingine mbalimbali ambayo inazidi kuniingizia pesa kila kukicha.Karanga zimenitoa kimaisha.

USHAURI KWA VIJANA.
Using'ang'anie kukaa mjini wakati huna pesa. Kijijini ni dhahabu kama utajituma vyema na kuishi vizuri na watu.

AHSANTENI.

Usisahau kunipigia kura hapo chini.Bonyeza alama '^' kupiga kura.
 
Hongera sana mkuu. ila swali ni kua karanga ni zao la msimu na mavono hua ni muda mfupi uliwezaje kuuza/kukuza mtaji mpaka kufikia kununua magunia ndani ya muda mfupi?
 
UONGO. Unataka kusema hao wanunuzi walikuwa wakikungoja ww utoke mjini ukawakusanyie karanga huko kijijini???

Je ulipokuwa unatoka mjini hukujua unaenda kufanyaje huko bushland tena ukiambatana na mkeo, maana umesema ni mwenyeji WA huko

Ndani ya miezi 4 unasema umetoka kimaisha na miradi kibao ikiwemo saluni ya mkeo?

Unamaana bado mpaka muda huu unalelewa wewe na mke wako

Vijana tufanye kazi tunazoona zitatutoa, usihame kwenda popote kama hujajiandaa kwa lolote.
 
Alichoandika ni fictional story ila ina inspire japo kwa shilingi 100 kwa karne hii haupati pisi mbili za muwa.
 
Habarini wakuu.

Najua kuna wimbi kubwa sana la vijana wasio na ajira. Hata wanaothubutu kujiajiri nao bado wanapata changamoto mbalimbali na mitaji yao inapotea pasipo kufanya jambo la maana. Hebu soma kisa changu.

Ilikuwa ni mwaka jana(2020) mwezi wa saba nilipoamua kutoka mjini na kuhamia rasmi kijijini mikoa ya Kanda ya Ziwa. Sikuwa na ndugu huko kijijini nilipoelekea bali urafiki wangu na wanafunzi wenzangu tuliosomaga pamoja chuo ndio ulinisaidia kupata sehemu ya kufikia, pia mpenzi/mke wangu ni mwenyeji wa kanda hiyo.

Nakumbuka siku hiyo naingia pale kijijini nilikuwa nimebakiwa na elfu 50 tu mfukoni kama akiba. Nashukuru Mungu sikupata shida ya kula wala kulala kwani mwenyeji wangu alinisaidia hivyo vyote. Nilitumia siku takriban tano kuyasoma na kuyazoea mazingira.

Huku Kijijini ni wakulima wazuri wa karanga,dengu,mpunga,pamba,choroko nk.Na hapa kijijini debe moja(ndoo la lita ishirini) la karanga nyeupe ambazo hazijaondolewa maganda linauzwa kwa shilingi elfu saba au nane na debe moja la karanga nyekundu linauzwa kwa shilingi elfu tano au sita.

Kwa hiyo siku ya sita tangu nifike pale kijijini,asubuhi baada tu ya kuamka nikamuuliza mwenyeji wangu lilipo soko au gulio. Alinielekeza kuwa lipo umbali wa masaa matatu kama utaenda kwa baiskeli. Na bahati nzuri ni kwamba rafiki yangu alikuwa na baiskeli yake,kwahiyo nikaitumia hiyo kwenda huko sokoni.

Nilipofika sokoni nikaulizia bei ya kilo moja ya karanga zilizomenywa/zilizoondolewa magamba ni shilingi ngapi?,nikajibiwa kwamba kwa karanga nyekundu kilo ni sh.1700/= na karanga nyeupe kilo ni sh.2300/=
Ikabidi nimuite pembeni yule muuzaji na nikamdanganya kwamba nina karanga zangu nyumbani,je nikimletea atanunua kwa bei gani ya jumla?.Akanijibu kuwa "Hapa sokoni huwa tunanunua karanga nyekundu kwa bei ya jumla sh.1500/= kwa kilo moja,pia karanga nyeupe tunanunua kwa bei ya jumla sh.2000/= au 2100/= kwa kilo moja".

Basi nikamshukuru kwa maelezo yake na kumuahidi kuwa nitamletea karanga zangu,hatimae nikaondoka na kumfuata muuzaji mwengine ambaye nae alinipa maelezo yaleyale kama ya yule muuzaji wa kwanza. Kwahiyo nilirudi nyumbani nikiwa na taarifa zote kuhusu uuzaji wa karanga.

Nilipokuwa narudi nyumbani baiskeli ilipata pancha tairi moja,nikatumia shilingi mia tano kuziba na shilingi mia moja nikanunulia muwa vipande viwili.Safari ikaendelea.

Nilipitia kwenye baadhi ya familia za wanakijiji wa pale,nikaulizia kama wanauza karanga. Wakanijibu ndio wanauza. Pia nikauliza debe moja la karanga zilizo na maganda ukimenya unaweza kupata kilo ngapi?.Wakanijibu kuwa inategemea ni aina gani ya karanga kama ni 'Sukuma' au 'daki',pia inategemea kama zilikomaa vizuri ama la!!,ila inacheza kwenye kilo 6 hadi 8 kwa debe moja.
Basi nikaamua kununua debe sita za karanga nyeupe.Ambapo nililipa jumla ya shilingi elfu 42/=.Kwahiyo kwenye bajeti yangu nilibakiwa na elfu saba mia nne tu.

Nilipofika nyumbani nilitafuta kijana mwenye mashine ya kumenyea/kuondolea maganda karanga.Nilimpata na tukakubaliana kwamba atamenya kwa shilingi 800/= kwa kila debe moja.Kwakuwa mimi nilibakiwa na elfu saba mianne.Nilimlipa elfu nne mia nane ili amenye debe sita zote.Pia nilimpatia dada mmoja elfu 2 ili anisaidie kupepeta baada ya kuondolewa maganda.Mfukoni sasa nikawa nimebakiwa na shilingi mia sita tu.

Nashukuru Mungu baada ya karanga kuondolewa maganda tukapata jumla ya kilo 35 kwa debe sita zote.Nikazichukua na kurudi nazo nyumbani.

Siku ya pili yake asubuhi nikazibeba na kuzipeleka sokoni ambapo baada ya kuuza nikapata elfu 70/=(kilomoja ya karanga nyeupe niliuza elfu mbili kwa bei ya jumla).Kwahiyo faida nilipata elfu 20/=.

Nilirudi nyumbani nikiwa na furaha sana.Kadiri siku zilivyosonga nilizidi kutengeneza pesa,sinunui tena gunia moja,bali magunia mengi.Nikafungua na saloon ya kike kwa ajiri ya mke wangu,nikafungua na miradi mingine mbalimbali ambayo inazidi kuniingizia pesa kila kukicha.Karanga zimenitoa kimaisha.

USHAURI KWA VIJANA.
Using'ang'anie kukaa mjini wakati huna pesa. Kijijini ni dhahabu kama utajituma vyema na kuishi vizuri na watu.

AHSANTENI.

Usisahau kunipigia kura hapo chini.Bonyeza alama '^' kupiga kura.
Tatizo la JF ni kwamba watu wanaandika tu kitu chochote. Binafsi sipendi sababu ninachoandika chochote hapa kina ukweli 100%. Na mtu ukiniuliza picha muda wowote Ninazo. Sasa kweli umeshindwaje kupiga picha za magunia hayo Mengi unayoyauza? Na picha za hio saloon ya mkeo na picha nyinginezo? Mimi sitaki ku-juddge lakini story yako inaleta maswali mengi tunayojiuliza kuliko kutoa majibu na inaonekana haina ukweli ndani yake. Samahani lakini mkuu
 
Hii story angeweka muda kama miaka mitano ingenoga sasa hata mwaka haujafika umeanza kutajirika BIG NO
 
Back
Top Bottom