gambakuffu
JF-Expert Member
- Jul 2, 2010
- 422
- 414
Mkuu umenena vyema sanaMimi ni mwanaume lakini niseme ukweli. Katika nchi zenye wanaume wa hovyo hovyo, wavivu na saa zote wanawaza ngono wanapoona mwanamke ni Tanzania. Tuko nyuma kweli kweli na hatujui dunia inakokwenda. Na hali imekolezwa zaidi na mitandao kuingia. Watu wana approach kila wanayedhani ni mwanamke kwenye mtandao. Comments zimejaa sexism za kijinga na zilizopitwa na wakati. Habari ya nzuri yenye mafundisho mazuri ikiambatana na picha ya mwanamke watu wanakimbilia ku-comment kuhusu yule mwanamke na kuacha habari. Hii ni sehemu nzuri sana ya kuingiza kipato kwa wale matapeli wanaijifanya ni wanawake wanaotafuta wanaume.