Nilivyokwenda Afrika Kusini bila kuwa na Ndugu wala Rafiki kule

Keagan Paul

JF-Expert Member
Jul 19, 2018
366
1,000
Wakuu leo naomba kuleta Story yangu ya kweli ya jinsi nilivyokwenda South Africa bila kuwa na ndugu kule wala mtu wa kunipokea.

Ukweli kuna wakati ilifika nilichoka sana maisha ya hapa nyumbani, ilikuwa Mwaka 2014, nilikuwa napitia changamoto nyingi za maisha hasa katika familia. Ukweli akili ilikuwa imechoka sana ilisababishwa na kutokuwa na ajira muda mrefu.

Hata baadhi ya watu sikuwa napenda kukutana nao sana. Nikajiuliza kwani Maisha ni hapa tu nyumbani? kwani hakuna sehemu nyengine? Nikajisemea labda sikuandikiwa kutoboa hapa nyumbani ngoja nikajaribu bahati yangu sehemu nyengine.

Kabla ya kufanya maamuzi ya kwenda South Africa, Kwanza niliwaza kujaribu bahati yangu Marekani, nina ndugu kama watatu huko. Nikamcheki ndugu yangu mmoja akanitumia Invitation Letter. Nikaanza kupambana pale Ubalozini. Nilifika kwenye Usahili lakini nilikosa VISA.

 

Keagan Paul

JF-Expert Member
Jul 19, 2018
366
1,000
SEHEMU YA PILI

Nilivyokosa VISA pale Ubalozi wa Marekani, nikasema hapa ni South Africa tu. Nikajiuliza Je Nina Rafiki au Ndugu huko? Jibu hapana. Kwa kuwa nilikuwa nimechoka maisha ya hapa nyumbani, nikasema nikiendelea kusubiri mpaka niwe na ndugu au Rafiki South nitachelewa sana kwenda. Nikasema hapa najilipua.

Nikaenda mpaka Ubungo kwenye Ofisi za Bus la Taqwa kuulizia Nauli ya kufika huko ni kiasi gani. Nakumbuka wakaniambia Taqwa linafika mpaka Harare Zimbabwe kwa nauli ya Shilingi Laki Moja na thelathini. Nikauliza nauli ya kutoka Harare mpaka Joberg wakaniambia ni kama Elfu 50 za Kitanzania. Nikasema kama ni hivyo nikiwa na Laki Mbili na Nusu mpaka pesa ya kula nimepata. Nikauliza Safari inachukua siku ngapi, wakaniambia mpaka Harare ni siku 3, halafu Harare mpaka Joberg ni siku moja. Jumla ni Siku 4.

Swali likawa ni kiasi gani cha Akiba, cha kuanzia maisha huko napaswa kuwa nacho. Je Kiasi hicho cha Pesa nitakitunza wapi? Kwenye Begi? Maana safari ni ndefu, nikawa na hofu nikiweka kwenye Begi, safari yote macho yote yatakuwa kwenye Begi, vipi ikitokea Begi likaibiwa. Nikasema hapa nakwenda kufungua Account ya Benki. Niseme ukweli sababu ya kufungua Account ilikuwa kwanza kutunza hii Akiba yangu ya kuanzia Maisha huko. Pili, Niliwaza endapo nitafika huko halafu nisipate mchongo kwa wakati, Basi Account hii itanisaidia endapo nitaomba Msaada kwa ndugu au rafiki hapa Bongo itakuwa rahisi kwa wao kuniingizia pesa.

.
 

Keagan Paul

JF-Expert Member
Jul 19, 2018
366
1,000
SEHEMU YA TATU

Nikafanya research kidogo nikaambiwa Benki inayopatikana kwa urahisi huko South afrika ni First National Bank (FNB), Kwa hapa Dar es Salaam hii Bank ilikuwa na Tawi lake Posta. Nikaenda mpaka Posta, Nikafungua Account, Nikaweka Akiba Kama ya Milioni Moja. Huyo Nikasepa zangu na ATM Card yangu. Niliona ni Salama zaidi kwenye hii Safari kutembea na ATM Card mfukoni kuliko kutembea na Million Moja Mfukoni ukizingatia safari yenyewe ni ndefu na niendako sipajui na wala simjui mtu.

Siku ya Safari ikawadia, Huyo mpaka Ubungo. Ukweli ile hofu ya kwenda mahali nisipopajua, na sina Rafiki wala ndugu ilinitawala sana, sema nilikuwa nimechoka sana kuishi Bongo mpaka nikasema liwalo na Liwe. Unajua katika maisha kuna wakati mtu unachoka kuishi sehemu moja, kupiga story zile zile kila siku na watu wale wale.

Hivyo safari ya kutoka Ubungo kuelekea South Africa ikaanza. Kwenye Bus Watanzania tulikuwa kama nusu ya Bus zima, Abiria waliobaki walikuwa Wakenya, Waburundi walikuwa wengi, wanawake kwa wanaume. Pia kulikuwa na Wazambia na Waangola waliokuwa wakirudi Makwao.

Ukweli kabla ya Safari hii, Sikujua kama pale Ubungo huwa kunapokea wageni wengi kiasi hichi. Sikujua kama Tanzania ni njia kubwa sana ya kuelekea kusini mwa Bara la Africa. Sikujua kama tunapokea Waburundi wengi hivi, Kila kitu kilikuwa kigeni kwangu.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom