Nilivyokwenda Afrika Kusini bila kuwa na Ndugu wala Rafiki kule

Hawa jamaa huwaga wakisifiwa wanakula kona...
inatakiwa wamwage story kama bujibuji....
bujibuji akilianzisha mpaka mnakoma na story
ndio maana mwanzoni uzi unaanza nilimwambia aache Ufala.

napenda sana stories kama hizo...ila kusubiri naonaga ujinga shusha kitu kiishe...kuna mwamba alitupa story ya south jins alivyoponea kuuliwa na polisi alishusha episode moja ndefu sana story ikaisha

hawa nitarud sijui itaendelea wanaboa sana

Sent from my SM-N960F using JamiiForums mobile app
 
nanunua ugomvi mama...ole wake wapenda pajama waje kudiss

ulienda na basi au mwewe??

Sent from my SM-N960F using JamiiForums mobile app
Nilienda kwa bus, kupitia njia aliyopita mtoa mada nikarudi kwa mwewe. Njia Dom-Mbeya-tunduma (Nakonde border)-Lusaka-Chirundu one stop border- Beitbridge border moya kwa moya Jozi. Nililala tunduma boda, nikalala na kukaa Lusaka wiki, nikaongoza Jozi.

Kutoka tunduma nilipanda power tools mabasi fulani ya njano, Kutoka Lusaka nilipanda basi inaitwa Joldan kama sijakosea spelling, nalikumbuka tu ni la rangi ya zambarau.

Changamoto ya safari ya barabara, ni kuombwa rushwa uhamiaji, hata mimi niliombwa tunduma na chirundu, tena aliyeniomba chirundu ni mdada, wanasema kuwa ukionekana na passport ya kijani, lazima uombwe mpunga. ( enzi hizo ni zile pass zetu za kijani) Sijui kwa sasa.
 
SEHEMU YA NNE

Kwenye Bus kama kawaida ya Watanzania tulianza kufahamiana na kupiga story za hapa na pale. Wengi wetu ilikuwa ni mara etu ya kwanza kwenda South isipokuwa jamaa mmoja alituambia anaitwa Ahamad yeye ndo ilikuwa kama mara yake ya Tatu kwenda huko na Kuna Dada aliitwa Matlida, ni mtu wa Mbeya ila yeye ilikuwa anaishi South Miaka Mingi. Hata kwenye hii Safari yeye bus alikuja kupandia Mbeya.

Tulifika Boda ya kwanza Tunduma Majira ya saa Sita Usiku. Kulikuwa na Baridi sana. Ukweli Wakuu nitaahadithia kila kitu kama kilivyotokea. Tulivyoshuka pale Tunduma tulipokelewa na Vishoka wengi sana waliokuwa wanakimbilia Abiria ili kuwapa Msaada kwenye zile Ofisi za Uhamiaji. Vishoka walikuwa wengi sana tena walikuwa wanajiamini sana na kuingia mpaka ndani ya Ofisi za Uhamiaji.

Ukweli nilishangaa sababu nilishawai kufika Boda ya HoroHoro kwa Upande wa Tanga, Nilishawai kufika Boda ya Sirari kule Tarime, Boda ya Namanga Arusha pia naifahamu lakini sikuwai kuona Vishoka wanaingia mpaka ndani ya Ofisi za Uhamiaji kama vile unaweza kudhani wao ni Maafisa Uhamiaji.

Niligonga Mhuri wa EXIT kwenye Passport yangu upande wa Tanzania kisha nilikwenda kugonga upande wa Nakonde Zambia. Nakumbuka nilivyofika kwenye ile Kaunta ya yule Dada wa Uhamiaji Upande wa Zambia alinikatalia kugonga muhuri kwa madai kwamba nimuoneshe kama Nina Balance ya Pesa ya kutosha ya kuweza kuishi South Africa. Alisema hayo ndo Matakwa ya Sheria. Kwa wakati ule sikujua kama alichosema ni kweli ama La. Nilimwambia yule Dada kuwa Pesa ninazo kwenye Account ila alikataa, alihoji nina uhakika gani kama kweli kwenye Account una Pesa? Niliwaza labda nilipaswa kutembea na Bank Statement lakini ndo ivo nimeshachelewa.

Yule Dada alivyokataa kunigongea nikasogea pembeni ya ule mstari kupisha wengine waendelee. Nikaona Vishoka kama watatu hivi wananifuata kuniuliza nini Tatizo, Nikawaeleza kuwa yule Dada amekataa kunigongea mhuri. Mmoja ya wale Vishoka nakumbuka akaniambia kazi ndogo sana hiyo, akaingiza mkono wake mfukoni akanipa Kwacha 50 pesa ya Zambia. Akaniambia chukua hii pesa mdogo wangu weka katikati ya Passport yako kama Rushwa halafu rudi tena kwa yule Dada. Nikafanya kama alivyoniambia.
Nimependa asee katika Utaftaji
 
Nilienda kwa bus, kupitia njia aliyopita mtoa mada nikarudi kwa mwewe. Njia Dom-Mbeya-tunduma (Nakonde border)-Lusaka-Chirundu one stop border- Beitbridge border moya kwa moya Jozi. Nililala tunduma boda, nikalala na kukaa Lusaka wiki, nikaongoza Jozi.

Kutoka tunduma nilipanda power tools mabasi fulani ya njano, Kutoka Lusaka nilipanda basi inaitwa Joldan kama sijakosea spelling, nalikumbuka tu ni la rangi ya zambarau.

Changamoto ya safari ya barabara, ni kuombwa rushwa uhamiaji, hata mimi niliombwa tunduma na chirundu, tena aliyeniomba chirundu ni mdada, wanasema kuwa ukionekana na passport ya kijani, lazima uombwe mpunga. ( enzi hizo ni zile pass zetu za kijani) Sijui kwa sasa.
kwann ulikaa lusaka week...au uliamua??

au kuna kitu kilikukwamisha

Sent from my SM-N960F using JamiiForums mobile app
 
Afu Roadtrip inakua tamu kama hamjazidi watatu hivi, huku mko kwenye hata defender ina tent lenu juu, ndani mna soft drinks plus maboksi ya ceres kibao, unagonga huku unachungulia grants zako kwa jicho la mafanikio, maji katoni kadhaa, ngoma inaanzia songea inapumua kidogo makambako unachoma kuku kizushi then inajaza mafuta, gari inawekwa kwa mexisons inapigwa povu kiaina, ikikamata highway inakuja kusimama Dom kidogo, inanunua wine za bei ya jumla, inaamsha kwenye nyama bahi kidogo unakula mbuzi na whisky funda mbili tatu, ngoma inaenda kulala manyoni kuna lodge za maana, hapo asubuhi inakamta supu ya kuku wa kienyeji then inatembea vumbi vumbi inakuja kula Tinde hapo unapumzika gari unafungua milango yote ipate hewa vizuri, baadae. Ikitoka tinde ngoma inasound hadi kahama unashangaa phantom kidogo unapita masumbwe, Ushirombo, Runzewe ngoma inapandisha Bwanga, inakula geita unaenda kulala hapo kwanza unasoma upepo haya mbele utaendelea mwenyewe
Mwongo mkubwa wewe, eti Manyoni - Tinde unakula vumbi kidogo, wapi hapo? Halafu ramani ya Bwanga-Geita unaenda wapi huko? (Mkuu huu ni utani usije ukanirarua). Halafu nyie si ndio mmetangazwa bungeni hamna nguvu za kiume? Kumbe ni hayo mavyakula yenu mnayokulakula njiani eeeeh?
 
Naomba ufafanuzi huwa naona hizo T1, A1, N2, kwenye vibao barabarani, huwa na maana gani!?
Hizi ni freeways au highways na inategemeana kati ya nchi na nchi mfano N(ni national roads ndani ya SA)na kuna N1 hii ni Beitbrige hadi cape town;N2 hii ni cape town hadi Durban,N3 hii ni Durban to Jhb etc etc vile vile wana Rs hizi zipo chini ya local governments:T1 hizi ni freeways za nchini hapa from T1 ni kutoka Tunduma hadi Dar na As hizi ni freeways za Botswana. Wengine wataongezea mkuu
 
Mwongo mkubwa wewe, eti Manyoni - Tinde unakula vumbi kidogo, wapi hapo? Halafu ramani ya Bwanga-Geita unaenda wapi huko? (Mkuu huu ni utani usije ukanirarua). Halafu nyie si ndio mmetangazwa bungeni hamna nguvu za kiume? Kumbe ni hayo mavyakula yenu mnayokulakula njiani eeeeh?

Mkuu mbona unanishambulia, Bwanga ukiacha kuelekea chato, unaenda katoro Buseresere/ katoro geita, sengerema, mwanza, mwanza unaweza kuamua uende Musoma then upite mbugani serengeti ili utokee geneva of africa, au urudi utokee Bariadi/simiyu uingie Arusha kupitia loriondo. Bado unaswali? Kule juu nimetaja njia ya Runzewe lakini unaweza kukatisha njia ya vumbi ushirombo kutokea katoro ukaendelea na safari zako
 
Mwongo mkubwa wewe, eti Manyoni - Tinde unakula vumbi kidogo, wapi hapo? Halafu ramani ya Bwanga-Geita unaenda wapi huko? (Mkuu huu ni utani usije ukanirarua). Halafu nyie si ndio mmetangazwa bungeni hamna nguvu za kiume? Kumbe ni hayo mavyakula yenu mnayokulakula njiani eeeeh?

Nakupa route kidogo kwa maandishi, Mbeya To Tabora kupitia chunya, makongorosi, unafika Rungwa unachoma kuku na mtungi kidogo baada ya hapo break kidogo kitunda mgodini ukanyage hadi ipole, then sikonge ndio ufike Tabora tumsubiri keagan hapa tukipata wadhamini kidogo
 
Back
Top Bottom